Kwani Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB) haiwezi kuwa na accounts za malengo kwa wanafunzi wa darasa la kwanza?

Infantry Soldier

JF-Expert Member
Feb 18, 2012
15,893
16,316
Habari zenu waungwana wa humu jamiiforums

Kwanini Bodi ya mikopo ya elimu ya juu (HESLB) isianzishe campaign ya kuhamasisha wazazi kuanza kuwalipia watoto wao pesa kidogokidogo katika accounts maalum ya bodi wangali wakiwa bado wanasoma elimu ya msingi (Darasa la Kwanza)?

Jenga picha mtoto anasoma darasa la kwanza kwa miaka saba (7) kisha baada ya kuhitimu anajiunga na kidato cha kwanza mpaka cha nne kwa miaka minne (4) ambacho kwa sehemu kubwa hapa Tanzania ndicho kiwango cha elimu ambacho wanafunzi anaruhusiwa kujiunga na chuo cha ufundi (kama vile VETA) kama amekosa fursa ya kuendelea na Advanced Level.

MATHEMATICAL BREAK DOWN
==========
Idadi ya miezi ndani ya mwaka: 12

Idadi ya miaka atakayosoma mwanafunzi kabla ya kujiunga na elimu ya juu/ufundi: 11

Kiwango cha chini cha uchangiaji kwa kila mwezi: 8,000/=

Makusanyo ya mwaka mzima kwa mwanafunzi mmoja - 12 x 8,000 = 96,000

Makusanyo ya miaka 11 kwa mwanafunzi mmoja - 12 x 11 x 8,000 = 1,056,000

Kutokana na takwimu niliyoipata humu humu jamiiforums: "Wanafunzi 947,221 wa darasa la saba kutoka shule 17,051 za Tanzania bara, wanatarajia kufanya mtihani wa kumaliza elimu ya msingi kesho Jumatano na keshokutwa Alhamisi Septemba 12, 2019"

Just assume kwamba wanafunzi walioanza la kwanza ndio haohao waliomaliza darasa la saba na hakuna aliyekufa wala kuacha shule na idadi kamili ni 947,221.

Makadirio ya makusanyo ya mwezi kwa wanafunzi wote wa darasa la kwanza - 8,000 x 947,221 = 7,577,768,000

Makadirio ya makusanyo ya mwaka mzima kwa wanafunzi wote wa darasa la kwanza - 8,000 x 12 x 947,221 = 90,933,216,000

Kwa makusanyo kama haya kwa mwezi kwa wanafunzi wote takribani shilingi 90,933,216,000 bodi ya mikopo wanaweza kuwekeza hii pesa katika fixed deposits kwenye banks za kibiashara pamoja na kununua "government securities" na kupata returns kubwa na za maana tu kila baada ya miezi sita au mwaka.

Kama familia ina wanafunzi wawili mmoja akifa pesa zinahamia kwenye account ya mdogo/kaka yake.

Ndugu zangu, mimi sio mtaalam sana wa hesabu na uchumi lakini bila shaka idea yangu mtakuwa mmeielewa. Ninawakaribisha kwa michango zaidi pamoja na kukosolewa (Constructive Criticism)

USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
 
Siyo jambo jema kwa nchi iliyojaa mafisadi na majizi. Hizo pesa zitaishia kwa wahuni wachache na kuzipata itakuwa ngumu kitu ambacho kitakuja kuwafanya wanafunzi kukosa kabisa meals & accommodation allowance, vyuo navyo havitapata ada kwa wakati.
Refer to NSSF, mifuko mingine ya, BIMA YA AFYA n.k
 
Serikali haiwezi kufanya biashara.

ref; nssf
Hii sio biashara mkuu, hapa unaweka pesa kwa ajili ya mtoto wako. Kama mwanafunzi atasoma mpaka kidato cha sita inakuwa hivi;

8,000 x 12 x 13 = 1,248,000

Mtoto wako anapewa mkopo huku tayari akiwa na collateral ya 1,248,000 kwenye account ya HESLB
 
Hizo pesa zitaishia kwa wahuni wachache na kuzipata itakuwa ngumu kitu ambacho kitakuja kuwafanya wanafunzi kukosa kabisa meals & accommodation allowance, vyuo navyo havitapata ada kwa wakati.
Pesa zitaishia vp kwa wahuni wakati kuna documentations? Kwa hiyo Tanzania isisonge mbele kwa sababu ya wahuni wachache?
 
