Mystery
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 15,480
- 30,152
Kama tulivyomsikia majuzi, wakati anakutana na viongozi wa vyama vya siasa nchini huko Ikulu, Rais Samia Suluhu Hassan, alitoboa Siri kuwa haikuwa rahisi kufikia Maridhiano na chama kikuu Cha upinzani nchini Cha Chadema, Kwa kuwa pamoja na nia yake njema ya kuleta Maridhiano ya kisiasa nchini, lakini baadhi ya wasaidizi wake, walimshauri akatae kukutana na viongozi wa Chadema!
Ikumbukwe kuwa ni chama Cha Chadema pekee, ambacho kilitoa masharti ya kukutana peke yake, bila kuvishirikisha vyama vingine vya upinzani.
Kama alivyosema Rais, baada ya watu kuumizwa Sana na utawala wa awamu ya 5, lengo lake la ni kuleta umoja na mshikamano nchini Kwa lengo la kuleta maendeleo endelevu na lengo la kukutana na viongozi wote wa kisiasa nchini ni kuleta umoja na mshikamano wa kitaifa,.
Je ni kwanini baadhi ya wasaidizi wake hao walipinga, viongozi wao wa CCM wasikutane na viongozi wa Chadema?
Hizi hapa ni baadhi ya hisia zangu, kwanini baadhi ya viongozi hao waandamizi wa CCM walimpinga Rais, asifanye maridhiano na Chadema.
1. Inajulikana wazi kuwa chama kikuu Cha upinzani nchini Kwa hivi Sasa ni chama Cha Chadema, viongozi hao walipinga kukutana na chama Cha Chadema, Kwa kuwa Wana misimamo wa kihafidhina, wakijua wazi kuwa chama Chao ni chama dola, Kwa hiyo vyama vya upinzani nchini, havina ubavu wa kupambana nao
2. Viongozi hao walipenda namna Rais wa awamu ya 5, Hayati Magufuli alivyoiendesha nchi, bila kufuata Sheria za nchi (ikumbukwe kuwa mikutano ya kisiasa nchini ni takwa la kisheria na Wala siyo hisani Kutoks Kwa Rais aliyeko madarakani)
3 Viongozi hao Kwa namna nchi ilivyokuwa ikiendeshwa, walifurahia hali hiyo, Kwa vile walikuwa wakiendeleza kufanya maovu, wakijua kuwa vyama vya kisiasa vya upinzani nchini vyenye uwezo wa kukemea maovu yao vipo "kifungoni"
4. Viongozi hao walikuwa wakifurahia kula Kwa urefu wa kamba zao, Kwa hiyo walijua fika kuwa kuleta Maridhiano nchini, kutawapunguzia "ulaji" wao
5. Viongozi hao walikuwa wakifurahia mitafaruku hiyo, Kwa kuwa chama Chao ni chama dola, Kwa hiyo walijua kuwa vyama vya upinzani havina ubavu wa kufurukuta Kwa kuwa chama Chao dola, kingeweza kuvitumia vyombo vyake vya dola, kuweza kuwashughulikia viongozi wa vyama vya kisiasa vya upinzani, endapo wataleta "fyoko"
6. Wao CCM hawakuona athari yoyote ya zuio hilo la mikutano ya hadhara, Kwa kuwa tulishuhudia viongozi waandamizi wa CCM (wakipewa upendeleo maalum) wakizunguka nchi nzima, bila kizuizi chochote wakimwaga sera zao!
Kwa kuwa Rais Samia alikuwa na nia ya dhati ya kuleta Suluhu nchini, hizo ni baadhi ya hisia zangu, ni kwanini baadhi ya wasaidizi wake walipinga vikali hatua zake za kuleta Maridhiano hapa nchini.
Kama na wewe msomaji wa hii post, utakuwa na sababu zako, ni kwanini baadhi ya wasaidizi wa Rais walimpinga Rais, asilete Maridhiano nchini, naomba "uzi-add" hapa
Mungu ibariki Tanzania