Kwani CHADEMA inahitaji back up ya waislam ili kwenda ikulu?watuachie uislam wetu wafanye siasa zao

Status
Not open for further replies.

Farudume

JF-Expert Member
Jan 10, 2013
3,946
3,676
kiini cha hayo uyasemayo ni ushirikishaj wa chombo cha bakwata kiholela katika maslahi na shughui za waislam

na muasisi anafahamika,tunachofanya sisi ni kukemea kwa kila mmoja pasi na kuangalia huyu anatokea chama gani au ni wa dini gani

Kama ni hivyo kwa nini Mlishindwa Kumkemea Kikwete na CCM walipokuwa wanapiga Kampeni Misikini na kuwahadaa kuwapa Mahakama ya Kadhi?Baada ya kushindikana ndio mnakuja kuumbuana,hatutaki unafiki.
 
THE BIG SHOW

JF-Expert Member
Feb 28, 2012
14,805
9,662
chadema wabunifu sana.....wametafuta imam fake kurubuni waislam kusudi tu ya kupata kura zao, wakiingia mkenge watatupwa kuleee kama zito!!
sote hatujasahau mchango mkuu wa zito (wa2 baada ya slaa!) ktk chadema lakini leo hii opportunist lema kawa mali ili hali kajiunga majuzi tu kusaka ubunge baada ya kushindwa alikotoka (tlp)!!
leo lema anaamrisha zito afukuzwe ndani ya chama kwa sabb tu ya 'ukaribu' na wenye chama (mtei na mbowe), maajabu haya!!!
kwa muktadha huu, bora maccm yaendelee kushika hatamu 2015 kuliko giza nene ktk future ya chadema!

wajitahid kuweka utaifa mbele,iman za watu ziko complicated sana,hawataziweza
 
THE BIG SHOW

JF-Expert Member
Feb 28, 2012
14,805
9,662
Kama ni hivyo kwa nini Mlishindwa Kumkemea Kikwete na CCM walipokuwa wanapiga Kampeni Misikini na kuwahadaa kuwapa Mahakama ya Kadhi?Baada ya kushindikana ndio mnakuja kuumbuana,hatutaki unafiki.

mimi nazungumza hapa kama muislam,na sio mwanasiasa

hilo unalolisema nimeshalisema pale juu,angalia tena bandiko langu kwa umakin

shukran sana
 
kajirita

JF-Expert Member
Jul 27, 2013
1,575
633
Nadhani mmeanza KUPANIC mapema!

Mbona hoja hizi hukuzitoa wakati JK anajipitisha misikitini na msemo wa "ni muda wetu wa kuitafuna nchi?"

Au ndo mmeshagundua rais wa tano wa Tanzania LAZIMA awe MKRISTO?

Poleni lakini MTUVUMILIE tu,maana na sisi muda wetu wa 'kutafuna nchi' umekaribia!

TULIA MNYOLEWE!
 
Babu Kijana

JF-Expert Member
Jan 24, 2013
574
260
Ni vizuri sana nimependa ulivyoflow, mie kinachonishangaza baadhi ya waislam kutumika kwa maslahi ya dunia, huyo Said ni darasa la saba amewekwa tu kuhalalisha dhana ya udini ndani ya CDM..Mie namshangaa yeye la 7 hata sauti ndani ya chama sauti hana..Mungu amlipe na amuongoze katika uongofu kwani jambo alilolifanya ni la kupgwa vita sana!
 
THE BIG SHOW

JF-Expert Member
Feb 28, 2012
14,805
9,662
Unalalamika kwamba kuna rais kutoka CCM hakuwaanzishia Mahakama ya Kadhi kama alivyoahidi
Unalalalamika pia kwamba kuna rais mwingine kutoka CCM aliwaanzishia BAKWATA.
Chombo kimoja mmeanzishiwa, mnalalamika. Chombo kingine hamkuanzishiwa, mnalalamika tena.

Sasa tupeni msimamo mmoja, mnapenda au hampendi kuanzishiwa vyombo vyenu na serikali?

kama vile serikali isivyowaingilia watu wa iman zingine

ndivyo hivyo hivyo tusivyotaka sisi wasituingilie
 
THE BIG SHOW

JF-Expert Member
Feb 28, 2012
14,805
9,662
Nadhani mmeanza KUPANIC mapema!