Wazo zuri ila utekelezaji wake ni mgumu hasa ukilinganisha na hali ya umasikini wa kaya. Mfano kaya yenye watoto watatu kijijini huko itabidi itoe 24,000/= kwa mwezi hii hela sio ndogo hata baadhi ya waajiriwa ikifika mwisho wa mwezi hawàna hiyo hela kwenye account
Ndio maana nimesema ni makadirio kwa maana kuna baadhi ya familia zina mtoto mmoja na zingine zina watoto hao watatu na wana uwezo mzuri kabisa wa kifedha.
 
Kwa mfano ikatokea mtoto kafeli hela itarudishwa ???

Au mtoto kafa??

Au mzazi akawa amefariki ni isifikiwe ilo lengo je hela atarudishiwa mtoto???

Au itakuwa kama wanachofanya psssf ??

Wazo ni zuri ila sehemu ambapo linaweza kufanyiwa kazi ndio tatizo
Wamejaa watu wafisadi wanaoangalia maisha Yao tu hawana utu kama psssf hela ni zako lakini unazungushwa wanataka sijui utoe rushwa wakati hela ni zako

Izo hela inawezekan kuwekwa ila kuna uwezekano mkubwa sana wa hizo hela kupigwa na watu wakatumia kwa matumizi Yao binafsi

Ila wazo ni zuri sana ila sehemu litakopo enda kufanyiwa kazi itakuwa tatizo kubwa mno
 
Angalia nyuma yako ulioanza nao darasa la kwanza je la saba mlimaliza nao?

Walioingia form 1 je ndio uliomaliza nao la saba? Umeacha wangapi nyuma? Ulioanza nao form 1 ulimaliza nao wangapi form 4?
Waliomaliza form 4 wangapi wameingia advance au tech school?

Hiyo inaenda mpaka mkimaliza degree ya kwanza.

Mfumo wetu wa elimu ni pyramid. Mnaanza wengi mnamaliza wachache...

Sababu:
1. Kufeli
2. Kukatisha masomo kwa sababu mbalimbali (utoro, mimba) n.k
3. Vifo
4. Umasikini
5. Uhaba wa shule

N.k n.k
Mind you, shule za sekondari haziwezi kumudu wanafunzi wote waliomaliza la saba. The same to advance na same to chuo.

Sasa kwa sababu za hapo juu unawekeza wakati huna uhakika huko mbele kuna nini?
 
Angalia nyuma yako ulioanza nao darasa la kwanza je la saba mlimaliza nao?...
Ndio maana nimesema kuwa hii ni assumption mkuu. Mawazo mengi hutekelezwa kwa misingi ya makadirio. Hata budget za serikali ni makadirio ya mapato na matumizi. Soma tena nilichokiandika.
 
Pesa zitaishia vp kwa wahuni wakati kuna documentations? Kwa hiyo Tanzania isisonge mbele kwa sababu ya wahuni wachache?
Hata NSSF, NHIF kuna document lakini bado pesa zinapigwa na ikifika wakati wa uhitaji wa pesa hizo unakuta hamna kitu. Hatuna mifumo na sheria nzuri za kutunza pesa kama hizo; wakati mwingine wakuu wa nchi wanajifanya kukozikopa hali hawarudishi, wengine wanabeba tu kama za kwao. Naamina unakumbuka sakata la waziri fulani kujichotea mamilioni NSSF na wakati mwingine wahuni hao hao wanachota hadi hazina au benki kuu.

Wasiwasi wangu ni kujirudia kwa makosa yale yale endapo pesa zitawekwa bodi ya mikopo na kutunzwa hadi watoto husika wafikie umri wa kuanza chuo. Pia bodi wameshaonesha ujanja wa kutotoa pesa kwa wanafunzi kwa wanufaika wa mikopo licha ya serikali kutoa pesa hizo kwa wakati, na wakati mwingine wanashirikiana na wakuu fulani wa vyuo kuchelewesha pesa hizo kwa minajiri ya kujinufaisha na riba toka fixed account.

Na kikubwa zaidi hawana biashara ya nzuri na ya kuzalisha hiyo pesa maana kuiweka tu nako ni hasara tupu.
 
10 Reactions
Reply
Back
Top Bottom