Kwanini ajira nyingi za muda Serikalini wanapeana wenyewe watumishi ambao tayari ni watumishi.?

sili SG

Member
Oct 12, 2018
22
26
Habari wana JF. Siku hizi kwenye serikali kumepatikana nafasi mbalimbali za kazi za muda na kutangazwa nafasi za kazi za kwa wananchi wenye sifa mfano kuna hizi za tume ya taifa ya uchaguzi katika kuboresha daftari la kudumu la wapiga kura na n,k lakini cha kushangaza asilimia kubwa ya hizi nafasi wanapeana wenyewe watumishi wa ndani wenye mishara na marupurupu kibao ili hali kuna wimbi kubwa la vijana wenye sifa stahiki na kuzidi wananyimwa hizo nafasi.?

Sasa hivi kuna zoezi la uchaguzi wa serikali za mtaa linakuja nchi nzima na wameanza kutangaza nafasi nyingi kwenye halmashauri mbalimbali lakini cha kushangaza kigezo kinawekwa ili upate hizi nafasi inabidi uwe mtumishi wa umma Kweli kwa Tanzania hii yenye watu Zaidi ya million 50 bado tuna endeleza mtindo wa kuvishana kofia mbilimbili.Inakuwa hatuwatendei haki wasomi wetu pamoja vijana wenye sifa halafu hawana ajira.(hata hizi za muda mnabana )Kwanini tusiwaachie hizi nafasi vijana ambao wanasifa.?

kama mnaisi kigezo cha form 4&6 mtapata wengi sana na itakuwa ngumu kuchagua basi pandisheni kigezo angalau mwenye certificate na kuendelea (kwa sababu hakuna mambo complicated kwenye hayo majukumu) ila sio mwenye ajira tena anapewa ajira nyingine matokeo yake wanafanya kazi chini ya kiwango (mshika mawili moja humponyoka) .

Niwaombeni vijana wenzagu tulalamike kila kona kupitia platform mbalimbali naamini hili swala likimfikia mkuu litafanyiwa kazi na watatengua hichi kigezo kandamizi cha ili upate kazi lazima uwe mtumishi wa umma.wakati wao tayari wana majukumu mengine ya kufanya.

Na ikiwezekana wakatazwe kabisa kuomba hizo nafasi waachie vijana ambao hawana ajira na wajue kwamba hata kazi za muda inapunguza unemployment rate.(mf ukiajiri kwa muda vijana 50,000 hujawapunguzia magumu hawa).?
 
Kwakweli nashindwa kuelewa hii Kazia mana vijana wamejaa wengi hawana ajira
 
Niliambiwa eti watumishi wauma n waatifu na wachapakazi.
 
Zen hao viongozi wao cjui wa uchaguzi hata hawalizungumzii nasijaona kiongozi yoyote wala waandishi wa habari wakihoji iyo ishu.
 
Iyo kazi ni ya wiki1 wala kijana asiyekua na ajira hawezi kujikwamua kimaisha na ajira ya wiki1. Acha wapeane tu
 
Mkuu nikupongeze kwa kupaza sauti yako asee, sio poa kwakweli inabidi waache hii kitu. Hizi nafasi hata mimi niliziona ni nyingi sana lakini kigezo kimoja tu ndo shida, nafikiri kuna siri nzito ya serikali kufanya hili la lazima uwe mtumishi wa uma...
 
Acha mawazo mgando mkuu, 20,000/=kwa week ni shilling ngapi...? Hiyo pesa kwa week ukipewa huwezi fanya kitu au ndo....
Iyo kazi ni ya wiki1 wala kijana asiyekua na ajira hawezi kujikwamua kimaisha na ajira ya wiki1. Acha wapeane tu
 
Wadogo zangu msilie sana kuna baadhi ya kazi ni nyeti zinaitaji usiri na umakini wa hari ya juu , serikali ikisema izitoe kwa kila mtu kwa kigezo cha kuwa ana elimu ya sekondari au chuo serikali itajikuta inaingia hasara kubwa sana

Mfano hili zoezi la uandikishaji wapiga kura uchaguzi wa serikali za mitaa 2019 ukisema uchukue mtu yoyote tu yule yanaweza jitokeza mambo haya

Kijana yupo mtaani kafanya usaili kampuni X anasubilia majibu kati kati ya zoezi anapigiwa sm njoo kuripoti kazini au njoo kwenye usairi je atakomaa na kazi ya wiki moja ya kuandikisha au atabwaga aenda kwenye usaili au kuanza kazi jiulize wewe utafanyaje

Pili kijana kapewa document nyeti atunze kwa umakini sana pamoja na kumsisitiza umuhimu wake kwakua hana dhamana ya kitu chochote tofauti na mtumishi wa umma ambaye ajira yake ndio dhamana basi si ajabu kukuta karatasi moja kachana kafungia vitumbua au kumuachia mtu afanye kazi yeye anachat na sm au kaenda nyumbani mala moja

Kwaiyo wanapoombwa watumishi wa umma wanakuwa na uhakika kazi itafanyika kwa umakini bila usumbufu kwani hakuna mtu anayeweza kuacha kazi kisa elfu 20
 
Uko sahihi. Sababu nyingine ya kufanya hivyo ni urahisi wa hao Watumishi wa umma kujidhamini wenyewe. Kuna baadhi ya majukumu yanahitaji viapo vya utunzaji SIRI, uaminifu, nk.

Kuna madhara yanaweza kutokea iwapo utampa jukumu mtu ambaye hana cha kupoteza, hadhaminiki, halafu akaharibu hilo zoezi ambalo kimsingi ni la Kitaifa.

Hata mimi siungi mkono serikali kutokuajiri wahitimu wenye sifa za kufanya kazi nchini mwetu, ila kuna mambo mengine hakuna namna, ni lazima uwape watu ambao ni rahisi kuwabana na kuwachukulia hatua za kinidhamu iwapo wataharibu kazi/mchakato.
 
Habari wana JF. Siku hizi kwenye serikali kumepatikana nafasi mbalimbali za kazi za muda na kutangazwa nafasi za kazi za kwa wananchi wenye sifa mfano kuna hizi za tume ya taifa ya uchaguzi katika kuboresha daftari la kudumu la wapiga kura na n,k lakini cha kushangaza asilimia kubwa ya hizi nafasi wanapeana wenyewe watumishi wa ndani wenye mishara na marupurupu kibao ili hali kuna wimbi kubwa la vijana wenye sifa stahiki na kuzidi wananyimwa hizo nafasi.?

Sasa hivi kuna zoezi la uchaguzi wa serikali za mtaa linakuja nchi nzima na wameanza kutangaza nafasi nyingi kwenye halmashauri mbalimbali lakini cha kushangaza kigezo kinawekwa ili upate hizi nafasi inabidi uwe mtumishi wa umma Kweli kwa Tanzania hii yenye watu Zaidi ya million 50 bado tuna endeleza mtindo wa kuvishana kofia mbilimbili.Inakuwa hatuwatendei haki wasomi wetu pamoja vijana wenye sifa halafu hawana ajira.(hata hizi za muda mnabana )Kwanini tusiwaachie hizi nafasi vijana ambao wanasifa.?

kama mnaisi kigezo cha form 4&6 mtapata wengi sana na itakuwa ngumu kuchagua basi pandisheni kigezo angalau mwenye certificate na kuendelea (kwa sababu hakuna mambo complicated kwenye hayo majukumu) ila sio mwenye ajira tena anapewa ajira nyingine matokeo yake wanafanya kazi chini ya kiwango (mshika mawili moja humponyoka) .

Niwaombeni vijana wenzagu tulalamike kila kona kupitia platform mbalimbali naamini hili swala likimfikia mkuu litafanyiwa kazi na watatengua hichi kigezo kandamizi cha ili upate kazi lazima uwe mtumishi wa umma.wakati wao tayari wana majukumu mengine ya kufanya.

Na ikiwezekana wakatazwe kabisa kuomba hizo nafasi waachie vijana ambao hawana ajira na wajue kwamba hata kazi za muda inapunguza unemployment rate.(mf ukiajiri kwa muda vijana 50,000 hujawapunguzia magumu hawa).?
Waiter naomba niongeze bia nyingine tafadhali... :cool: :cool: :cool:
 
Back
Top Bottom