Mbona hoja hizi hukuzitoa wakati JK anajipitisha misikitini na msemo wa "ni muda wetu wa kuitafuna nchi?"

Au ndo mmeshagundua rais wa tano wa Tanzania LAZIMA awe MKRISTO?

Poleni lakini MTUVUMILIE tu,maana na sisi muda wetu wa 'kutafuna nchi' umekaribia!

TULIA MNYOLEWE!

its not a war between christians and muslims

its a war between tanzanians and politicians

jaribu kujielewa
 
Mbelwa Germano

JF-Expert Member
May 7, 2011
789
289
CHADEMA,
Inafuata mkondo ule ule,
Kwa mara nyingi sana na kwa muda mrefu chadema imekuwa kwenye shutuma za malumbano na wanasiasa wenzao wa CCM ya kwamba kwenye chama hiko kuna kasumba za udini na kubaguliwa watu wenye iman ya kiislam kwa wazi wazi bila sababu za msingi,
Inawezekana jambo hilo likawa na uhalisia au lisiwe na uhalisia,ila hoja yangu kuu hapa ni kwamba CHADEMA kama chama,kitafute namna ya kupambana na wapinzani wao kwa utaratibu wao huo huo wa kisiasa,

Wasitake kutafuta sympathy kwa kuchukua baadh ya watu wahun wahun na kuwavisha uislam,kuwavisha madaraka ya uislam kama huyo SAID MOHAMED,makamu mwenyekiti wa chadema zanzibar ili kufikia malengo yao ya kisiaisa kwa kutafuta backup ya waislam.

Tunapinga jambo hilo,mimi sio msemaji wa waislam,.ila mimi ni miongon mwa waislam nilioudhika kwa kitendo hiko kama nilivoudhika kwa vitendo alivyofanya NYERERE kwa waislam,na kama vitendo walivyofanya CCM kwa waislam.

Tunajua uislam unapigwa vita na dunia yote kwa sasa,na tunajua wakati mgumu tunaoupitia,ila sio kwamba hatufaham namna ya kuzikabili changamoto kama hizo,

Tunawaambia chadema kama sample ya wanasiasa wengine waachane na waislam na uislam kama wanataka kuwa salama katika harakati zao,
Sisi hatuwez tumiwa na wanasiasa hata kdgo eti kwa maslahi yao ya dunia,sisi hatuwez kuwa subset ya wanasiasa na siasa zao,

Uislam kama uislam ni mfumo uliokamilika na kujitosheleza kwa kias kikubwa sana,lengo letu ni kuish maisha yanayompendeza mola wetu hapa ulimwenguni na kesho tuweze pata stahiki yetu akhera.

Kama chadema inaamua kutumia proportions ya vingoz wa dini ya kikristo waliopo ndan ya chama chao na kutaka kupandikiza viongoz fake wa kiislam ili kufanikisha kujikwamua kwenye vita vyao dhidi ya CCM,sisi tunawaasa kwamba hilo halitawafikisha mbali,kwani sisi tuna maisha yetu mahususi ambayo hatuhitaji kuingiliwa wala kutumiwa kwa maslahi ya watu fulani.

Ndug zangu waislam,hili suala na mengine kama haya yanapotokea tusiposimama kidete kuyakemea wanasiasa kama hawa wa chadema na wengneo wanaweza dhan sisi ni watu rahis rahis kama wanavyodhania kwa watu wengine.

Naomba Kuwakilisha.

Moja,propapanda ya Udini au dhana nzima ya udini muasisi wake ni CCM na wamefanya hivyo kwa malengo mafupi ya kisiasa "Kushinda Uchaguzi" kwa kuwagawa wakristo na waislamu. Kumbuka walisema/wanasema CUF ni waislamu,CHADEMA Wakristo hivyo kuhatarisha umoja wa kitaifa.

Mbili,umeonyesha chuki za wazi dhidi ya SAID MOHAMED na kumfananisha na "wahun wahun" sababu amezungumzia Uislam akiwa CHADEMA na kuhalalisha wazi kwamba wewe binafsi una mentality ya kidini na chuki dhidi ya wakristo na CHADEMA.

Tatu,Kwa kusema kwamba SAID MOHAMED ni "mhun mhun" umehalalisha kwamba viongozi wote wa kislamu ndani ya CHADEMA ni wahuni,Marehemu Bob Makani alikuwa mhun mhun,Prof.Safari ni mhun,Said Arfi ni mhun n.k. na hivyo kuhalalisha uwezo mdogo cha kifikra ambao umesababishwa na fikra za kibaguzi.

Tatu,Alichofanya SAID MOHAMED ni kung'oa hii mentality ya udini na si kumtumia Muislamu au Mkristo kwa manufaa ya kisiasa.Ni kujenga umoja wa kitaifa na si ubaguzi wa kidini kwenye mwamvuli wa kisiasa.Hakuzungumzia Muislamu kwa maana ya kumchukia Mkisto bali kusimamia matendo mema bila kupotoshwa kwa kutumia mwamvuli wa udini.

MWISHO, kwa mtu mwenye uwezo wa kuona mambo kwa uhalisia kwa kutumia fikra zake bandiko lako linajaribu kujenga ubaguzi na sio kubomoa ubaguzi,linaendeleza chuki.
 
FUSO

JF-Expert Member
Nov 19, 2010
29,499
33,848
Mleta hoja kumbe kazi yako ni kuhesabu waislamu wangapi ni viongozi ndani ya vyama vya siasa? kama hivyo basi kazi unayo.

Sisi tunaangalia ni chama gani kina lengo thabiti la kuwakomboa watanzania kwenye lindi la umaskini - hata iwe CUF, CCM, PPT maendeleo mimi sintajali inaongozwa na Mpagani, Mwislamu ama Mkristo - cha msingi nahitaji mtu atakanifanya nipate haki zangu ninazostahili kama mtanzania mzawa wa nchi hii.

Haya ya kuhesabu viongozi na madhehebu yao wewe endelea nayo.
 
Ralphryder

JF-Expert Member
Nov 16, 2011
4,853
1,135
Tokea lini chadema iliwapenda waislam? Chadema ni wanafiki na sijui huyo mnywa ulevi wa Jang'ombe wamemwokota wapi kutumika kama kikaragosi! Chadema mtume wetu wanamwita Malaya, mbakaji,mwamedi, na Allah wanadai ni shetani! Vp kumtumia huyo Saidi mlevi kuwasaidieni!
 
JERRY

JF-Expert Member
Feb 18, 2009
629
499
Miongoni mwa kosa kubwa ambalo wanasiasa ama kwa kutoliona au kwa kukusudia kabisa ni hili la wanasiasa la kudhani kwamba kwa kutumia sympathy ya waumin wa dini fulani basi itawasaidia kuwavusha katika changamoto zao za kisiasa na kufanikisha malengo yao ya kuingia ikulu.

Mimi nataka kuchukua kama case study kwa dini yangu,mimi muislam na namna ambavyo wanasiasa wamekuwa wanachukua nafasi zao kwa nyakati mbali mbali kujiingiza katika uislam na waislam kwa ujumla kuwafanya kama hao watu wa jamii hiyo ni mazuzu,wasiojitambau na kuingiza malengo yao kwao kwa matumain ya kupata backup yao na uungwaji mkono.

Hili limetokea mfano kipindi ambacho JK alikuwa anajiandaa kuingia ikulu kwa awamu ya pili ya utawala wake kwa wazi wazi kabisa,kwan CCM ilisimama kidete kuwarubun baadhi ya viongoz wa kiislam hususan wa bakwata na kuwaambia kwamba wawashawish waumin na kuwaambia kwamba endapo CCM itachukua dola basi itahakikisha inawasaidia kuanzisha mahakama ya kadhi na mambo kama hayo,kama hiyo haitoshi ilijinasibu kwa kuweka vipaombele vya waislam kama group linalojitegemea kipekee katika jamii ya watanzania.

Mimi kama Muislam haikunishangaza hata kidogo kwa CCM kutumia janja kama ile,ila niliumia kwa kuona ni kwa namna gani wanasiasa wanajaribu kucheza na hisia zetu katika mambo ya msingi yahusuyo iman zetu kwa maslahi yao kwa dunia yao.

