Kwamba Serikali ya Tanzania haiwafahamu wenye nyumba kiasi cha kumkata mpangaji kodi ya Majengo ni uongo wa kiwango cha chini sana na ni wizi

Suala hili limeelezwa vizuri sana na serikali na utaratibu umewekwa vyema. Wewe unajaribu kulitumia kufikiri linaweza kukupa millage ya kisiasa. Bahati mbaya kwako watanzania tumelipokea vyema na tunalipa kazi inaendelea. Tafuta lingine
Nilidhani mambo mengi wanayo yapinga wanakuwa na hoja. Kumbe jamaa wanapinga tu, Ndiyo ubora wao.
 
Wenye nyumba tayari wanalipia kodi ya sijui ya kiwanja au ya kumiliki jengo ila wapangaji ni wakwepaji wakubwa wa kodi sasa kupitia luku ni lazima wamewaweka kwenye kona.
 
Kodi ya Majengo imelipwa ndani ya nchi hii kwa miaka na miaka , kwa kipindi kirefu ililipwa kwenye Halmashauri na kuwa mapato ya Halmashauri husika ili kusaidia miradi mbali mbali , mimi mwenyewe nina nyumba 2 kwenye halmashauri ya Temeke , nafahamu ninachoandika , Jina langu linafahamika vema kabisa na Halmashauri hiyo kama wenye nyumba wengine wanavyofahamika , huku kila jengo au nyumba ikirasimishwa kwa kupewa namba Maalum na kubandikwa Ukutani ili kila mtu aone .

Baada ya uchaguzi Mkuu wa 2015 ccm kuangushwa kwa kunyang'anywa halmashauri kubwa kubwa , ikiwemo Halmashauri ya Jiji la DSM , yenye majengo mengi na yenye kulipiwa pesa nyingi , kwa roho yake Mbaya , Rais wa wakati huo Magufuli akaamua kuzinyang'anya kodi ya majengo halmashauri kwa vile sasa zilikuwa chini ya Chadema , na kuamuru wenye majengo wote nikiwemo mimi kulipia kodi hiyo kupitia TRA , rekodi zote zipo na wenye nyumba wote wapo na wanatambulika na tayari walishawekwa kwenye mfumo wa malipo ( japo baada ya uchafuzi wa 2020 kodi hii imerejeshwa tena halmashauri maana chadema hawapo tena ), sasa kuwalipisha watu wasiohusika huku wahusika wanaopaswa kulipa kodi wapo na wanafahamika ni wizi wa kishamba sana uliolenga kutunisha mfuko wa serikali kwa NJIA YA HARAMU .

Kama walipaji walishakuwa kwenye mfumo na wanafahamika , huku kila nyumba mpya inayojengwa ujenzi wake hufanywa baada ya vibali vya halmashauri , kwanini Serikali imeamua kupora pesa za raia wasiohusika ?

Itaendelea ....
Wamepiga hesabu ya idadi ya mita za luku wakaona ni nyingi na zitawapatia pesa nyingi. Walikosa Jina la kuita hayo makato wakaona isiwe tabu, tuite kodi ya jengo. Hakuna zaidi ya hilo.
 
Kodi ya Majengo imelipwa ndani ya nchi hii kwa miaka na miaka , kwa kipindi kirefu ililipwa kwenye Halmashauri na kuwa mapato ya Halmashauri husika ili kusaidia miradi mbali mbali , mimi mwenyewe nina nyumba 2 kwenye halmashauri ya Temeke , nafahamu ninachoandika , Jina langu linafahamika vema kabisa na Halmashauri hiyo kama wenye nyumba wengine wanavyofahamika , huku kila jengo au nyumba ikirasimishwa kwa kupewa namba Maalum na kubandikwa Ukutani ili kila mtu aone .

