Kwani kuna mtu anawaza wala kuongelea kodi (tax)? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwani kuna mtu anawaza wala kuongelea kodi (tax)?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Uswe, Apr 10, 2012.

 1. U

  Uswe JF-Expert Member

  #1
  Apr 10, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,201
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Kodi ni agenda kubwa sana, ni kitu unategemea wanasiasa wangekua wanakiongelea sana lakini kwa nini hapa kwetu sisikii wanasiasa wakiongelea kodi.

  Kuna mambo mengi ya kuongea katika suala la kodi na ni kitu muhimu kwa maendeleo.

  1. Kodi inalipwa na kina nani
  Hapa nategemea mjadala mkubwa kuhusu nani alipe nini, lakini hapa kwetu kimya! nategemea kuwe na hoja kwamba wanaoingiza pesa zaidi walipe zaidi, nilitegemea kuwe na hoja ya namna gani serikali itapanua wigo wa kodi, namna gani shughuli zisizo rasmi, kama sanaa na baadhi ya biashara zikatengenezewa utaratibu na zikalipa kodi. . . ila hoja kubwa hapa natamani iwe kuijadili vizuri hiyo kodi na mgawanyo wake, ninaamni hii serikali inawabana sana watu wa kati (waajiriwa) kuliko hao wenye mihela mingi walio nje na ajira rasmi ambao wao ndio wenye pesa nyingi zaidi.

  2. Kodi inayokusanywa inatumikaje.
  hapa ndio kidogo huwa nawasikia wanasiasa wanapigapiga kelele, lakini hawatuambii in details, sioni kama kuna analysis zozote huwa wanafanya kwa mfano kama kiasi flani tunainvest katika jambo flani, say elimu ya chuo what is the return, kama tunaweka katika barabara, maji, umeme badala ya kununua shangingi tutakua tumetoa ajira kwa watu wangapi, tutakua tumeboresha afya kwa kiasi gani nk, kwa nini wanasiasa wetu wanaongea mambo juuu juu tu?

  nimetoka kumsikiliza obama na Buffett rule yake ambapo ni Tax Plan aliipendekeza mwaka 2011 kwa ajili ya kupunguza income inquality, hoja yake kubwa ni wale wenye mamilioni ya dola basi walipe 'fair share' kama kodi, obama anasema, 'those with more opportunities (ambazo huwa wanapata humohumo nchini) have more scope of responsibility'

  The plan is named after American investor Warren Buffett, who publicly stated in early 2011 that he disagreed with the rich paying less in federal taxes, as a portion of income, than the middle class, and has voiced support for increased taxes on the wealthy.

  Mi sijawahi kumsikia rais wetu au hata mwanasiasa akija na hoja yeyote kuhusu kodi na akazunguka nchi nzima kuitetea kwa kuwaelewesha wananchi anajenga hoja ipi na kwa nini.

  Wakati kodi ni nguzo muhimu katika serikali yeyote kwa nini hapa kwetu kodi si hoja kabisa, hakuna mtu anaiwaza wala kuiongelea?
   
 2. N

  Njaare JF-Expert Member

  #2
  Apr 11, 2012
  Joined: Sep 26, 2010
  Messages: 1,075
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Dear Uswe,

  Hapa huwezi kumsikia mwanasiasa akiongelea issue za kodi kwa maana wengi wanaingia kwenye siasa ili kufaidi unafuu wa kodi au kutokulipa kabisa. Kama si kwenye biashara zake basi kwenye biashara za waliomfadhili akaingia kwenye siasa. Ndo maana huwezi kusikia wakiongelea ukusanyaji wa kodi maana kila mwanasiasa ana kampuni analolisimamia ili lisilipe kodi ipasavyo.
   
 3. U

  Uswe JF-Expert Member

  #3
  Apr 11, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,201
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  hicho ndicho kinachoshangaza, wao ndio income kubwa wao tunategemea ndio walipe kodi kubwa zaidi kwa sababu wengi wao hawahitaji hiyo misamaha ya kodi, kinyume chake wao ndio wanapata unafuu wa kodi
   
 4. Adharusi

  Adharusi JF-Expert Member

  #4
  Apr 11, 2012
  Joined: Jan 22, 2012
  Messages: 10,630
  Likes Received: 3,014
  Trophy Points: 280
  Muhimu vilevile waelewe atuliziki na matumizi ya kodi zetu
   
Loading...