Kwanini ACT Wazalendo hawashiriki uzinduzi Ripoti ya Uchaguzi Mkuu 2020 wakati wameunda Serikali huko Zanzibar?

mshale21

JF-Expert Member
Apr 8, 2021
2,050
4,903
Wakuu, natumai hamjambo!

Mbali na CHADEMA, walioonesha nia ya dhati ya kutoshiriki hafla ya kukabidhi report ya uchaguzi 2020 inayotarajiwa kufanyika Leo , tar 21/8/2021, Vyama vya ACT na NCCR, vimetoa misimamo yao ya kutohudhuria hafla hiyo kwa madai mwaka 2020 hakukua na uchaguzi.

Kwa, upande wa ACT wao wamesema hawatoweza kushiriki katika hafla hiyo kwa sababu mwaka 2020 hakukua na uchaguzi Bali kile walichokiita UCHAFUZI na hivyo kutanabaisha kuwa hawawezi kuhalalisha hujuma hiyo.

NCCR wao wametoa sababu ya kutohudhuria kuwa, ofisi ya tume ya uchaguzi haikutoa ushirikiano juu ya malalamiko na maoni yao katika mchakato mzima wa uchaguzi.

Vyama vinginevyo, visivyokuwa na uwakilishi bungeni, wao hawajatanabaisha msimamo wao, lakini bila shaka watajihudhurisha kwenye hafla hyo, kwa sababu siku chache zilizopita walitoa msimamo wao kuwa hawaoni haja ya katiba mpya kwa sasa mpaka muda utakapofika.

Inashangaza kuona ACT wazalendo hawajahudhuria, kwani ni chama kinachounda serikali huko Visiwani!

Binafsi sijawaelewa wanataka nini?

IMG_20210821_101058.jpg
IMG_20210821_101041.jpg
 
Wamesema serikalini wameingia na kushiriki hawashirki kwenye uvumbuzi ,mtawafanya nini ? ACT ndio aliyekamata mpini Zanzibar na CCM wanalijua hilo kwamba Zanzibar hio inajiondoa kivyake vyake.
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom