The Initiator huru
JF-Expert Member
- Dec 4, 2017
- 1,530
- 1,733
we are poor because we are poorDuniani kuna aina za nchi kulingana na mfumo, nguvu zake kiuchumi, kijeshi na kisiasa:
1. Super powers
Hizi ni nchi zinazoitawala dunia. Ndiyo zinashikilia mfumo unaoendesha dunia (ideology) Ndani yake kuna taifa kiongozi (leading nation) ambayo kwa hali ya sasa mfumo Ni Ubepari (capitalism), superpowers ni nchi kama Amerika, China, Urusi, Ujerumani, na taifa kiongozi ni Amerika
2. Independent States
Hizi ni nchi huru ambazo zinaweza kuamua sera zake zenyewe bila kulazimishwa na superpowers. Hizi huwa nchi zenye uwezo pia. Nchi kama Sweden, Denmark, Switzerland zinaingia hapa
3. Subordinate States
Hizi ni nchi zinazokoloniwa, hazina sera binafsi bali sera zake ni sera za mkoloni wa muda huo. Nyingi ni nchi masikini za Afrika na zinazoendelea. Wakoloni hupanga chama cha kutawala, muda wa kutawala, na nani atawale,nk
Afrika inaingia kwenye hili kundi la tatu hivyo haina mfumo, haina uhuru, haina nguvu za kijeshi, kiuchumi, wala kisiasa na kwahiyo inabaki kuwa masikini