Kwanini baadhi ya taasisi na mashirika ya umma ajira zao hazipitii Sekretariet ya Utumishi?

Hawatoki nje ya mliofanya nao oral, Hawa wanapitia process zote
Kwa hiyo hapo kwenye Oral ndipo figisu zinakoanzia, au siyo? Halaf hivi PSRS huwa wanaajiri wao au taasisi inayohitaji employees ndo yenye final say?
 
Kwa tz hii ni heri ukose vyeti ila uwe na connection.nakumbuka tulienda oale maktaba house kwa ajili ya interview moja hivi OSHA. Kumbe mtu wao wanamjua na ikishapangwa kitambo.Watu tunasubiri majibu tulikuja sikia mtu alishaanza kazi kitambo na mpka leo hii utumishi hawakutangaza matokea ya ile interview.

Sent using Jamii Forums mobile app
Yeah zile nafasi za mtu 1 ni heri usiende kama huna connection!
 
Aisee nilibahatisha kupata nafasi ya buildup capacity kwenye moja ya taasisi ya Umma usiombe Manager anakaba kinoma sema kinachosaidia siku hizi ukipata chance maboss wanajua ni pandikizi kutoka juu so kukutimua kizembe wanaogopa, but ninachokiona kwasababu sina connection nikimaliza programme yangu niende tu kitaa nikapambane.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hili mpaka rais analijua ndo maana siku ile alimchana naibu waziri wa mambo ya ndani nafasi 11 alikuwa anapeleka jamaa zake,magu akacancel.
Habari zenu wanajamvi,
Naungana nanyi wote mlioko Tanzania kwa msiba wa kijana mwenzetu Ruge..! Hakika kazi yake ya hapa duniani ameimaliza na mungu ailaze roho yake mahali pema peponi,

Pia naona kwenye mitandao ya kijamii habari za kurudi nyumbani kwa mzee EL poleni pia mlioguswa kwa namna yeyote na huu uamuzi wake(Kama taarifa zitakuwa ni sahihi).

Niliahidi wiki ijayo siku ya alhamisi nitaleta humu uzi wa kuelezea fursa mbalimbali zilizoko nje ya nchi kwa wale watafutaji wanaoingia kihalali hili mpaka mda huu uzi ushakamilika unasubiri siku tu urushwe humu.

Leo naomba kuzungumzia ubovu uliopo kwenye michakato ya ajira unaowapa ugumu watoto wa maskini katika baadhi ya taasisi na mashirika ya umma na jinsi wakuu Hawa ambao michakato ya ajira ya taasisi zao haipitii utumishi wanavyopeana ajira kwa kujuana, ninayozungumza nina uhakika nayo kwa asilimia zaidi ya 100 maana nimefanya kazi serikalini kabla ya kuacha na kwenda nje ya nchi na nilipata kujenga connection na taasisi nyingi za serikali kwa nature ya kazi niliyokuwa nafanya hivyo Siri nyingi nilizijua.

Tangu psrs ( Sekretariati ya ajira) ianze kuratibu michakato ya ajira kwa taasisi na mashirika ya umma,. Urasimu na udanganyifu umepungua kwa kiasi kikubwa ( sio kwamba psrs haupo urasimu upo, huu urasimu nitauzungumzia siku moja), Leo nazungumzia hizi taasisi ambazo ajira zake hazipitii utumishi.

Kuna mashirika na taasisi ambazo ajira zake hazipitii utumishi Kama TANROAD, TANAPA, HIFADHI YA NGORONGORO, TANESCO, TPDC,WCF, NSSF, na hayo mashirika yaliyounganishwa kuunda (PSSSF) pia Kuna BOT, EWURA, TAKUKURU ziko nyingi Mimi nazungumzia hizi nilizo na uzoefu nazo.

Hawa BOT Kama hauna connection pale ya kukufanya ujulikane Basi hata wakikushortlist utaenda kukamilisha ratiba tu, nafasi zikitoka pale wanaanza kuulizana wao Kama Kuna mtu ana ndgu anakidhi vigezo then wanakuscreen kwa vimemo kwa watu wote wanaohusika na huo usaili ushahidi ninao sihitaji kuuweka wazi kwa watu walioingia hapo BOT kwa mlango huu, inaweza fanya wakanijua mapema maana wengi ni watu wangu wa karibu.

Kuna Hawa TANROAD ( Hawa ni warasimu kwelikweli kwenye masuala ya ajira) kwa nature za ofisi zao hasa mikoani kote isipokuwa makao makuu Hawa ofisi zao zinakuwa jengo moja na ofisi za Temesa, TBA, TAPE na pia huwa zinapakana na GPSA na kwenye hayo magodauni ya GPSA utazikuta ofisi za MSD wamepanga humo kwa ukanda wa ofisi hizi wafanyakazi wa TANROAD na MSD ndo huonekana matawi ya juu kwa sababu wanalipwa vizuri, Safari nyingi wanapata ikiwa wafanyakazi wa ofisi zingine Kama TAPE,TBA TEMESA, na GPSA wako hoi bin taaban ( labda kwa mfanyakazi wa GPSA kituo Cha mafuta huyu Yuko njema), hivyo hii inawafanya wawe wababe kwenye ukanda wa ofisi hizi, Hawa huwachukua ndgu zao au watoto wa kike wazuri waliohitimu vyuo wanawafanya vimada wao then wanawaweka kwenye ofisi wakiwa kama wafanyakazi wanaojitolea then nafasi za kazi zikitoka TANROAD mkoa wowote ule wanaanza kuwafanyia connection Kama mkoa husika uliotangaza hakuna mtu aliye ndani anafiti vigezo, kasheshe linakuja Kama huna mtu wa kukushika mkono hata nafasi ya kujitolea hupati labda uwe msichana mrembo then wakwere wakuone ukikubali masharti Yao Basi hapo utaula, MSD na TRA zamani nao walikuwa na tabia hii baada ya michakato ya ajira yao kuhamishiwa Psrs urasimu kwenye taasisi hizi umepungua.
Ushahidi wa taasisi hizi ninao na kwa kifupi fuatilieni ajira zilizotoka mwaka Jana mikoa ya tanga, njombe na Kilimanjaro, kigoma na ruvuma na kwingineko
Hawa ni watu ninaowajua na jinsi walivyopata kazi najua kwa hiyo najua ninachokiongea kwa zaidi ya asilimia 100

TANESCO Hawa ndo walewale ukiona umepata nafasi ya kazi hapa basi ujue wamemtafta wa kumuweka wamekosa, Tena Hawa wameenda mbali mpka nafasi zao za kazi Mara nyingi huwa wanatoa Kama "INTERNAL ADVERTISEMENT" tabia hii walikuwa nayo pia TPA kabla ya michakato Yao kuhamishiwa psrs, ili kuwapa nafasi watu wao waliowaweka kujitolea, Yaani hapa utakuta baba meneja, mtoto dereva, mwipwa afisa ugavi, binamu mhasibu hawaachani na TANAPA, Hifadhi ya ngorongoro na WCF ( kwa Sasa Hawa ndo wanaolipa vizuri + malupulupu kwa taasisi za serikali) Wala NSSF.

Hizi tabia zinachangia kuwafilisi watoto wa maskini just Imagine haya mashirika yanatoa nafasi labda Kilimanjaro, mtu Yuko ruvuma Hana nauli anauza mifugo au anakopa kwenda usaili ambao wenye michakato ya ajira wanajua nani mshindi wa kazi husika.

Pia hivi vibali wanavyopewa mameneja wa taasisi kuajiri watumishi wa mikataba nashauri hapa kuwe na utaratibu mzuri. Nakumbuka ilishawahi kufanyika ofisini kwetu kulikuwa Kuna upungufu wa madereva, phone operator, mhasibu,mgavi na mhudumu wa ofisi kwa uhitaji wa watumishi Hawa tulipewa kibali tuajiri ajira za mikataba, mimi nilianda tangazo then likasambazwa kubandikwa kwenye ofisi za serikali ili watu waone waweze kuomba ilikuwa mwaka Jana na kweli watu waliomba wengi, tukaita wote usaili ukafanyika na meneja alikuwa sauti ya mwisho kwenye hizi ajira Cha kushangaza watu walioitwa kuanza kazi wote ni ule mkoa anaotoka boss, siku zilivyoenda tukaja kugundua kumbe ni jamaa zake, na hii iko karibia ofisi zote za umma kwenye hizi ajira za vibali maalumu wanawekana kwa undugu na ujamaa na hapa ndo MAUMIVU yanapokuja kwa mtoto wa mkulima na maskini ambaye kwenye familia anakuwa hana mtu wa kumuongoza.