Hili lilianzia tokea enzi ya Julius Kambarage Nyerere,yeye ndie kinara wa haya tunayoyaona kwa sasa na wanachokifanya wengine ni muendelezo tuh wa legacy yake,

Wote mtakuwa mnakumbuka kwamba kwa kias kikubwa sana waislam wameshiriki katika pilika pilika za kudai uhuru wa nchi hii kama group moja linaloojitegemea mingoni mwa magroup mengine yaiyokawepo katika zama hizo,
Na waislam walifanya hivyo sio kwa sababu ya kwamba wallikuwa wanataka kuismamisha dola ya kiislam la hasha,
Walifanya hivyo kwa kuwa wanajua fika kwa mujibu wa mafundisho ya iman yao utumwa,unyanyasi na ukoloni ni dhambi na dhulma kubwa kwa mwanadamu,na kwa mujibu wa mafunzo ya iman yetu tunaambiwa tuipinge dhulma kwa njia zote,thats why unaweza kuona kwamba waislam walisimama kidete kupigania uhuru kwa maslahi ya kujiweka huru na kuliweka huru taifa zima kwa ujumla.

Nyerere kwa kuona juhudi zile,aliingia na taharuki ya kibinadamu kwa kuona nguv ambayo waislam walikuwa nayo enz hizo na kwa kuona kwamba wanaweza kuibuka kuwa group hatari kwa baadae kitu ambacho wala hakikuwa na uhalisia,kwa mamlaka yake AKAAMUA KUWAUNDIA WAISLAM CHOMBO CHA BAKWATA ili kiweze kuwaratibu na kuwaregulate mambo yao on behalf of his goverment,pale ndipo palipokuwa kiini cha haya yanayotokea kwa sasa.

Waislam wakawa wanaratibiwa na kupangiwa kila aina ya propaganda na shutuma pasi na sababu za msingi kana kwamba wao sio watanzania au wao sio wananchi huru,hili lishasemwa sana mimi nafanya kama kukumbusha tuh,na sio nia yangu kuleta malalamiko au shutuma,au kuhubiri utengano katika jamii yangu,naipenda jamii yangu kwa utaifa wangu na uzalendo wa hali ya juu,japo siwez kuikanan iman yangu.

CCM, kwa jambo lile walilolifanya kipindi cha awamu ya pili ya JK waislam waliliona na wamejifunza,lakin niweke wazi kwamba ni group dogo sana la waislam ambao waliingia kwenye mtego ule.nalo ni lile lililofanikiwa kurubuniwa na BAKWATA ambacho ni chombo kilichoasisiwa na NYERERE.

CHADEMA,
Inafuata mkondo ule ule,
Kwa mara nyingi sana na kwa muda mrefu chadema imekuwa kwenye shutuma za malumbano na wanasiasa wenzao wa CCM ya kwamba kwenye chama hiko kuna kasumba za udini na kubaguliwa watu wenye iman ya kiislam kwa wazi wazi bila sababu za msingi,
Inawezekana jambo hilo likawa na uhalisia au lisiwe na uhalisia,ila hoja yangu kuu hapa ni kwamba CHADEMA kama chama,kitafute namna ya kupambana na wapinzani wao kwa utaratibu wao huo huo wa kisiasa,

Wasitake kutafuta sympathy kwa kuchukua baadh ya watu wahun wahun na kuwavisha uislam,kuwavisha madaraka ya uislam kama huyo SAID MOHAMED,makamu mwenyekiti wa chadema zanzibar ili kufikia malengo yao ya kisiaisa kwa kutafuta backup ya waislam.

Tunapinga jambo hilo,mimi sio msemaji wa waislam,.ila mimi ni miongon mwa waislam nilioudhika kwa kitendo hiko kama nilivoudhika kwa vitendo alivyofanya NYERERE kwa waislam,na kama vitendo walivyofanya CCM kwa waislam.

