Kwanini Amani haipatikani Duniani?

ndege JOHN

JF-Expert Member
Aug 5, 2015
19,553
44,719
Jibu la Biblia

Jitihada za wanadamu za kuleta amani hazijawahi kufanikiwa na zitaendelea kutofanikiwa kwa sababu kadhaa:

“Njia ya mtu wa udongo haimo katika uwezo wake.” (Yeremia 10:23) Wanadamu hawakuumbwa wakiwa na uwezo na pia haki ya kujiongoza, hivyo hawatafanikiwa kupata amani ya kudumu.

“Msiwategemee viongozi wa kibinadamu, hakuna mwanadamu anayeweza kukuokoa. Wanapokufa, wanarudi mavumbini; siku hiyo mipango yao yote inakwisha.” (Zaburi 146:3, 4, Good News Translation) Viongozi wa serikali, hata wale walio na nia nzuri kabisa, hawawezi kutokeza suluhisho la kudumu ili kuondoa chanzo kikuu cha vita.

“Katika siku za mwisho kutakuwa na nyakati za hatari zilizo ngumu kushughulika nazo. Kwa maana watu watakuwa . . . wakali, wasiopenda wema, wasaliti, wenye vichwa vigumu, wenye kujivuna kwa kiburi.” (2 Timotheo 3:1-4) Tunaishi katika “siku za mwisho” za ulimwengu huu mwovu, wakati ambapo mitazamo ya watu inafanya iwe vigumu kupata amani.

“Ole wa dunia na wa bahari, kwa sababu Ibilisi ameshuka kwenu, akiwa na hasira kali, akijua kwamba ana kipindi kifupi cha wakati.” (Ufunuo 12:12) Ibilisi, ambaye ni adui ya Mungu, ametupwa katika ujirani wa dunia na anawachochea watu wawe na roho kama yake ya ukatili. Mradi anaendelea kuwa “mtawala wa ulimwengu huu,” hatuwezi kamwe kuishi kwa amani.—Yohana 12:31.

View attachment 2140573
 
Kwani huyu mwamba hapa anasema je?

IMG_20220305_073032_979.jpg
 
Amani kwa wote ni vigumu kupatikana, kwa sababu, amani ya mmoja ni vita ya mwingine.

Fikiria kama kuna chakula kwenye sahani, cha kutosha mtu mmoja tu, halafu kuna watu kumi wanakitaka.

Hapo hakuwezekani wote kushiba, na asiposhiba hata mmoja amani inakuwa ngumu.
 
Dunia kwa wakati huu na miaka 70 iliyopita ina amani kuliko kipindi kingine chochote katika historia.
Kabla ya Empires na baadaye mataifa ya kisasa binadamu walikuwa wanauana sana kwa vita vya koo, makabila na mipaka. Empires zilipunguza vita kwa kiasi kikubwa katika jamii ya mwanadamu kwa sababu zilikuwa zinakusanya pamoja jamii nyingi tofauti katika eneo kubwa.Zilikuwa zikiendeleza vita ila zilijitahidi sana pia kuhakikisha amani na utulivu unakuwepo kwa ustawi wao.

Baada ya kuanguka kwa Empire ya mwisho duniani (British Empire) na dunia nzima kuwa na haya mataifa ya kisasa ilikuja miungano na shirika(alliances) ambazo kwa kiasi kikubwa imesaidia kutunza amani katika sehemu kubwa ya dunia kwa muda mrefu tangu mwaka 1945 baada ya kuisha kwa vita vya pili vya dunia.
 
Back
Top Bottom