Baada ya uchaguzi Mkuu wa 2015 ccm kuangushwa kwa kunyang'anywa halmashauri kubwa kubwa , ikiwemo Halmashauri ya Jiji la DSM , yenye majengo mengi na yenye kulipiwa pesa nyingi , kwa roho yake Mbaya , Rais wa wakati huo Magufuli akaamua kuzinyang'anya kodi ya majengo halmashauri kwa vile sasa zilikuwa chini ya Chadema , na kuamuru wenye majengo wote nikiwemo mimi kulipia kodi hiyo kupitia TRA , rekodi zote zipo na wenye nyumba wote wapo na wanatambulika na tayari walishawekwa kwenye mfumo wa malipo ( japo baada ya uchafuzi wa 2020 kodi hii imerejeshwa tena halmashauri maana chadema hawapo tena ), sasa kuwalipisha watu wasiohusika huku wahusika wanaopaswa kulipa kodi wapo na wanafahamika ni wizi wa kishamba sana uliolenga kutunisha mfuko wa serikali kwa NJIA YA HARAMU .

Kama walipaji walishakuwa kwenye mfumo na wanafahamika , huku kila nyumba mpya inayojengwa ujenzi wake hufanywa baada ya vibali vya halmashauri , kwanini Serikali imeamua kupora pesa za raia wasiohusika ?

Itaendelea ....
Kodi zipo sehemu nyingi duniani.

mafano Canada ukinunua kitu cha anasa au kisicho ulazima unalipa kodi ya 13%. Mfano chakula hakina kodi lakini mzulia ya gari yako au mawigi au vipodozi na vyenginevyo unalipia kodi.

Pia mfanya kazi yeyote yule akiajiriwa au akijiajiri mwenyewe ana stahiki kulipa kodi kutokana na kipato chake.

Majengo ya nalipiwa kodi na kodi hizi zinalipwa na owners. ( wapangaji wanapolipa kodi huwa imeshaengezwa kodi ya jengo)
Simu zinalipiwa kodi Na wateja wasimu hulipia simu zao ikiwemo hiyo ya bila kujuwa.
Money transfer pia tunalipia charges ambazo bank au company za simu wa na zijumuisha kwenye service charges wanazo wakata wateja.

Kodi zipo isipokuwa system haip[o sawa
 
Kodi ya Majengo imelipwa ndani ya nchi hii kwa miaka na miaka , kwa kipindi kirefu ililipwa kwenye Halmashauri na kuwa mapato ya Halmashauri husika ili kusaidia miradi mbali mbali , mimi mwenyewe nina nyumba 2 kwenye halmashauri ya Temeke , nafahamu ninachoandika , Jina langu linafahamika vema kabisa na Halmashauri hiyo kama wenye nyumba wengine wanavyofahamika , huku kila jengo au nyumba ikirasimishwa kwa kupewa namba Maalum na kubandikwa Ukutani ili kila mtu aone .

Baada ya uchaguzi Mkuu wa 2015 ccm kuangushwa kwa kunyang'anywa halmashauri kubwa kubwa , ikiwemo Halmashauri ya Jiji la DSM , yenye majengo mengi na yenye kulipiwa pesa nyingi , kwa roho yake Mbaya , Rais wa wakati huo Magufuli akaamua kuzinyang'anya kodi ya majengo halmashauri kwa vile sasa zilikuwa chini ya Chadema , na kuamuru wenye majengo wote nikiwemo mimi kulipia kodi hiyo kupitia TRA , rekodi zote zipo na wenye nyumba wote wapo na wanatambulika na tayari walishawekwa kwenye mfumo wa malipo ( japo baada ya uchafuzi wa 2020 kodi hii imerejeshwa tena halmashauri maana chadema hawapo tena ), sasa kuwalipisha watu wasiohusika huku wahusika wanaopaswa kulipa kodi wapo na wanafahamika ni wizi wa kishamba sana uliolenga kutunisha mfuko wa serikali kwa NJIA YA HARAMU .