Tunajua uislam unapigwa vita na dunia yote kwa sasa,na tunajua wakati mgumu tunaoupitia,ila sio kwamba hatufaham namna ya kuzikabili changamoto kama hizo,

Tunawaambia chadema kama sample ya wanasiasa wengine waachane na waislam na uislam kama wanataka kuwa salama katika harakati zao,
Sisi hatuwez tumiwa na wanasiasa hata kdgo eti kwa maslahi yao ya dunia,sisi hatuwez kuwa subset ya wanasiasa na siasa zao,

Uislam kama uislam ni mfumo uliokamilika na kujitosheleza kwa kias kikubwa sana,lengo letu ni kuish maisha yanayompendeza mola wetu hapa ulimwenguni na kesho tuweze pata stahiki yetu akhera.

Kama chadema inaamua kutumia proportions ya vingoz wa dini ya kikristo waliopo ndan ya chama chao na kutaka kupandikiza viongoz fake wa kiislam ili kufanikisha kujikwamua kwenye vita vyao dhidi ya CCM,sisi tunawaasa kwamba hilo halitawafikisha mbali,kwani sisi tuna maisha yetu mahususi ambayo hatuhitaji kuingiliwa wala kutumiwa kwa maslahi ya watu fulani.

Ndug zangu waislam,hili suala na mengine kama haya yanapotokea tusiposimama kidete kuyakemea wanasiasa kama hawa wa chadema na wengneo wanaweza dhan sisi ni watu rahis rahis kama wanavyodhania kwa watu wengine.

Naomba Kuwakilisha.
Bwana muhammad umeandika vizuri tu, ila tatizo lako hujamuelewi mheshimiwa Said. Alichokisema ni kuwaambia watanzania wakae chonjo za propaganda za muda mrefu za CCM kuhusu CDM na mambo ya UDINI, na ndio maana katika kuweka fair ground akasema kama ni suala la Slaa kuwa padri huko siku za nyuma basi yeye mbona pia ni Imamu wa Msikiti huko pemba mbona hawasemei hilo.
 
The Wolf

JF-Expert Member
Sep 10, 2013
9,104
19,386
Mkuu hoja ni nzuri lakini kuna baadhi ya vitu umeviongelea vinaonyesha you are biased

1. Naomba utuambie na nafasi ya CCM katika kuutumia uislamu kana kinga yao na kuchafua CDM

2. Sawa BAKWATA ilianzishwa na NYERERE lakini hakuwahi kuwa mkuu wa hicho chombo ni nyie wenyewe mnaokiongoza na kama bado kipo controlled na serikali basi ni serikali ya CCM nini maoni yako kuhusu hilo?

3. Kila mtu ana uhuru wa kuwa na kujishughlisha na siasa bila kujali dini yake kwa nini inakuuma wewe huyo mwenyekiti wa zanzibar kuwa CHADEMA?

4. Ukiangalia facts utaona CCM ndio yenye historia na kucheza na hisia zenu za kidini mpaka sasa mbona tuhuma zako umezirusha kwa CDM pekee na siyo CCM au CUF?
 
THE BIG SHOW

JF-Expert Member
Feb 28, 2012
14,805
9,662
Moja,propapanda ya Udini au dhana nzima ya udini muasisi wake ni CCM na wamefanya hivyo kwa malengo mafupi ya kisiasa "Kushinda Uchaguzi" kwa kuwagawa wakristo na waislamu. Kumbuka walisema/wanasema CUF ni waislamu,CHADEMA Wakristo hivyo kuhatarisha umoja wa kitaifa.

Mbili,umeonyesha chuki za wazi dhidi ya SAID MOHAMED na kumfananisha na "wahun wahun" sababu amezungumzia Uislam akiwa CHADEMA na kuhalalisha wazi kwamba wewe binafsi una mentality ya kidini na chuki dhidi ya wakristo na CHADEMA.

Tatu,Kwa kusema kwamba SAID MOHAMED ni "mhun mhun" umehalalisha kwamba viongozi wote wa kislamu ndani ya CHADEMA ni wahuni,Marehemu Bob Makani alikuwa mhun mhun,Prof.Safari ni mhun,Said Arfi ni mhun n.k. na hivyo kuhalalisha uwezo mdogo cha kifikra ambao umesababishwa na fikra za kibaguzi.

Tatu,Alichofanya SAID MOHAMED ni kung'oa hii mentality ya udini na si kumtumia Muislamu au Mkristo kwa manufaa ya kisiasa.Ni kujenga umoja wa kitaifa na si ubaguzi wa kidini kwenye mwamvuli wa kisiasa.Hakuzungumzia Muislamu kwa maana ya kumchukia Mkisto bali kusimamia matendo mema bila kupotoshwa kwa kutumia mwamvuli wa udini.

