Kwani ni lazima wawe Wabunge?

Kuzeekea bungeni haimaanishi kuwa wafanyiwe figisu kwenye chaguzi. Hakuna sheria yenye kuweka ukomo wa vipindi vya ubunge
Kuna upumbavu uliopitiliza kwa misukule fulani mkuu.
Mtu anasema fulani amekaa bungeni vipindi fulani,kwa nini asiachie wengine?
Mtu huyo huyo anasema fulani aachiwe amalize kipindi chake cha pili cha urais.
Sasa hapa nashindwa kuelewa. Kunya anye kuku,bata kaharisha!?
 
Kila mtu ana ndoto na matamanio yake. Nakumbuka Mama A.S.Makinda hakuwa anapenda siasa,lakini alivyoingi siasani na kuona utamu wake,alisema atastafia humo siasani,na kweli ndivyo ilivyokuwa.
Kumkatisha mtu ndoto au matamanio yake (ambapo havunji sheria) ni udikteta mambo leo.
 
Labda tunatofautiana ni nini maana ya kufanikiwa kwa kila mtu!

Mimi maana yangu ya kufanikiwa ni. kupata kile ninachokipenda bila kuvunja sheria za nchi.

Kama ninaupenda ubunge basi si sahihi kuniengua kifigisu hata kama nimekaa bungeni miaka 50.

Hata huko Marekani kuna "Wabunge" wamekaa humo bungeni hata miaka 30 na wenhine wamekufa wakiwa wabunge,, akina John Lewis, Senators kama Teddy Kennedy, John Mccain, hatu huyo Biden mwenyewe alikuwa Senator kwa miaka kibao huko. Kwa hiyo as long as sheria zinaruhusu na mtu anapendwa basi its OK. Tatizo labda ni kwa wale wanaobanwa na sheria kisha wanajaribu kuzifinyanga ili waendelee kupata wakitakacho
Kama ujavyo hata huku Marekani Kuna Wabunge waliokaa muda mrefu wakaangushwa ama kwenye Kura za maoni au kwenye Uchaguzi....wameendelea na maisha nje ya Bunge..hata walikuwa wanaenda Sana kuwemo hump...
 
Kura za maoni Marekani kwa maana ya primaries huwa zinapigwa na wanachama. Ni popular votes mostly. Hakuna figisu za kuhonga wajumbe wakupitishe. Ni wanachama wanapiga kura.

Kwa hiyo mtu akiangushwa kwenye hizo kura, inakuwa ni matakwa ya wananchi.

Tofauti na Tanzania wanaweza kukaa wajumbe wanamkata mtu kwa sababu aliwahi kusimama bungeni na kusema ukweli ambao mwenyekiti hakutaka kuusikia.

Au mwenyekiti mwenyewe anakwambia atamkata mtu yeyote kwa kuangalia alivyoamka siku hiyo. Si katiba, si muongozo, si sera, anajiamulia tu.

Kura za maoni za Marekani ni tofauti na hizi habari za wajumbe.

Na mtu akikatwa kwenye kura za maoni maana yake hata kwenye uchaguzi hafiki kwenye chama chake.

Tulinganishe vitu vinavyolingana.
 
Lakini hata Marekani mtu akishindwa kwenye primaries za chama chake, anaweza bado kugombea kama mgombea binafsi/ huru asiyefungamana na chama cha kisiasa.

Unamkumbuka Joe Lieberman?
 
Lakini hata Marekani mtu akishindwa kwenye primaries za chama chake, anaweza bado kugombea kama mgombea binafsi/ huru asiyefungamana na chama cha kisiasa.

Unamkumbuka Joe Lieberman?
Yeah.

Kwa hiyo kufananisha Tanzania na Marekani ni kufananisha apples with oranges.Two different systems.

Kwa sababu primaries za Marekani mostly wanachama wanapiga kura moja kwa moja. Na pia wagombea wakikatwa wanaweza kugombea kama wagombea binafsi.

Tanzania hatuna hayo.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom