Kwani hakuna uwezekano wa kufanya hivi wakitaka kujenga Fly Over?

Mkuu hata mimi nilidhani hivyo lakini baada ya kuingia chimbo kwa kuzungumza na mkurugenzi mmojawapo imedhibitika lile jengo ni mali ya tanesço asilimia mia,! Hawana ubia na mtu yeyote. Maana yake ni kodi zetu! Hakuna cha Rostam wala Lowasa wala PPF.
Wa asilimia kubwa ya wasio jua wanadhani hivyo hivyo
 
Inawezekana hata ulaya kipindi wanajenga walibomoaga, habomoi sababu kajiskia ila ni sababu lipo njiani, hata akijenga vipi kama jengo lipo njiani ni lazima libomolewe tu ili kupisha hiyo cjui fly over
 
Inawezekana hata ulaya kipindi wanajenga walibomoaga, habomoi sababu kajiskia ila ni sababu lipo njiani, hata akijenga vipi kama jengo lipo njiani ni lazima libomolewe tu ili kupisha hiyo cjui fly over
fa057e6b9485d7e46a7565a26106a666.jpg
 
Mtajuaje kuwa yeye hajaribiwi na hapangiwi kama bomoa bomoa isipofanyika....

Wabongo hebu eleweni kauli za mkulu buana, mbona ni rahisi mno kuzielewa....
 
20040abc39d7fd4dbf91e1c25603297a.jpg
7e0909f842b75bf605a462b89b31fd66.jpg


Baada ya Rais kutembelea miradi miwili ya ujenzi wa Barabara za Juu maeneo ya Tazara na Ubungo, Rais aliagiza kuwa Makao Makuu ya Shirika la Umeme Nchini (TANESCO) lililopo eneo la Ubungo sambamba na jengo la Wizara ya Maji yawekwe alama X tayari kwa kubomolewa kupisha ujenzi wa mradi huo.

Sipingani na Rais yuko sawa katika amri ya kubomoa, ila hoja yangu hakuna uwezekano kufanya kama picha zinavyoonyesha hapa? Maana nijuavyo ni kwamba unajenga Fly Over kuepusha msongamano wa magari wakati huo huo shughuli zingine kama za Ofisi au Kibiashara zikiendelea maeneo hayo. Au hata Ulaya nako wanabomoa majengo wakitaka kujenga Fly Over, Au Ubungo Interchange?

Nawasilisha

==========
Mdau Mwingine
Asipobomoa ataonekana mnyonge ,yeye sio rais ,hana mamlaka n.k anataka kuonyesha nani ndiye boss!
 
Penye pesa hapajawahi kukwama kitu.

Kilikwama kitu kimoja tu, binadamu kuumba (kutengeneza) binadamu.

Ila kila kitu kingine unachojua kinawezekana ukiwa na hela.
tuna pesa ipi hii hii tunayokopa au??

kwann wasifanye kama hapo juu kiacha kulitia hasara taifa
 
Mleta hoja, kuna watu hawatataka kuiona hoja yako kwa sababu: watakosa dili kwenye hayo (politicians), beside I don't think if we have enough qualified engineers, archtectures and q/surveyors to man such a project.
 
Walishajaribu kumuita hapo mwanzoni hilo jina, it didnt take long wakagundua JPM ni mumber nyingine kabisa! kupunguza speed sahau, labda kuongeza.
Itakuwa hawakuspecify soda ipi, mimi nimependekeza Fanta, mana povu lake halizidi kwenye mdomo wa chupa. Ukisema povu la soda inajulikana ni Coca cola, sasa coca cola ukiwa unaimix na MENTOS.... kasi haipungui leo yaani inaweza kuharibu vitu kabisa
 
Hili la juzi la Magufuli kutoa amri kubomoa jengo la Tanesco pale Ubungo limeniacha hoi. Nilijiuliza, kwa nini asiwaagize mainjinia kumpa mapendekezo ya kutengeneza flyover bila kubomoa jengo la Tanesco? Hivi hajui kwamba kuwa na jengo la Tanesco pale Ubungo pamoja na flyover pia kungetoa taswira ya kipekee sana? Labda nimuelewe kuwa kaamuru hivyo kwa kuwa, kama alivyosema, yeye ndio raisi - anaweza kuamua chochote hata kama hakina busara na hakuna wa kumpinga!

Kisha nikakumbuka kwamba katika kutembea kwangu nimeona hilo likifanyika, Johannesburg, Cape Town, Dubai na kwingineko. Wakati huo huo nikakumbuka kuwa kumbe Magufuli hawezi kuelewa hili kwa kuwa yeye ametembea sehemu chache sana hapa duniani, kwa hiyo hajui kinachoendelea!

Labda ushauri wangu wa bure kwa Magufuri ni kwamba hata kama wewe ndio raisi - na hakuna anayepinga hilo - waachie wataalamu wanaohusika kufanya maamuzi ya vitu vya kitaalamu. Wasiliana na wataalamu kabla ya kutoa matamko ambayo mengi ni impulsive na mara nyingi yanatutia hasara tu kama Watanzania.

Angalia hapa chini wenzetu walichofanya wakati wa kujenga flyovers;

Johannesburg
upload_2017-12-1_11-12-30.png


Cape Town

upload_2017-12-1_11-13-7.png


Dubai
upload_2017-12-1_11-13-47.png


Kwingineko
upload_2017-12-1_11-14-26.png
 
Umenena vema mkuu..Ila natamani engineers wa humu JF waje watudadavulie pia ulazima wa kuvunja jengo lile
 
Unatakiwa kuwa na uhakika ukiwa unasema hasa kwenye v2 kama hv vya maendeleo, Je? Una uhakika kama hakuna ushauri aliofuata.
 
Back
Top Bottom