Kwanini alama ya kidole isibebe maelezo, bila msaada wa namba ya Kitambulisho?

nyumbamungu

JF-Expert Member
Mar 3, 2017
996
826
Kuna tofauti gani ya mfumo wa NIDA na ule tunaoukuta kwenye Mapokezi au Milango ya ofisi mbalimbali inayompasa mfanyakazi kabla hajaingia ndani ya ofisi au jengo inamlazimisha aweke kidole kwenye kifaa kilichopo ukutani, na pindi anapoweka kidole ndio maelezo ya mfanyakazi husika yanapohifadhiwa kwenye kanzi data (database) na mlango ndio unafunguka.

Dhumuni ni kufahamu mfanyakazi amefika sangapi, mfumo unafanya kazi bila mfanyakazi kuweka namba yake ya Kitambulisho cha kazi.

Kwanini wakati wa zoezi la kusajili laini za simu mfumo usifanane na huo? Yaani kwa wale wenye kitambulisho cha NIDA itoshe kwa kuweka kidole tu bila kuweka namba ya kitambulisho, iwe hivyohivyo hata kwenye ofisi za Umma kama TRA, BRELA, Manispaa, Benki nk.
 
Back
Top Bottom