Kwani kubandika kope lazima?

PRJ2012

Member
Oct 10, 2019
30
25
Siku hizi kuweka contact lens na kubandika kope imekuwa habari ya mjini. Ni wadada wachache sana ambao hawafuati trend hii.

Ila sasa jamani dada zangu mnapobandikwa vibaya kope huwa hamuoni? Shida ni kukosa wataalamu wa kazi hizi au mnafanya kwa bei chee? Kiukweli muda mwingine unatamani kuuliza mtu amekumbwa na nini usoni ila ndo hivyo tena sio kazi yako.

Macho ni sehemu sensitive sana jamani na inahitaji umakini mkubwa. Kuna urembo wa kuacha tu upite usilazimishe kufanya kila kitu utajikuta unapofuka bure.

Kuna wengine wanapendeza lakini 😂
 
Na wanapendeza kweli, honestly huwa natamani kufanya hivyo pia ila hapana aseee
 
Macho yanakuwaga kama ya mdoli kila saa yanacheza cheza.

Waweke wenye kuweza mimi hapana kwa kweli.
Mwanamke akiingia kwenye salon hizo akitoka huwezi kumjua, macho yanakua kama ya paka, nyusi zimetindwa na kupakwa wanja wa "mbona huntongozi", kope hizo sasa dah! Amakweli ukitaka uzuri sharti udhurike
 
Niliwahi kubandika kope siku moja..ule usiku sikulala ..niliamka mwenyewe kuzibandua .

Nikaapa sitobandika kope Wala kucheza na macho yangu na kitu chochote kile.
 
Similar Discussions

1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom