T2015CCM
JF-Expert Member
- Sep 13, 2012
- 7,931
- 987
Mkuu sasa endapo mwalimu Nyerere angemteua Kinana ktk nafasi kubwa kama hiyo hujui kama tembo wetu wangeisha?
kama yule mzee alivoteuliwa pale sasa wake zetu wanaisha
Mkuu sasa endapo mwalimu Nyerere angemteua Kinana ktk nafasi kubwa kama hiyo hujui kama tembo wetu wangeisha?
me naona unajadili ujinga tu, sasa Uraia wa kinana na CCM wapi na wapi bwana, Kinana ni Raia wa Tanzania na hata kama asingekuwa Raia wa Tanzani basi asingeweza kuwa katika Jeshi la Tanzania na hata kama angezaliwa Somalia akaja kuishi Tanzania na kupata Uraia wa TZ hakuna ubaya kuwa kiongozi, sio kwa sababu hakuchaguliwa na Nyerere basi ndo awe hafai sasa si muda wake hujafika kwani wangapi Nyerere hajawachagua na leo viongozi?? Kwan lazima kiongozi achaguliwe na nyerere?? Yeye Nyerere kwani Nchi ya baba yake au ya kwake??? Hii Nchi ya Watanzania bwana na wala haiitwi Nchi ya Wananyerere kwa hiyo stop kutpa fikra mgando, na Uteuzi wa Chama chochote cha siasa watajua wenyewe kama wewe Chadema ya CCM ya nini??? Acheni kuzingua bwana me sioni Tatizo la Kinana mwacheni mwaka wake Nyota imeng'aa acha ale Bata.
Kila mtu na msimu wake, yuko wapi Mrema mbona aliwika sana kipindi cha Mkapa na upinzani mkubwa lakn sasa hivi hana upinzani, so mambo yanabadilika hata Chadema sasa hivi ndo chama chenye Upinzani sana lakin baadae kitakuja chama kingine wala usijal ni mabadiliko tu. tulia kama moja
Baada ya uteuzi wa Sekretariati mpya ya Chama Twawala-CCM na Kinana kuibuka kama Katibu Mkuu mpya wa CCM kwa mara ya kwanza watu wamesifia sana uteuzi huo kutoka kila kona ya nchi hii hasa wanachama wa Chama Cha Mafisadi-CCM.
Mimi nataka tu niwakumbushe hawa wanachama wachovu wa CCM kwamba Kinana alikuwepo tangu enzi za Baba wa Taifa lakini hakuwahi kupewa wadhifa wowote ndani ya TANU wala CCM. Hapa ndipo mahali pakuanzia kutafakari uteuzi huu wa Kinana. Abdurhaman Kinana alikuwa mwanajeshi wa cheo cha Kanali mpaka alipostahafu mwaka 1972 baada ya kuitumikia JWTZ kwa miaka 20 tu. Baada ya hapo hakusikika tena kwenye medani za siasa wala za Jeshi. Sikumbuki hata kamaalishiriki vita vya Nduli Iddi Amini miaka ya 1978/79 sina hakika!!!
Bila shaka Mwalimu(Baba) wa Taifa hili alikuwa akimjua Kinana vizuri sana kuanzia URAIA wake,UZALENDO wake kwa Tanzania na WELEDI wake katika siasa za Tanzania. Nina hakika Mwalimu alikuwa anajua vizuri sana kuhusu URAIA wa Kinana ambaye hapana shaka huyu jamaa ana ASILI ya SOMALIA. Hili mwalimu alilijua na ndiyo maana hakuwahi kumpa nafasi yoyote kubwa katika nyanja za kisiasa maana KINANA'S CITIZENSHIP IS QUESITIONABLE!!!!
Sasa napenda kuwauliza Wana CCM na mwenyekiti wao Kikwete huyu Kinana amepata wapi uzalendo wa kuwa Katibu Mkuu wa Chama chenu cha Mafisadi???Je, wanaweza kututhibitishia pasipo shaka kuwa Kinana ni Raia halisi wa Tanzania? Je, katika vita vya kumwoa Nduli Idd Amini, huyu Kinana alikuwa wapi maana hata kama alistahafu Jeshi mwaka 1972 nijuavyo sheria za Jeshi mahali popote duniani vita vikiripuka hata wanajeshi waliostahafu huitwa kuungana na wenzao ili kuitetea nchi yao. Now CCM tell us Kinana's role in the Tanzania/Uganda war!
Nje ya hapo Kinana hafai kuwa Katibu Mkuu wa Chama chenu cha Mafusadi maana hana Uzalendo wa nji hii.
Nawasilisha.
Mkuu,
Ni vizuri sana kujua historia sahihi ya mhusika kabla ya kumjadili.
Pili, mambo ya kuambiwa, changanya na akili yako ili kujiridhisha. Hivi kwa Kinana huyo unayemwona unaamini kweli alistaafu jeshi mwaka 1972 baada ya kulitumiakia miaka 20? Ina maana aliingia jeshi mwaka 1952? Kama hilo ni kweli basi aliingia jeshi akiwa na umri wa mwaka mmoja.
Kuanzia miaka ya 70 mpaka Nyerere anastaafu, Kinana alikuwa political commissar jeshini. Hao enzi hizo wlaikuwa kama ni walimu wa siasa jeshini. Hizo zilikuwa ni nafasi za chama cha TANU ndani ya jeshi.
Nyerere amestaafu Kinana akiwa kijana kabisa chini ya miaka 35.
Mijadala inakuwa mizuri pale tunapojadili ukweli na sio habari ambayo sio sahihi. Sisi kwenye technology tunasema garbage in garbage out. Kwasababu premise uliyoanza nayo kwenye mjadala huu sio sahii ina maana hata majibu yake au conclusion yake itakuwa sio sahihi.
Mtanzania,
Uko sahihi kwa hili. Hata hivyo katika kuchanganya akili zangu na za Absolom Kibanda nilijaribu kutafuta habari za Kinena kwenye search engine kama alizaliwa mwaka gani,alisoma wapi na aliajiriwa lini jeshini mpaka kustahafu kwake sikupata!!!
Kama wewe una taarifa sahihi za Kinena ziweke hadharani ili tujue huyu jamaa ni nani hasa katika siasa za Tanzania na kwanini Baba wa Taifa hakuwahi kumpa madaraka makubwa ya kuongoza TANU na baadaye CCM! Watanzania wanahaki ya kujua undani wa Kinena ili kujenga imani naye au kumtosa!