Mada inajieleza. ACT ni mdau ndani ya Serikali ya Zanzibar. Makamu wa kwanza wa Rais ndie mshauri Mkuu wa Rais ingawa Rais hapangiwi la kufanya sawa.
Tatizo linakuja kwenye Dhamira ya kweli ya kile anachohubiri Rais Mwinyi. Haiwezekani katika hali ya mashaka ya kile kilichotokea uchaguzi wa 2020 na kilichotokea Zanzibar hasa Pemba kuuliwa watu wasiopungua 20 kwa uchaguzi ulioacha makovu halafu Rais Mwinyi amrejeshe Mkurugenzi wa ZEC huyo anaeshutumiwa kwa uharibifu. Lazima kuna tatizo.
Mahubiri ya Mh Rais ya maridhiano ya kweli yametatizwa kwa makusudi ama na yeye mwenyewe au hao waliomzunguka. Haiwezekani kwamba mpaka maamuzi ya uteuzi yanafanyika bila ushauri wa pande muhimu.
Speculations.
1. Rais aidha hana dhamira nzuri za maridhiano.
2. ACT wanalazimishwa kukwamishwa kwa makusudi ndani ya serikali pengine kuna azma imepangwa
3. Rais kaelemewa na mzigo wa chama chake kwa kulazimishwa kumrejesha mkurugenzi anayelalamikiwa.
4. CCM inamkwamisha Rais Mwinyi juu ya haja ya maridhiano ya kweli vyenginevyo wangeliona hili na kumshauri.
Hayo ni mawazo yangu tu.
Haiwezekani kwamba wiki moja imepita nyuma imetoka ripoti ya kamati Maalumu kuhusu Demokrasia na maridhiano Zanzibar na kupendekeza hatua kadhaa za kujenga zama mpya halafu papo hapo Rais ateue mtu ambae kwa uhakika alijua ataleta zogo kwa muktadha wa Zanzibar hapo lazima kuna tatizo.
Kishada.