Kama walipaji walishakuwa kwenye mfumo na wanafahamika , huku kila nyumba mpya inayojengwa ujenzi wake hufanywa baada ya vibali vya halmashauri , kwanini Serikali imeamua kupora pesa za raia wasiohusika ?

Itaendelea ....
nhi ya kusadikika ccm wamepoteza dira
 
uzalendo ni kulipa kodi,
maendeleo yataletwa na kodi
kodi ndio kipimo cha uzalendo
uzalendo sio kujipendekeza kwa raisi
zile fremu za ccm zilizotapakaa nchi nzima zitalipa kodi ya kutosha
 
Hivi kweli unaandika kwa kutoa povu kabisa kuwa kila nyumba inayojengwa Tanzania serikali inaijua na imeipa kibali cha ujenzi? Eti hii ndiyo msingi wa hoja yako kuwa serikali inawafahamu wenye nyumba wote Tanzania!! Ndiyo tatizo la kushikiwa akili na watu kama Lema na Lissu. Sijui Chadema mnafeli wapi
Sikiliza taifa likiwa na data benk sahihi ya walipa kodi wake ,kodi ya ongezeko la thamani inatosha kabisa matumizi ya serikali kuu.tozo,ushuru,ada,leseni ni tozo za serikali za mitaa na zinakusanywa kutoka kwa mnufaika tu! Hebu fikiria una nyumba mpangaji anakulipa simu ,anakata tozo ya serikali,unaendakutoa fedha unakatwa tena tozo ya serikali,unaenda kulipa umeme unakatwa tozo ya serikali.serikali iangalie vizuri mifumo yake ya Kodi
 
Hili limeshatolewa ufafanuzi, kwamba mwenye nyumba aende na hizo taarifa za mita zote TRA ili akabainishe ni mita ipi itakuwa inatozwa kodi ya jengo! Tuache kubisha tu ili tuonekane tunajua kubisha. Kodi ya nyumba ni halali, tulipe jamani, tumekwepa sana hii kodi!
mwenyenshida ni mwenye nyumba au mpangaji anayenunua umeme????mwenye nyumba kwa kuwa haishi hapo haimlazimishi kupeleka hiyo taarifa na anapeleka mita ya mpangaji yupi ambaye yeye ndio atataka kukatwa???
 
Nadhani hili jambo waliolileta wamekurupuka bila kufanya upembuzi yakinifu ndio maana maswali ni mengi kuliko majibu….
1. kwa nini waliamua kuweka katika mita ya umeme na sio ya maji?
2. kwa nini hawakupembua kuwa nyumba moja inaweza kuwa na mita nyingi hasa zenye wapangaji… na hizo mita zina jina moja la mwenye nyumba
3. Inaitwa kodi ya jengo wakati kuna mita zinawekwa kwenye vibanda au miti mfano wale wafyatua tofali, ana uwanja tu ila kavuta umeme
4. serikali ina viongozi toka mjumbe,mwenyekiti wa kitongoji, wa Kijiji, wa kata,diwani nk ambao wote hawa wanaweza kutambua nyumba ya zamani na inayojengwa hata kama haina kibali na mmiliki wake
5.kuna wanaosema mpangaji alipe tu na atamkata mwenye nyumba wakati wa kulipa kodi, sawa...ni vip pale unapotaka kuhama na unamdai mwenye nyumba,atakulipa kirahisi???
Wenye nyumba sidhani kama wanakataa kulipa kodi, ila mfumo wa ulipaji uwekwe vizuri….!!!!
 
Yaani hata huyo mpiga tofali anakwepa buku yaani Buku unatoa pointi 5. Ninadhani kuna shida zaidi ya hiyo. Nipange nyumba ya laki moja kisha nikatwe buku kwa mwezi. Nimwambie mwenye nyumba anilipe Buku!
 
Hili jambo ni dogo sana kama kodi ya mpangaji ni elfu 20 lipa 19 elfu kwa mwenye nyumba onyesha na ushahidi wa malipo yako
 
Back
Top Bottom