MWISHO, kwa mtu mwenye uwezo wa kuona mambo kwa uhalisia kwa kutumia fikra zake bandiko lako linajaribu kujenga ubaguzi na sio kubomoa ubaguzi,linaendeleza chuki.

Shukran kwa kuja kujadiiana na mimi ndug mtanzania mwenzangu

Awali ya yote mimi sijaamua kuwagusa viongoz wengine ambao ni waislam walioko chadema kama hao uliowataja kama Prof Abdallah safari,Said Arfi na kadhalika kwa kuwa wao wameamua kufanya siasa na kuacha uislam wao nyumban,kwao,na kuaacha uislam wao misikitini

Hawakuthubutu kuuchukua uislam wao na kuupeleka kwenye majukwaa ya siasa kwa masilahi yao,hicho ndicho najaribu kufikisha kwa watu kama hao

Na kwa mantiki hiyo basi ninayo hoja ya kumwita makamu mwenyekiti wa CHADEMA zanzibar bwana said mohamed kuwa ni muhun kwani yeye kama imamu kazi yake inafahamika ndan ya uislam

Imam ni kiongoz wa ibada kwa waislam,na haruhusiwi kufanya shughuli hiyo ya siasa kwa kutumia backua ya uislam wake au uimamu wake

Lait angekwenda hapo kwenye jukwaa la siasa bila kuutaja uislam na uimamu wake mimi nisingemgusa,ila ni muhun kwa kuwa anajua fika mafundisho yanasemaje ila anaamua kupotosha kwa njaa zake

Chadema hiyo imeshawagharim tayari

Shukran
 
kibaravumba

JF-Expert Member
Dec 21, 2012
6,638
6,989
Nadhani mmeanza KUPANIC mapema!

Mbona hoja hizi hukuzitoa wakati JK anajipitisha misikitini na msemo wa "ni muda wetu wa kuitafuna nchi?"

Au ndo mmeshagundua rais wa tano wa Tanzania LAZIMA awe MKRISTO?

Poleni lakini MTUVUMILIE tu,maana na sisi muda wetu wa 'kutafuna nchi' umekaribia!

TULIA MNYOLEWE!

Mkuu,hizi hoja za udini hazitakiwi ushabiki kama wako huu ni hatari sana!Mimi ni mkristo lakini nakuapia kwa Mungu aliye hai,sijawahi kufaidika na rais mkristo kwa vile tu mimi ni mkristo! kwa hiyo kwangu haileti tofauti kuwa na rais wa dini yoyote ili mradi anatumikia wananchi kwa bidii!Nakuomba kama una nia njema na nchi hii usiongee ushabiki namna hii

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 
mzalendokweli

JF-Expert Member
Apr 21, 2012
579
137
Wasitake kutafuta sympathy kwa kuchukua baadh ya watu wahun wahun na kuwavisha uislam,kuwavisha madaraka ya uislam kama huyo SAID MOHAMED,makamu mwenyekiti wa chadema zanzibar ili kufikia malengo yao ya kisiaisa kwa kutafuta backup ya waislam.
.
Nimependa the way unajenga hoja, japokua sina hakika sana na usahihi wa data unazotumia katika kusukuma hoja zako.
Mfano wa Chadema kumvisha Madaraka Saidi Mohamed; Kwanza napenda kujua kama unafahamu utaratibu uliotumika mpaka Saidi Mohamed kua makamu mwenyekiti wa chadema kwa Zanzibar!
Pili; Kwa mujibu wa CIA Factbook, asilimia 99 ya wanzibari ni waislam... Ukiwa huna misukumo mingine zaidi ya "facts", haitakuwia vigumu kuona kua ukifanya uchaguzi uwezekano wa kupata kiongozi Mkristo kwa zanzibar ni mdogo mnooo kama haupo kabisa. Hii inapunguza nguvu sana hoja yako kua amewekwa ili kupata uungwaji mkono wa Waislam.
 
Status
Not open for further replies.
12 Reactions
Reply
Top Bottom