Kwanin screen ya tv haiwezi kuwa monitor.

ENGINE CONTROL

Senior Member
Nov 20, 2011
136
27
Wakuu aulizaye anataka kujua ni bora nionekane mshamba na mpumbavu kwa mda.

Wataalam na wenye ufaham na ujuzi naomba kufahamishwa na kuelimishwa juu ya hili.Je zile tv za chogo kwa nin huwezi kuzitumia kama monitor??
Je kama inawezekana ni nin inabidi kiongezwe au kupunguza au kwa kuwa hazina sehem ya kuconect cpu??

Na je mbona kuna hizi tv za flat ambazo unaweza kutumia kama monitor kwanin kwa hizo iwezekane na kwa zile tv chogo ishindikane??

Na je kwa monitor zile za chogo huwezi kuzitumia kama tv ya kawaida?? Je ni vitu gan inabidi viongezwe ili iwezekane??

Naomba mnitoe ushamba mwenzenu.
 
Tv za siku hizi (LCD TV) unaweza kuitumia kama monitor kwa sababu inakuja na Connetor ya VGA au DVI kwa ajili ya kuchomekea CPU yako, kitu ambacho TV za "chogo" hazina na atahitajika fundi mwenye ujuzi sana kuweza kuiweka hiyo connector.......

Ukitaka kutumia monitor za chogo kama tv inabidi uwe na computer iliyofungwa TV card!! unachomeka antena au kingamuzi chako unakula life!!..........
 
kwa hiyo kwa maelezo yako hayo mkuu kwahiyo inawezekana kabisa saketi ya tv ya chogo ikiungwa hiyo connector ya VGA au DVA itafanya kazi kama kawa au kuna kitu kingine kinatakiwa kuongezwa ndan ya saketi yake??
 
TV hizo za chogo ambazo kwa jina la kitaalam zinaitwa Cathode ray tube zinaweza pia kutumika kama monitor endapo utakuwa na cable yake ya kuconnect. Kinachowafanya watu wasitumie TV hizo kuconnect kwenye system unit ni kwa sababu cable zake hazipatikani kwa urahisi
 
Back
Top Bottom