Kwani TANROAD barabarani wasipande miti ya matunda kuliko hii ya sasa

ommytk

JF-Expert Member
Jul 30, 2015
482
1,053
Wadau nakumbuka kipindi cha zamani posts kulikuwa na miti ya mikungu kila kona mpaka maeneo ya Osterbay hadi baadhi sehemu za Masaki.

Ukienda Morogoro kuna barabara ina miembe dodo pande zote yaaani kulikuwa na miti ya matunda barabarani kwanini hii isiwe moja ya taratibu kuliko hii miti ya kizungu faida take moja tu kivuli.

Mfano nimeenda nchi za kiarabu nuingi barabarani wamepanda mitende hii naona inafaa yaani hata minazi kipemba inafaa tu kuliko hii miti, langu wazo tu asanteni.
 
Fikiria embe dodo au fenesi limemuangukia mtu au limeangukia kioo cha mbele cha gari!

Fuatilia miembe inavyo katika matawi au inavyo anguka ovyo wakati wa vuli au masika.

Fikiria miembe inavyo kuwa na matawi mapana sana na kuingia barabarani.

Fikiria tabia ya hatari ya makuti ya mnazi kupeperuka toka kwenye mti na kupiga vioo vya magari.

Labda tupande matunda jamii ya michungwa.

Kumbuka miti yenye mizizi mirefu kama mikungu jinsi ilivyo kuwa inaharibu lami au kingo za barabara au mitaro kule Posta na Oyesterbay.

Hata hivyo umeleta wazo zuri.
 
Wadau nakumbuka kipindi cha zamani posts kulikuwa na miti ya mikungu kila kona mpk maeneo ya osterbay hadi baadhi sehemu za masaki.ukienda morogoro kuna barabara ina miembe dodo pande zote yaaani kulikuwa na miti ya matunda barabarani kwanini hii isiwe moja ya taratibu kuliko hii miti ya kizungu faida take moja tu kivuli mfano nimeenda nchibza kiarabu nuingi barabarani wamepanda mitende hii naona inafaa yaani at a minazi kipemba inafaa tu kuliko hii miti langubwazo tu asanteni
Miti yoyote yenye mizizi inayosambaa na minene inayoweza kujongea umbali mrefu huwa sio rafiki sana kwa barabara na pia wakati mwingine kuipanda karibu kabisa na nyumba yako labda hiyo inaweza kuwa pengine ni sababu ya hiyo miti unayoitaka wewe kutopandwa barabarani.

FACT, nyingine umri wa ukuaji wa mti inachangia kupewa kipaumbele kupandwa barabarani mfano:- mti kukua hata walau mita mbili tu ni jambo la kuchukua miaka 20.
 
Huu ujinga wa kupanda ma miti yasiyo na faida uliletwa na wakoloni kipindi hicho wanatutawala lengo likiwa ni kutengeneza utegemezi kwa maana watu wakose chakula na wakafanye kazi kwenye mashamba yao

Wakoloni waligundua matunda yaliyopo kwenye mazingira yanasaidia sana kukinga njaa na pia yanapunguza matumizi makubwa ya vile vyakula vya msingi kama mahindi, mchele na ndizi

Kwa hivyo ikafanyika kampeni ya kundoa miti ya matunda kwenye mazingira

Ukiacha sababu za kihandisi za kutopanda miti ya matunda barabarani hasa barabara kuu, utaona hata kwenye ma taasisi wamepanda miti ya hovyo isiyokua na faida yoyote mfano kwenye viunga vya shule za msingi secondary na vyuo

Hata kwa baadhi ya watu unaenda kwake unakuta kapanda ma miti ya ovyo ovyo lakini hana mti hata mmoja wa matunda.

Kule Isimani Iringa walikua na kampeni ya kupanda miti ili kutunza mazingira, hiyo aina ya miti waliyopanda sasa ni kituko tupu, mpaka unajiuliza hawa watu wanatumka akili au makalio kufikiri.
 
Panda minazi halafu ikianza kuzaa uje utuambie hivyo vioo vya magari vitasamilika vipi. Actually kupaki gari chini ya miti ya matunda ni risky sana, tawi la mnazi likikatika linaweza kuharibu gari yako na safari ikaishia hapo.
 
Wanataka ipanwe mipalachichi, michungwa au mikungu nk, matunda yasiyoweza kuleta madhara.

Msimu wa mavuno ukifika kuwepo na wakala wa mavuno.
 
Miti ya matunda ni hatari labda sijajua umbali unaosemea ila kwa ninavyoona wanavyopanda ni hatari kwa most of miti mingi mfano Maembe, Maparachichi, Mafenesi n.k

Hata hivyo kuna baadhi ya miti ambayo inaweza pandwa kama machungwa, Mapera n.k ila bado distance kidogo inabidi isiwe karibu sana. Chukulia mtu yupo kwenye spidi ghafla chungwa au tawi la mti linaanguka kwenye gari kwa juu au kwenye kioo.

Hiyo inaweza mshtua na kusababisha mengine ambayo ni hatari zaidi au ata kuvunja vioo/kioo na uharibifu mdogo mdogo wa apa na Pale.
 
Wadau nakumbuka kipindi cha zamani posts kulikuwa na miti ya mikungu kila kona mpk maeneo ya osterbay hadi baadhi sehemu za masaki.ukienda morogoro kuna barabara ina miembe dodo pande zote yaaani kulikuwa na miti ya matunda barabarani kwanini hii isiwe moja ya taratibu kuliko hii miti ya kizungu faida take moja tu kivuli mfano nimeenda nchibza kiarabu nuingi barabarani wamepanda mitende hii naona inafaa yaani at a minazi kipemba inafaa tu kuliko hii miti langubwazo tu asanteni
Well Said. Nilienda Marakhesh Morocco kila mti Barabarani ni Ndimu, Limau au Chungwa au Chenza. Ukiagiza Juice hotelin ni full Citrus fruits hadi Raha. Huku ni Mwarobaini, palm trees ambazo hata mbao hazivunwi. Hivi hawa Viongozi wanaosafiri kwenda nje ya Nchi huleta Elimu gani ya nje? Bora Mzee Karume alileta Flat za Michenzani na hotel ya Bwawani.
 
Nani atakuwa anakula hayo matunda? Wadau watayavuna mabichi mchana kweupe..
 
Ukifikiria kwa upande wa utunzaji mazingira na kukwepesha ajali barabarani.. bado unataka matunda kila barabara!!! na huko unasemaka ni matunda je yapo kwa Tanroad waliyapanda au watu binafsi walio na hayo maeneo?
 
Well Said. Nilienda Marakhesh Morocco kila mti Barabarani ni Ndimu, Limau au Chungwa au Chenza. Ukiagiza Juice hotelin ni full Citrus fruits hadi Raha. Huku ni Mwarobaini, palm trees ambazo hata mbao hazivunwi. Hivi hawa Viongozi wanaosafiri kwenda nje ya Nchi huleta Elimu gani ya nje? Bora Mzee Karume alileta Flat za Michenzani na hotel ya Bwawani.
Wakienda huenda kushangaa na kula bata tu,hayo ya kujifunza hawana moango nayo.
 
Back
Top Bottom