Kwanini baadhi ya ajira za mashirika ya umma michakato yake haipitii utumishi?

Witmak255

JF-Expert Member
Feb 5, 2019
3,264
5,403
Habari zenu wanajamvi,
Naungana nanyi wote mlioko Tanzania kwa msiba wa kijana mwenzetu Ruge..! Hakika kazi yake ya hapa duniani ameimaliza na mungu ailaze roho yake mahali pema peponi,

Pia naona kwenye mitandao ya kijamii habari za kurudi nyumbani kwa mzee EL poleni pia mlioguswa kwa namna yeyote na huu uamuzi wake
Kama taarifa zitakuwa ni sahihi.

Niliahidi wiki ijayo siku ya alhamisi nitaleta humu uzi wa kuelezea fursa mbalimbali zilizoko nje ya nchi kwa wale watafutaji wanaoingia kihalali hili mpaka mda huu uzi ushakamilika unasubiri siku tu urushwe humu.

Leo naomba kuzungumzia ubovu uliopo kwenye michakato ya ajira unaowapa ugumu watoto wa maskini katika baadhi ya taasisi na mashirika ya umma na jinsi wakuu Hawa ambao michakato ya ajira ya taasisi zao haipitii utumishi wanavyopeana ajira kwa kujuana, ninayozungumza nina uhakika nayo kwa asilimia zaidi ya 100 maana nimefanya kazi serikalini kabla ya kuacha na kwenda nje ya nchi na nilipata kujenga connection na taasisi nyingi za serikali kwa nature ya kazi niliyokuwa nafanya hivyo Siri nyingi nilizijua.

Tangu psrs ( Sekretariati ya ajira) ianze kuratibu michakato ya ajira kwa taasisi na mashirika ya umma,. Urasimu na udanganyifu umepungua kwa kiasi kikubwa ( sio kwamba psrs haupo urasimu upo, huu urasimu nitauzungumzia siku moja), Leo nazungumzia hizi taasisi ambazo ajira zake hazipitii utumishi.

Kuna mashirika na taasisi ambazo ajira zake hazipitii utumishi Kama TANROAD, TANAPA, HIFADHI YA NGORONGORO, TANESCO, TPDC,WCF, NSSF, na hayo mashirika yaliyounganishwa kuunda (PSSSF) pia Kuna BOT, EWURA, TAKUKURU ziko nyingi Mimi nazungumzia hizi nilizo na uzoefu nazo.

Hawa BOT Kama hauna connection pale ya kukufanya ujulikane Basi hata wakikushortlist utaenda kukamilisha ratiba tu, nafasi zikitoka pale wanaanza kuulizana wao Kama Kuna mtu ana ndgu anakidhi vigezo then wanakuscreen kwa vimemo kwa watu wote wanaohusika na huo usaili ushahidi ninao sihitaji kuuweka wazi kwa watu walioingia hapo BOT kwa mlango huu, inaweza fanya wakanijua mapema maana wengi ni watu wangu wa karibu.

Kuna Hawa TANROAD ( Hawa ni warasimu kwelikweli kwenye masuala ya ajira) kwa nature za ofisi zao hasa mikoani kote isipokuwa makao makuu Hawa ofisi zao zinakuwa jengo moja na ofisi za Temesa, TBA, TAPE na pia huwa zinapakana na GPSA na kwenye hayo magodauni ya GPSA utazikuta ofisi za MSD wamepanga humo kwa ukanda wa ofisi hizi wafanyakazi wa TANROAD na MSD ndo huonekana matawi ya juu kwa sababu wanalipwa vizuri, Safari nyingi wanapata ikiwa wafanyakazi wa ofisi zingine Kama TANROAD,TEMESA, na GPSA wako hoi bin taaban ( labda kwa mfanyakazi wa GPSA kituo Cha mafuta huyu Yuko njema), hivyo hii inawafanya wawe wababe kwenye ukanda wa ofisi hizi, Hawa huwachukua ndgu zao au watoto wa kike wazuri waliohitimu vyuo wanawafanya vimada wao then wanawaweka kwenye ofisi wakiwa kama wafanyakazi wanaojitolea then nafasi za kazi zikitoka TANROAD mkoa wowote ule wanaanza kuwafanyia connection Kama mkoa husika uliotangaza hakuna mtu aliye ndani anafiti vigezo, kasheshe linakuja Kama huna mtu wa kukushika mkono hata nafasi ya kujitolea hupati labda uwe msichana mrembo then wakwere wakuone ukikubali masharti Yao Basi hapo utaula, MSD na TRA zamani nao walikuwa na tabia hii baada ya michakato ya ajira yao kuhamishiwa Psrs urasimu kwenye taasisi hizi umepungua.
Ushahidi wa taasisi hizi ninao na kwa kifupi fuatilieni ajira zilizotoka mwaka Jana mikoa ya tanga, njombe na Kilimanjaro, kigoma na ruvuma na kwingineko
Hawa ni watu ninaowajua na jinsi walivyopata kazi najua kwa hiyo najua ninachokiongea kwa zaidi ya asilimia 100

TANESCO Hawa ndo walewale ukiona umepata nafasi ya kazi hapa basi ujue wamemtafta wa kumuweka wamekosa, Tena Hawa wameenda mbali mpka nafasi zao za kazi Mara nyingi huwa wanatoa Kama "INTERNAL ADVERTISEMENT" tabia hii walikuwa nayo pia TPA kabla ya michakato Yao kuhamishiwa psrs, ili kuwapa nafasi watu wao waliowaweka kujitolea, Yaani hapa utakuta baba meneja, mtoto dereva, mwipwa afisa ugavi, binamu mhasibu hawaachani na TANAPA, Hifadhi ya ngorongoro na WCF ( kwa Sasa Hawa ndo wanaolipa vizuri + malupulupu kwa taasisi za serikali) Wala NSSF.

