Kwanini baadhi ya wanaume hamuwapendi Feminists?

Status
Not open for further replies.
unafikiri hizo equality of sexes economically, politically and socially inawezekana for 100%..au ni theory tu?

hapa mjadala umejikita sana kwenye home affairs kwa maana ya majukumu ya mke ndani ya nyumba na mwanamme ndani ya nyumba, wengi unaosema wanakufokea wanaongelea ukuu wa mwanaume ndani ya nyumba based on his hard responsibilities kama baba kwa familia hapa ndipo anatakiwa aheshimiwe..

Imani za kidini zimempa mwanaume ukuu wa familia kama baba na mama ni msaidizi aka mshauri na mfariji kwa baba zikibase kwenye mahangaiko anayoyapata mwanaume kwenye maisha ya kila siku..
Uumbaji pia umeampa mwanaume vitu vinavyomfanya awe na nguvu kwenye familia kwa yeye kuweza kupambana kwenye hali zote ngumu ili alete mkate mezani na aweze pia kuilinda familia ndio maana kazi ngumu zote duniani for 90% wafanyaji ni wanaume..

Usawa kwenye familia upo kiasili kwenye upande wa majukumu ya mwanamme na mwanamke, mwanamme ana yake na mwanamke anayake na hii iko automatic ukienda tofauti lazima shida itokee..Ukiangalia majukumu ya asili ya mwanamme ni makubwa na magumu ukifananisha na ya mama ndio maana mume akirudi atapewa pole na usiku wakati wa kwichikwichi mtapeana updates za siku based majukumu ya kila mtu..

Nilivyokuelewa uko na shida kwenye vitu vidogo sana ambavyo kimsingi karne ya sasa sio issue mfano kutekeana maji, kupika sijui kufua nk hivi ni vidogo na sio issue mwanamme kusaidia inapobidi au kuweka nyenzo rahisi umpunguzie mkeo kazi...

Yapi ni majukumu ya mume na yapi ni majukumu ya mke kwenye familia?
Nilivyokuelewa, hakuna majukumu ya mke wala mume wote lazima mkubaliane huyu atende kile na wewe utende kile, hapo binafsi sidhani kama kuna mume na mke..

sorry kwa mkeka mrefu, somo ni refu sana hili kulielewa...
Ndio maana from beggining I said watu wanachaganya hyo concept ya feminism na Mambo ya relations za maisha zinazoendelea kwenye maisha na watu hawajui in deep hii kitu na hyo feminism wakakimbilia kutukana tu maana majority hawajui hata gender equality ni Nini and I advised watu ku read kuhusu hii concept vizuri wakaja na matusi, mtu kashabeba na maandiko as defend mechanism bila kuelewa vizuri na hata hyo feminism imetofautiana Kuna liberal feminism, critical third world feminism, radical feminism and even African feminism, hizo ni concept zinatofautiana, na hata hivo hata mwanaume anaweza kuwa faminist vile vile.
Sasa wanaume wengi au jamii ya kitanzania wanaamini mwanamke akigombana na mumewe tarehe ni feminist, mwanamke akitafta hela tayari ni feminist, watu wakishindwana kwenye mahusiano tayari ni feminist kumbe Hali sio hivo.
Naweza kubishana na watu hapa Hadi kesho na Mimi sio feminist, naweza kuwa much know lakini sio feminist vile vile maana hizo ni tabia tu ya mtu ka walivo waomgeaji Sana, wakimya, machepele Sana, so msipende ku confuse feminism na hivo vitu maana Ni vitu tofauti.

Halafu pia mabadiliko mengi yaliyotokea yamekuja ghafla Sana na wanaume hamkuandaliwa hasa hizi globalization so wanaume mumekuwa ka mmepigwa shot flani Sasa mna blame wanawake hata mkitofautiana ugomvi wa kawaida you term it feminism kumbe sio sawa, na nyie mulilelewa ili muwe vidume lazima mumutese mwanamke, mumuonee, hata akitoa wazo zuri hamtaki kisa ni mwanamke, hicho ndio kinachowatesa wanaume Hadi kunifokea mitusi humu.
 
Pia katika issue ndogo kama za kupika,kufua, kupiga deki na kuosha vyombo mimi sioni ubaya wa wmanaime kuwa unafanya siku mojamoja maana naamini feminist wenyewe sio kama wanataka mtu afanye hivyo sikuzote ila tu afanye siku chache.....it looks good kwa familia siku mojamoja kids wanaona baba anapika anaosha vyomho, it sound more family pia....
 
Mwanamke mbishi wwe kha
toka asubuhi unapambana tu,....
nikikushika nitakupigia bakora tatu....
uimbe nyimbo zote za kwenu.....
na asubuhi uniamkie...
utanishikia wapi Sasa siku nikiwa free nikushinda tu humu kabla Mambo hayajawa busy tena
 
Pia katika issue ndogo kama za kupika,kufua, kupiga deki na kuosha vyombo mimi sioni ubaya wa wmanaime kuwa unafanya siku mojamoja maana naamini feminist wenyewe sio kama wanataka mtu afanye hivyo sikuzote ila tu afanye siku chache.....it looks good kwa familia siku mojamoja kids wanaona baba anapika anaosha vyomho, it sound more family pia....
safi sana kaka kila mtu na sheria zake hapa mjini.

Piga sana deki kwanza vifaa vya deki ni vya kisasa sana..
 
kazi pekee ya kumsaidia mwanamke ni kumbebea mtoto ili akapike tule..

kumpasulia kuni..

kutandika kitanda wakati akiwa bafuni anaoga, baada ya hapa tunacheza mechi..

sina zaidi
 
Hata nikizeeka Kuna shida nilizaliwa kufanya makubwa zaidi kuliko kufanya vitu visivo happy, Kuna watu wameoa, olewa with nothing to show zaidi ya viungo vya uzazi ambavyo kila mtu anacho.

So depending na uelewa wa mtu na mipango yake
Taratibu dada usikashfu watu.... nahisi wewe ni below 30yrs. Jipe muda......
 
Habari?

Hebu Leo semeni ni kipi ambacho kinafanya mchukie feminism? Hamjiamini? Au mnaogopa kutawaliwa? Kuna tatizo gani mwanamke akijua haki zake na kuzisimamia?
Ni kwa sababu they can't withstand criticism. Sehemu ninakotoka kulikuwa na mkuu wa nyumba ya watawa wa kike (masista) - mother superior - alikuwa 'very assertive' akiongea na baadhi ya watu walikuwa wakisema "sijawahi kuona sista anayeongea kama mwanaume!" Alikuwa akitoa hoja critically and constructively. Hakumwogopa mtu. Binafsi napenda sana watu wa aina hii kwa sababu wananifanya nifanye 'homework' yangu. Hata mke wangu sitaki awe mtu wa "ndiyo...ndiyo" maana mtu wa namna hiyo ananifanye nijisikie vibaya kwamba hawezi kusema kitu cha moyoni mwake kwa kuogopa kuwa ndoa itavunjika au nitamfukuza nyumbani. Binafsi napenda mtu aseme "hapana" kama ana sababu ya kusema hivyo au "ndiyo" kama ana sababu ya kusema hivyo pia.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom