Kwanini awamu ya Nne inatupiwa lawama na kudharauliwa?

DNR

JF-Expert Member
Mar 28, 2013
523
337
Ni ukweli usiofichika kwamba awamu ya nne hasa miezi ya hivi karibuni baada ya kuingia awamu ya tano imekuwa ikitupiwa Maneno ya dharau ,kashfa hata matusi ,Ushahidi hapa hapa JF likitajwa jina la JK comments zitakazofuata ni as if he did nothing wakati akiwa madarakani na kudharaurika .

Maswali yanakuja je :-
1. Ni kweli hiyo awamu ya nne ilikuwa mbovu kiasi hichi watu wanachoizungumzia ?
2. Kuna uwezekano na Ukweli wowote UHURU wa Habari na Upole wa JK ni sababu ya serikali kuonekana ilikuwa mbovu kiasi hicho ?
3.Je idadi ya majipu yanatumbuliwa ni ushahidi Tosha awamu iliyopita ilikuwa mbovu kiasi hicho ?
4.Je kuna haja ya kurudi nyuma na kuangalia mambo mazuri aliyofanya na kubadili mitazamo Yetu ?

TUJADILI. Kwa mimi naona kafanya mengi sana ambayo hata awamu ya tano inahitaji miaka mingi kutimiza hata kwenye wizara moja tu ya Ujenzi .
 
Mi naikumbuka sana kwa kuboresha maslahi ya wafanyakazi, alikuta lodi ya paye 18% akaishusha hadi 11%, kipindi chake ndicho wafanyakazi tumeweza kupata mshahara muda muafaka kumbuka kipindi cha mkapa hadi tarehe 10 ya mwezi unaofuata, nk
 
Mbona kichwa cha habari hakiendani na maudhui yako
unachotaka ni nini hasa
Serikali ya Magufuli ndio ina siku ya 201 tu unataka kuifananisha na miaka 10
Haya anza na kuadimika kwa Sukari
  1. Wafanyabiashara wanasimamisha kichwa ngumu na sukari
  2. umeme kidogo tungekufa kwa bei ya umeme kupanda kila siku sasa bweleleee
  3. vyombo vya habari na mitandao ni kabali hasaaa
 
Mkuu kunawatu wana akili za kunakili (kugezea).shuleni walikuwa wabanaji mara nyingi madaftari yao wanayakunja na kuchomeka mfuko wa nyuma,hawana lolote zaidi ya kuimba kama kasuku.wanaishi kama makinda ya njiwa, wanamezeshwa maneno na wanayameza mazimamazima.....sikuhizi wamekuwa kama (karakana ya kijeshi Kibaha kwa Matiasi ya kutengeneza magari)...
 
Jk kafanya makubwa kuliko maraisi wote waliowahi kutawala Tanzania mfano hai angalia kwenye kilomita za Barabara yeye ndio kajenga nyingi,idadi ya shule ndio usiseme,vyuo vikuu vingi,yeye ndie aliyeajiri watu wengi kuliko wenzake,ongezeko la wanachuo wanaopata mikopo,kipato kuongezeka kwa watu na watu wengi walipata uwezo wa kujenga Nyumba,mishahara kuwa mikubwa na mzunguuko wa pesa ulikuwa mzuri.jk nakutakia maisha mema.
 
Mi naikumbuka sana kwa kuboresha maslahi ya wafanyakazi, alikuta lodi ya paye 18% akaishusha hadi 11%, kipindi chake ndicho wafanyakazi tumeweza kupata mshahara muda muafaka kumbuka kipindi cha mkapa hadi tarehe 10 ya mwezi unaofuata, nk
Umenena kweli
 
Hakuna lolote la maana zaidi ya upendeleo kwa washikaji, marafiki zake, familia, ufisadi uliokithiri,trip za nje zisizo idadi na zaidi ya yote ni mipasho na matumizi mabaya ya fedha za nchi angalia bunge la katiba. Ukweli ni kwamba nikikumbuka miaka 10 ya huyu bwana natamani kupasuka. Pamoja na ujinga wangu mimi ningepewa hiyo nafasi kweli amini nisingefanya madudu kama alivyofanya huyu jamaa
 
Huna kumbukumbu wewe, mkapa alikuwa analipa mshahara kabla ya tar 25. Ongea issue za PAYE
 
Hakuna lolote la maana zaidi ya upendeleo kwa washikaji, marafiki zake, familia, ufisadi uliokithiri,trip za nje zisizo idadi na zaidi ya yote ni mipasho na matumizi mabaya ya fedha za nchi angalia bunge la katiba. Ukweli ni kwamba nikikumbuka miaka 10 ya huyu bwana natamani kupasuka. Pamoja na ujinga wangu mimi ningepewa hiyo nafasi kweli amini nisingefanya madudu kama alivyofanya huyu jamaa
Urais sio rahisi kihivyo ,jamaa kafanya kwa sehemu vizuri Nakumbuka ilikuwa taabu sana kutoka Iringa mpaka Tabora Lakini siku hizi unapanda basi saa 12 saa tisa uko Tabora .
 
Jk kafanya makubwa kuliko maraisi wote waliowahi kutawala Tanzania mfano hai angalia kwenye kilomita za Barabara yeye ndio kajenga nyingi,idadi ya shule ndio usiseme,vyuo vikuu vingi,yeye ndie aliyeajiri watu wengi kuliko wenzake,ongezeko la wanachuo wanaopata mikopo,kipato kuongezeka kwa watu na watu wengi walipata uwezo wa kujenga Nyumba,mishahara kuwa mikubwa na mzunguuko wa pesa ulikuwa mzuri.jk nakutakia maisha mema.
TENA YENYE BARAKA TELE...! JK TUTAKUJUMBUKA KWA MENGI SANA MAZURI Mfano: UJENZI WA SHULE ZA KATA AMBAZO HAO WANAOMBEZA LEO WAMESOMA KWENYE SHULE HIZO PIA MABORESHO MAKUBWA YA HOSPITAL ZA MIKOA YOOOTE NCHI NZIMA..
 
Sound km mleta mada kesha surrender ktk fikra za kijamaa kuwa haki yako kupewa ni hisani. Polesni sana. JK alikuwa dhaifu na alivyoviachia ni haki ya watanzania ambayo ccm iliamua kufanya iwe km hisani kwa watu maalumu ktk chama.
 
Jk kafanya makubwa kuliko maraisi wote waliowahi kutawala Tanzania mfano hai angalia kwenye kilomita za Barabara yeye ndio kajenga nyingi,idadi ya shule ndio usiseme,vyuo vikuu vingi,yeye ndie aliyeajiri watu wengi kuliko wenzake,ongezeko la wanachuo wanaopata mikopo,kipato kuongezeka kwa watu na watu wengi walipata uwezo wa kujenga Nyumba,mishahara kuwa mikubwa na mzunguuko wa pesa ulikuwa mzuri.jk nakutakia maisha mema.
Yah kwa hilo hata mm nasapot jk alijitahid japokuwa now watu hawaoni hayo
 
Mmmm! mbona ni kawaida kwa bin Adam unapokuwa hai watu wana angalia mapungufu yako ili wengine waya epuke na unapokuwa umekwenda wale wale wata angalia mema uliyotenda ili walio baki wayafuate. We subiri, mema yake yameshaandikwa ni muda tu ...
 
Back
Top Bottom