Hizi tabia zinachangia kuwafilisi watoto wa maskini just Imagine haya mashirika yanatoa nafasi labda Kilimanjaro, mtu Yuko ruvuma Hana nauli anauza mifugo au anakopa kwenda usaili ambao wenye michakato ya ajira wanajua nani mshindi wa kazi husika.

Pia hivi vibali wanavyopewa mameneja wa taasisi kuajiri watumishi wa mikataba nashauri hapa kuwe na utaratibu mzuri. Nakumbuka ilishawahi kufanyika ofisini kwetu kulikuwa Kuna upungufu wa madereva, phone operator, mhasibu,mgavi na mhudumu wa ofisi kwa uhitaji wa watumishi Hawa tulipewa kibali tuajiri ajira za mikataba, mimi nilianda tangazo then likasambazwa kubandikwa kwenye ofisi za serikali ili watu waone waweze kuomba ilikuwa mwaka Jana na kweli watu waliomba wengi, tukaita wote usaili ukafanyika na meneja alikuwa sauti ya mwisho kwenye hizi ajira Cha kushangaza watu walioitwa kuanza kazi wote ni ule mkoa anaotoka boss, siku zilivyoenda tukaja kugundua kumbe ni jamaa zake, na hii iko karibia ofisi zote za umma kwenye hizi ajira za vibali maalumu wanawekana kwa undugu na ujamaa na hapa ndo MAUMIVU yanapokuja kwa mtoto wa mkulima na maskini ambaye kwenye familia anakuwa hana mtu wa kumuongoza.

Nini kifanyike:

Ajira zote za serikali na mashirika yake zipitie Sekretariati ya ajira katika utumishi wa umma watu washindanie huko, haina maana ya kuundwa chombo hiki halafu taasisi zingine ziendelee kuajiri zenyewe wakati zinatumia pesa za umma, maana kwa Sasa zile taasisi zinazolipa vizuri zinaajiri zenyewe na ambazo Zina Hali mbaya kimaslahi ndo ajira zake zinapitia utumishi that's why Hawa watoto wa kimaskini wakishapata ajira huko mawazo yao yanakuwa ni kuhama taasisi kwenda taasisi zinazolipa vizuri na sio kufanya kazi kwa ufanisi.

Mungu ibariki Tanzania
 
Nahisi tunlaumu anaetoa kibari cha ajira kwa hayo mashirika pasipo kuelekeza ajira zao zipitie UTUMISHI.

Pia, kuhusu PSRP sidhani kama kuna ulasimu kwa mtu ambaye amefaulu vizuri...... tumeshuhudia mara nyingi ajira inatangazwa moja & anapatikana mtu kutoka huko kijijin wala hana connection yeyote anapata kazi UTUMISHI

Mimi naona UTUMISHI wajipange zaidi kuzuia mitihani yao isije kivuja ingawa sijasikia kama imevuja.

Sent from my GT-N7000 using Tapatalk
 
Duuuh huu ukweli ni mtupu kabisa na world is not fair kwa kweli ajira mpaka awamu hii ni za kupeana na huko maofisini nimeona kila ofisi ina kijana anayekuwepo eti anasaidia mara atumwe vocha, chai utasema msaidizi ofisi wakitoa ajira utasikia amepita kwenye usaili. EL kurudi nyumbani ni yeye Wala wa kumpokea amna.
 
Hivi ni watu wa aina gani wanapeana ajira, si ni hawa wakijani manjano kwa huu utawala maana tuliwazoea wahaya ndio wazee wakuitana ukoo mzimaa, sasa hivi ni watu waziwani ndio wanaitana, sasa mtu alikuwa akisema una kazi hapo, unajibiwa nina kazi mi muhaya.
 
Hapa nilipo hadi afisa mtendaji wa kijiji na uongozi wote wanatokea ziwani, watu waziwani saa hii wanabaraka ukisikia wazee wa vyeo wote ni ziwani, sijui luteni, sijui mhasibu wa serikali, na wa bandari utakuta ni ziwani.
 
Hapa nilipo hadi afisa mtendaji wa kijiji na uongozi wote wanatokea ziwani, watu waziwani saa hii wanabaraka ukisikia wazee wa vyeo wote ni ziwani, sijui luteni, sijui mhasibu wa serikali, na wa bandari utakuta ni ziwani.
Hatari
 
Yote utaongea ila ishu ipo hivi, ukitaka kazi kirahisi kwa zama za sasa ni kujitolea kuchapa kazi bure tu. Ndani ya miaka miwili utakuwa ushapata mkataba wa kazi. Huwa wana consider wale Volunteers hasa kama umeonesha uwezo wako na walau sifa kidogo unazo (hata kama una lower second)
 
Back
Top Bottom