Uchaguzi 2020 Kwanini ACT-Wazalendo wanahimiza sana Wapinzani Kuungana tofauti na CHADEMA ambao wanataka kila Mtu apambane na hali yake tu?

Kila nikiwasikia ACT-Wazalendo wakizungumza naona wanatia sana Huruma na wakati mwingine hadi 'wanalazimisha' Waungane na CHADEMA lakini kila nikiwasikia CHADEMA wao nawaona hawataki huo Ushirikiano wa 'Kinafiki' na badala yake wanataka kila Chama Kipambane tu na hali yake kuelekea Uchaguzi Mkuu ujao. Safi mno CHADEMA hakuna Kuungana nao Lissu Wetu anatosha.

Kazi ipo mwaka huu!
Wewe jamaa umechanganyikiwa.

Hata wapinzani wakiungana, sisi lazima tushinde kwa namna yoyote ile.
 
Kuungana kuna hasara moja kubwa ambayo lazima wapinzani waielewe.

Wapinzani wakishaachiana majimbo ya uchaguzi ccm kwa kutumia zile 1.5 trillioni walizopora serikalini watazitumia kuwahonga wagombea ubunge/udiwani wa vyama vya upinzani na hasa wa Act-wazalendo kusudi wajitoe.

Mchezo huu tuliuona mwaka 2015 ambapo kuna wagombea ubunge wa chama cha Cuf walihongwa na ccm na kuacha kugombea na kupelekea wagombea wa ccm kupita bila kupingwa.

Hivyo mimi naona kila moja apigane tu kivyake. Kwa mazingira ya Tanzania vyama kuungana ni hatari kwa sababu nilizozitaja hapo juu, labda kwenye nafasi ya urais tu.
 
Labda pawe na muungano wa maandishi, lakini naona pana kitu hapo mbeleni juu ya hata kama wakiungana, hili lilitakiwa mapema sana japo lina faida na hasara kama ilivyo kawaida kwenye mambo mengi kuwa na pande mbili.
Happy kiachotafutwa ni mgombea mwenza mkuu
 
20200805_160702.jpg
 
Back
Top Bottom