Nini kifanyike:

Ajira zote za serikali na mashirika yake zipitie Sekretariati ya ajira katika utumishi wa umma watu washindanie huko, haina maana ya kuundwa chombo hiki halafu taasisi zingine ziendelee kuajiri zenyewe wakati zinatumia pesa za umma, maana kwa Sasa zile taasisi zinazolipa vizuri zinaajiri zenyewe na ambazo Zina Hali mbaya kimaslahi ndo ajira zake zinapitia utumishi that's why Hawa watoto wa kimaskini wakishapata ajira huko mawazo yao yanakuwa ni kuhama taasisi kwenda taasisi zinazolipa vizuri na sio kufanya kazi kwa ufanisi.

Mungu ibariki Tanzania

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sio kwenye oral mkuu huu mchakato unaanzia kuanzia kwenye paper, witten then oral, kea taasisi zilizo na maslahi kiduchu hakuna anaejali but Taasisi zinazolipa vizuri mara nyingi Mara nyingi ndizo Zina final say, nakupa mfano mmoja mdogo na uuconfirm mwenyew, mwaka Jana mwezi wa Saba TAA walitangaza nafasi za kazi za Assistant Airport security ( 23posts) watu wakatuma maombi, baadae TAA akawaambia psrs anataka akachukue jeshini na tangazo likawa Re - advertised Tena psrs, watu wakatuma Tena kupitia portal but TAA akaenda kuchukua mwenyew jeshini anavyojua na Wala watu waliotuma hawakuitwa kwenye interview japo walitoa tangazo na mwezi January mwishoni psrs wakatoa tu majina ya watu walioitwa kazini TAA Kama assistant Airport security lakini hakuna popote alipotoa tangazo la kuitwa watu kwenye usaili na lazma ujue mshahara wa huyu security pale TAA mtu wa bachelor hizi taasisi za kawaida hamkuti
Kwa hiyo hapo kwenye Oral ndipo figisu zinakoanzia, au siyo? Halaf hivi PSRS huwa wanaajiri wao au taasisi inayohitaji
employees ndo yenye final say?
 
Sio kwenye oral mkuu huu mchakato unaanzia kuanzia kwenye paper, witten then oral, kea taasisi zilizo na maslahi kiduchu hakuna anaejali but Taasisi zinazolipa vizuri mara nyingi Mara nyingi ndizo Zina final say, nakupa mfano mmoja mdogo na uuconfirm mwenyew, mwaka Jana mwezi wa Saba TAA walitangaza nafasi za kazi za Assistant Airport security ( 23posts) watu wakatuma maombi, baadae TAA akawaambia psrs anataka akachukue jeshini na tangazo likawa Re - advertised Tena psrs, watu wakatuma Tena kupitia portal but TAA akaenda kuchukua mwenyew jeshini anavyojua na Wala watu waliotuma hawakuitwa kwenye interview japo walitoa tangazo na mwezi January mwishoni psrs wakatoa tu majina ya watu walioitwa kazini TAA Kama assistant Airport security lakini hakuna popote alipotoa tangazo la kuitwa watu kwenye usaili na lazma ujue mshahara wa huyu security pale TAA mtu wa bachelor hizi taasisi za kawaida hamkuti
Duh

Aisee, so kumbe PSRS ni kama paper tiger tu, hana makali!
 
Aisee nilibahatisha kupata nafasi ya buildup capacity kwenye moja ya taasisi ya Umma usiombe Manager anakaba kinoma sema kinachosaidia siku hizi ukipata chance maboss wanajua ni pandikizi kutoka juu so kukutimua kizembe wanaogopa, but ninachokiona kwasababu sina connection nikimaliza programme yangu niende tu kitaa nikapambane.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hahahahaha pole mkuu
 
Back
Top Bottom