The hammer
JF-Expert Member
- May 17, 2011
- 2,396
- 1,784
Habarini wana jf!
Ni kwanini wizara na taasisi nyingi za serikali huwa hawajibu barua zinazotumwa kwao?
Mfano,taasisi fulani inaweza kutuma majina ya watumishi kadhaa wanaodai serikali..ni kwanini wizara husika isirejeshe majibu kwa kuleta majina yote yaliyokubaliwa madai yao,majina ambayo madai yao hayakukubaliwa na sababu za kutokukubalika.Mara nyingi utumishi(wizara) imekuwa ikileta majina ya yaliyokataliwa ambapo inaweka njia panda watu wengine kwamba hawajui majina yao yalienda au hayakwenda.
Pia kuna watu wanaomba ajira ndani ya serikali na taasisi zake,ingekuwa busara wakipata majibu ya kutoitwa kwenye usahili au ya kutofanikiwa kupata kazi na sababu za kutoitwa kwenye usahili au kupata kazi hii itamfanya anayetafuta kazi kuweza kurekebisha kasoro zake mapema.
Pia ndani ya serikali na taasisi zake mf kwenye halmashauri kungekuwa na tabia ya kupeleka majibu ya barua zao hata kwa e-mail iwapo mtu huyo ameweka e-mail katika barua yake hii ni kutokana na kuwa watumishi wengine wanafanya kazi mbali na halmashauri au makao makuu ya taasisi fulani hivyo kuweka majibu kwenye file tu inaleta usumbufu mwingi kwani mtu anaweza kwenda eneo husika kuangalia majibu ya barua zake akakuta haijashughulikiwa hivyo mfanyakazi anakuwa amepoteza siku bila kufanya kazi na pia anakuwa amepoteza fedha.
Kuna mtoto Mtanzania sikumbuki vizuri ni wa wapi,alimuandikia Obama barua na alijibiwa na Obama mwenyewe ile barua yake,kwanini hapa kwetu tunashindwa kujibu direct kwamba majibu yamfikie mhusika na copy ibaki kwenye file lake?Hapo shida ipo wapi.
Serikali ingeidhinisha matumizi ya e-mail pia kama njia ya mawasiliano kati ya wizara na taasisi zake na pia kati ya taasisi na wafanyakazi/mfanyakazi.
Nimewahi kufanya kazi katika kampuni fulani binafsi,hakika pale hakuna mambo ya kupewa maagizo ya kazi kwa njia ya makaratasi..zinatumika e-mail peke yake,hakuna individual file pale na makaratasi yaliyipo ni yale yanayohusu mikataba mbalimbali...
Matumizi ya e-mail yana athari gani wadau kwa serikali.