Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 92,001
- 112,619
Nazungumzia ratiba ya kuwapeleka mafisadi kwenye mahakama ya mafisadi na kuwafungulia mashitaka. Inawezekana labda aliwahi kuitoa au kuitaja hiyo ratiba lakini mimi ama sikuiona au sikuisikia.
Hivyo, ndo maana nauliza hapa. Kama kuna anayejua nitamshukuru akitufahamisha sie tusiojua. Aliwahi kuahidi kuwa fulani na fulani atawapeleka kwenye hiyo mahakama na atawapeleka lini?
Kikubwa kilichonifanya niulize ni kile kilichotokea jana kwa wale watu wawili [Harbinder Sing na James Rugemalira] kukamatwa na kupelekwa mahakamani kujibu tuhuma dhidi yao.
Inavyoelekea watu walio wengi hawakuwa wakitegemea kuwa hao jamaa wangekamatwa hiyo jana. Na ndo maana kitendo cha wao kukamatwa kimepokelewa kwa mshangao, furaha, na wasiwasi.
Sasa, kuna wale ambao wanahoji kuwa kama Lowassa ni fisadi kwa nini hapandishwi kizimbani. Ndo nami swali linalonijia ni hilo kwenye kichwa cha mada.
Sijui labda watu walitaka kumwona yeye akiwa wa kwanza kupandishwa kizimbani kujibu hizo tuhuma dhidi yake au sijui wanataka kuona kila siku kuna mtu mpya anapandishwa kizimbani!
Muhula wa huyu Ngosha ni bado sana kuisha. Bado ana zaidi ya miaka miwili ndipo amalize muhula wake wa kwanza.
Tayari keshaonyesha kuwa ni mtu ambaye hatabiriki kirahisi wakati mwingine. Hivyo msije shangaa siku moja mnaamka na kumwona [Lowassa] akiwa 'perp walked' nje ya mahakama ya Kisutu.
Hapo naweza hata kutabiri kuwa wengi wenu mnaohoji kwa nini kama yeye ni fisadi hapandishwi kizimbani, mtabadili magoli na si ajabu mkasema kuwa anaonewa kwa sababu za kisiasa.
Vita dhidi ya ufisadi ni vita ndefu na ni endelevu. Mnapokuwa vitani kamanda hawezi ku-telegraph mipango na matendo yake kwani kufanya hivyo kunaweza kumnufaisha adui na akajipanga vizuri ili akushinde.
Siku ya siku ikifika msije kusema sikuwaambia....na msije kulia na kuhamisha magoli hapa!