Zuriel_cfc
JF-Expert Member
- Nov 2, 2017
- 4,092
- 9,055
Hizi ni nzuri sana naomba kujua kwa ambao tumeweka grill hii itakaa nje au ndani?
Hizi ni nzuri sana naomba kujua kwa ambao tumeweka grill hii itakaa nje au ndani?
Kwamba ukifungua ile space iliyofunguka ni ndogo kulingana na madirisha mbadala ?
Unaona hio point ni duni ?; Kwanza Faida ya Dirisha au umuhimu wa Dirisha ni nini ?
Ukijibu hayo utaona mleta uzi ana point ya maana sana...
Mleta Uzi una point sana aisee wewe ni peponi moja kwa moja now kwangu nimeweka grill tu nimetia na nyavu basi kwa sasa kwani kuna jirani yangu kayaweka anapata tabu sana fikiria umeiweka dirisha la 5×5 ukiweka hayo madrisha maana yake dirisha linakuwa 2.5
Vitu viko on point mno. Mafundi sasa hapo uende akutengenezee hivyo atakutolea kitu cha ajabu mpaka ushangae
Tatizo wabongo tunskurupukia mambo,hizo dirisha za aluminum ni lazima iwe kubwa minimum futi 5*5 sasa mtu hata futi 4 anaona kubwa eti anakwepa gharama.Hii tumei discuss sana na mwanang mmoja hivi, ni kweli haina maana zaidi ya show tuuu, dirisha linatumika nusu
Wabunifu wapo tatizo ni ushamba na kuona eti kulipia ramani ni ghali wanachukua ya fundi Michael, kingine ni uoga wa gharama kwa vitu vipya.Vitu viko on point mno.Mafundi sasa hapo uende akutengenezee hivyo atakutolea kitu cha ajabu mpaka ushangae
Halafu kitu kingine nilishawahi kunote na kusema humu. Tanzania ni kama hatuna architecture binafsi. Majengo yoote karibia tunajenga mjengo wa aina moja tofauti yetu ni ukubwa wa vyumba tu
Watu hawaji na idea mpya za majengo zaidi ya Yale Yale na mapaa Yale Yale sijui wenye hela za kujenga kwann mmejificha kwenye kaboksi
Ngoja mie nijikusanye nijenge niache mdomo kusema ya watu😂😂
Ongeza ukubwa wa dirisha ndio design ya hayo madirisha badala ya hivyo viduchu eti mtu anakwepa gharama lazima italeta shidaYeah dirisha linakuwa wazi nusu, inabidi watengene ya kuzama chini kama vioo vya magari watie na power windows😂😂😂
Yanawakaribisha kwa kusema "karibu mbu"😂🤗Yanaingizaje mbu?
Yaaani mimi hata huwa sielewi mtu anaposema kajenga nyumba Kali nikija kuiona naona ile ile tu kama lodge tunazolala na nyumba nyingine.Wabunifu wapo tatizo ni ushamba na kuona eti kulipia ramani ni ghali wanachukua ya fundi Michael, kingine ni uoga wa gharama kwa vitu vipya.
Matokeo yake nyumba zote mtaani zinafanana tofauti ni ukubwa na rangi za mabati, mtaani kuna nyumba za ajabu Sana.
Ulipaswa wewe ndio utupe mbadala badala ya kuwatupia wengine mzigo.Binafsi si shabiki wa madirisha yanayotamba siku hizi, aluminiamu na pvc. Sababu kubwa ni kutokuwa na uimara wa kutosha na pia hata yakifunguliwa yanachukua sehemu kubwa ya dirisha na hivyo kuzuia hewa.
Hii ni mbaya zaidi kwa mimi wa sehemu ya joto. Madirisha haya yakifungwa, huko ndani mtajuta kuishi ndani hilo jengo. Kwani madirisha mengine ya kisasa ni yepi tukiacha yale ya tulipotoka?
Ndiyo tumekwama hapo?
Wabunifu mpo wapi?
Haya madirisha yanavutia sana
Ehee! Kuna kitu wajengaji wa siku hizi wanakisahau.Tatizo wabongo tunskurupukia mambo,hizo dirisha za aluminum ni lazima iwe kubwa minimum futi 5*5 sasa mtu hata futi 4 anaona kubwa eti anakwepa gharama.
Design ya hayo madirisha yanataka hivyo,pili zile vents za Juu ziwe wazi hata ukilala ucku
Ukipata fundi mzuri anakutengenezea inakuwa na double shutter, ndani kunakuwa na shutter za wavu halafu nje zinakuwa hizo.. Hapo mbu utawasikia kwa jirani.Asante sana. Haya ni mazuri mno. Kwa mimi, aluminium haziingii hapa hata kwa 1/4. Swali ni , wavu wa mbu unakaa wapi hapo?
kati kati ya zile sliders mbili za vioo kuna upenyo mdogo, kwa mbu ni hallway ya mita 500
ikifika saa 12 jioni inabidi ufunge, yawe sealed shut, la sivyo utalia, ndani panakua nje, bora hata nje
ukifunga jiandae na 'suffocation' ya kutosha , ikifika saa 3 usiku uyafungue tena, ukisahau ukalala
iyoivyo bila 'AC' kuwa ON ( sio feni )
kesho asubuhi jiandae na 'kizunguzungu'[/]
faida moja kubwa ya dirisha la alminium au kioo ni kuzuia vumbi ndan na moshi maana huku uswahili mtu kujichomea nyasi au takataka kawaida sasa bila madirisha hayo moshi wote utajaa ndan
swala la mbu basi kama kuna dirisha uliona liko hivyo litakuwa liliwekwa vibaya au ni cheap quality maana yanatofautiana ubora jinsi ya kuwekwa
hakuna namna mbu anaingi na ukiacha waz kuna nyavu za kuzuia mbu, maana hayo madirisha kwenye huo uwaz kuna raba flan inawekwa..ya kuzuia wadudu wa kutambaa na hata mbu hiyo rubber inakuwa inagusa kwenye kioo ukifunga au kufungua
mie natumia na wakati wa usiku nayafunga yote na situmii fan wala hakuna suffocation .. joto la dar hata uweke wavu mtupu kipind cha joto utaitafuta fan.. tumezaliwa na kukulia kwenye madirisha ya wavu na bado joto lilitukomesha
kama ni kiangaz na hakuna upepo jua lote la
mchana limechoma aridhi na kuta za nyumba usiku hakuwez kuacha kuwa na joto
Hili ndio suluhisho. Kuna Nyumba niliwahi kuona hii kitu. Wameweka na wavu wa kuslide kwa ndani ya dirishaUkipata fundi mzuri anakutengenezea inakua na double shutter, ndani kunakua na shutter za wavu alafu nje zinakua hizo.. Hapo mbu utawasikia kwa jirani.