Kwanini Balozi Mulamula alikuwa anaonekana smart sana na kuheshimika huko Ugenini?

Komeo Lachuma

JF-Expert Member
Oct 31, 2014
5,341
11,443
Nimeshangaa sana yeye ni kwanini alikuwa anapafa fursa hizi? Jamaa yangu mmoja yupo USA.

Anasema huyu dada alikuwa anaheshimika sana na walikuwa wanamwona very smart hata katika maongezi. Anasema ni nadra sana kwa mtu ambaye haheshimiki kuonana na akina Obama na Biden namna hii.

Kuna watu tena Marais huenda kule na kukaa hadi mwezi hawajapata nafasi hata ya kukutana na Biden kwenye korido katika meetings zake.

Screenshot_2022-10-03-15-27-19-061_com.twitter.android~2.jpg


Screenshot_2022-10-03-15-27-23-335_com.twitter.android~2.jpg
 
Nimeshangaa sana yeye ni kwanini alikuwa anapafa fursa hizi? Jamaa yangu mmoja yupo USA.

Anasema huyu dada alikuwa anaheshimika sana na walikuwa wanamwona very smart hata katika maongezi. Anasema ni nadra sana kwa mtu ambaye haheshimiki kuonana na akina Obama na Biden namna hii.

Kuna watu tena Marais huenda kule na kukaa hadi mwezi hawajapata nafasi hata ya kukutana na Biden kwenye korido katika meetings zake.

Nimekuelewa sana yaani !
 
Kama wazungu walikuwa hawamuelewi Samia kwasababu ya kuwa makamu wa Rais wa Magufuli aliyeharibu uhusiano wetu wa kimataifa, huyu mama alikuwa kiungo mzuri sana.

Kwenye mazingira kama haya kuleta habari za "collective responsibility" ni ujinga mtupu, hiyo "collective responsibility" ndio iliharibu mwanzo ikashindwa kumshauri vizuri yule aliyeharibu, then unamteua anayeaminika huko nje ili akatengeneze, ajabu baadae nae unamuondoa kwasababu ya kukumbatia mawazo ya wale waliofeli!.

Huyu mama alikuwa anatengeneza connection nzuri ya kurudisha imani ya wazungu kwa Samia na serikali yake, lakini kwa kuondolewa kwake, naona Samia ataendelea kupokewa na kina Mange kila akienda US.
 
Mtu yeyote anaweza akapewa nafasi, na nafasi ikambeba. Kwa mantiki hii, kwa hapa duniani hakuna mtu ambaye ni spesho kwa nafasi yoyote. Hata wewe hapo ulipo, unaweza ukapewa nafasi, na ukatimiza majukumu yanayotakiwa.
 
Kwa hiyo sisi watoa mada na wachangiaji ndo tunayajua mengi sana kuhusu uongozi husika,haya jamani sisi tupo seblen na wengine wapo kibarazani,waliopo jikoni ndo wanajua ya kuwa unga umezidi maji au maji yamezidi unga,chumvi hamna au ipo,na vipi kuhusu viungo vyengine,tutulie tu hapa tulipo tuendelee kuangalia drama na maisha mengine kwa ujumla ya watu kuuana kisa mapenzi,kisha tuletewe chakula hapo hapo tulipokaa tule tuondoke.

Na maanisha ya jikoni tuwaachie wapishi.
 
Pamoja na madhaifu yote ya viongozi wetu ila hata wao kuna point wakifika wanaweka maslahi ya nchi mbele ndo maana hadi leo TZ ni salama kwenye mipaka yake na hakuna shinikizo kubwa toka kwa wageni. Huyu mama inavyoonekana aliegemea kwa mabeberu zaidi. Wazungu ukiwa na maslahi nao hawana noma hata chai utaitwa kunywa nao... hiyo ndo style ya bepari.
 
Back
Top Bottom