Kwani demokrasia ni kuchagua wabunge wa CHADEMA na ACT-Wazalendo?

Wakudadavuwa

JF-Expert Member
Feb 17, 2016
17,506
15,997
Ndugu zangu,

Baada ya Watanzania kutafsiri kwa vitendo umuhimu wa maendeleo ya watu na vitu kumeibuka mjadala mpya wa eti kwa sababu wagombea wa ACT na CHADEMA hawajachaguliwa basi hakuna demokrasia.

Hivi demokrasia ni lazima kuwe na wabunge mchanganyiko? La hasha!

Kama hawata kaa chini kutafakari chanzo cha anguko lao hakika watapotea.

Kuna ubaya gani Mbunge aliyekaa Bungeni kwa zaidi ya miaka kumi kama akina Mbowe, Zitto na wenzao wakipigwa chini? Je, wana jambo lolote jipya kwa wananchi? La hasha!

Demokrasia haimaanishi kuwa lazima wabunge CHADEMA au ACT-Wazalendo wachaguliwe.
 
Uko sawa mkuu,pia uchaguzi wa mwaka huu tofauti kabisa na chaguzi zote,umekuja na aina mpya ya campaign.Uchaguzi wa mwaka huu ulikuwa ni juu ya maswala(ISSUES) na bla bla.

CCM walijiuza kwanza kwa kueleza WAMEFANYA nini miaka mitano iliyopita (wananchi wanatafakari na kuona kweli)Kiisha wanaomba kura na kuwaambia wanachi WATAFANYA nini miaka mitano ijayo(wananchi wanaona kuwa ni kweli maana waneona nini kimefanyika).
Ukienda upande wa pili hupati picha.

Mgombea kila kukicha issue ni yeye kupigwa risasi,kumtukana aliyeko madarakani,kulalamika,na kwa bahati mbaya sana kujichanganya,alichosema leo anasahau na kurukia kingine-mifano.

Kabla ya uchaguzi alisikika akisema watamshitaki Magufuli kwa kuwa amefanya campaign kwa miaka mitano baadaye amegeuka na kushangaa inakuwa ccm wameshinda wakati wao wamefanya mikutano mingi kuliko Magufuli?Sasa hapa uchue lipi?

Pili alisikika akisema wao wanataka maendeleo ya watu na sio vitu,Mara kauli hiyo akaisahau alipopand mwendokasi kwenda shopping kariakoo,akasikika akisema usafiri huu ni mzuri unapaswa uenezwe mji mzima EBO sasa ukienezwa mji mzima inakuwa maendeleo ya watu au vitu? Mtu kama huyu unamuelewa vipi?

Tatu amekuja na sera ya majimbo,alipobanwa kidogo tu hakuzungumza tena kuhusu majimbo.Sasa watu watakuelewaje?

Nne Kaja wa wakili Mr Armstadaum.Akawa mtovu wa nidhamu kupindukia anamwandikia mkuu wa nchi barua au waraka usiokuwa na heshima,anatisha na kusubutu kusema kwa nini CCM ipo wakati vyama vyote vilivyoleta uhuru vimekufa?

Ebo,mbona ahoji kwa nini Labour Party au Conservative vya Uiongereza bado vipo? Kwa nini haoji Republicane au Democratice vya marikani bado vipo?
 
Mimi hicho kitu kinanishangaza sana tumepiga kura kwa amani watanzania wamechagua maendeleo badala ya blah blah sasa ajabu upinzani walitaka wachaguliwe bila ya kuweka hata chembe ya matumaini kuhusu maendeleo ya nchi.

Mi naona wakulaumiwa ni Lisu kwa kupinga maendeleo labda na Magufuli kwa kutaka apewe betri zote tatu asiwekewe gunzi maana ndio kipenzi cha watanzania na kwa vile anaeleweka kazi yake Basi watu wamemuunga mkono
 
Endelea kuandika ujinga tu..zile buku saba saba ndio basi tena..mmetumika sasa ni wakati wa kutupwa chooni
 
Kamanda chapa kazi
Kungekuwapo na demokrasia unayo sema basi leo taifa lingekua halina mgawanyiko huu kisiasa ..useme kuna usawa ikiwa wengine wanalipwa pesa ili waingize kura kwenye vituo hapana.

Wakati mwingine tushirikishe akili zetu vizuri, tujaribu ficha ujinga
 
Demkrasia ni wagombea wa ccm tu kupita bila kupingwa, akipita wa upinzani bila kupingwa hiyo sio demkrasia
 
Ndugu zangu,

Baada ya Watanzania kutafsiri kwa vitendo umuhimu wa maendeleo ya watu na vitu kumeibuka mjadala mpya wa eti kwa sababu wagombea wa ACT na CHADEMA hawajachaguliwa basi hakuna demokrasia.

Hivi demokrasia ni lazima kuwe na wabunge mchanganyiko? La hasha!

Kama hawata kaa chini kutafakari chanzo cha anguko lao hakika watapotea.

Kuna ubaya gani Mbunge aliyekaa Bungeni kwa zaidi ya miaka kumi kama akina Mbowe, Zitto na wenzao wakipigwa chini? Je, wana jambo lolote jipya kwa wananchi? La hasha!

Demokrasia haimaanishi kuwa lazima wabunge CHADEMA au ACT-Wazalendo wachaguliwe.
Kamwe hiyo tabia yako ya upunguani ni urithi wako wa kudumu.

Kwa vile lengo ni kuwa na bunge la chama kimoja wabunge wa CHADEMA na ACT wa nini tena.

Subirini wananchi wenye mamlaka juu ya mstabali wao wawafikishie ujumbe.
 
Attachments

  • Wabunge-wa-bila-kupingwa.mp4
    1.6 MB
Back
Top Bottom