Kwamba makosa ya Sabaya hayapo Polisi yapo TAKUKURU? Wadanganyika

Beatrice Kamugisha

JF-Expert Member
May 18, 2019
762
6,979
Nimeangalia kwa upana makosa au tuhuma zilizoibuliwa na wananchi dhidi ya Sabaya, nyingi ya tuhuma zinaangukia Polisi isipokuwa tuhuma za Mali na fedha ndo zinaangukia TAKUKURU.

Kinachonishangaza nikuona TAKUKURU wamemshikilia huku Polisi ambao walipaswa kuanzisha uchunguzi kuhusu matumizi mabaya ya ofisi, matumizi ya walinzi au mabaunsa kuumiza watu, kutumia silaha kinyume cha taratibu wakiwa wapo kimya.

Hapo ndipo unapojifunza kwamba hakuna dhamira ya uchunguzi bali unaendelea ni udanganyifu dhidi ya wadanganyika. Tujifunze kwenye kesi ya kutekwa MO, tuliambiwa watuhumiwa wamekamatwa ila tumewahi kujua iliishia wapi?

Sabaya alifanya uhalifu Arusha akitumia ID ya TISS lakini alifutiwa kesi akapewa ukuu wa Wilaya, si kwa sababu ni muadilifu Bali kwa sababu tu ni mwanachama wa CCM.

Naaamini hata sasa hivi Sabaya yupo zake kwake ametulia huku tukiaminishwa ameshikiliwa na Kama ameshikiliwa soon ataachiwa au kufikishwa mahakamani kwa makosa yakusogeza muda. Sabaya kiburi alipewa na chama, alisifiwa na chama,hata alipomdharau Pm wakati wa usuluhishi wa mgogoro na RC alipewa maelekezo na hao hao wanaoelekeza achunguzwe leo.

Yawezekana alikwenda Dar akitaka kuingia ikulu akazuiliwa ndo wakaona asiwe kero akamatwe. Niwakumbushe pia kuwa nape alipotengwa na Magu alitumia mbinu hizi hizi za Sabaya kumwona Rais na alisamehewa so usishangae wapo wazee tayari amewatuma kwa Mkuu wa nchi kuomba msamaha life iendeleee.

Tunahitaji mfumo wa upelelezi unaozingatia haki siyo mwongozo wa siasa. Tunahitaji Katiba mpya.
 
Alichofanya sabaya kilikuwa na Baraka zote za chama , unamfungaje mtu uliyempa kazi akaitekeleze na akafanikiwa Kwa usahihi mkubwa ?? Ni maigizo tuu mwisho wa sku huyu hapo
 
Ni kweli kabisa tuhuma zinazomkabili Sabaya ni za jinai zaidi anapaswa kuwa mikononi mwa polisi.
 
Mm naielewa hii michezo, na watz ni wepesi sana wa kupelekeshwa, wanafkiri sababya atahukumiwa kama mtuhumiwa kumbe ni michezo wanacheza ili kuwazuga wasiojielewa
 
Yaani hata kama Sabaya angekuwa mikononi mwa polisi, bado hakuna hatua zozote angechuliwa, maana 90% ya aliyokuwa akiyafanya yalikuwa na baraka za chama kwenye ile dhana ya kunyoosha nchi. Na hizo 10% ndio aliamua kujiongeza. Katika mazingira hayo hakuna hatua yoyote atachukuliwa.
 
Kwa upande wangu hata sielewi hili sakata la Sabaya linaendaje. Kwa kweli katika hali ya kawaida inafikirisha sana na kuna maswali mengi kuliko majibu. Maana nilitegemea Polisi ndio waanze naye kwenye tuhuma za uhalifu wa kutumia silaha akamatwe awekwe kwenye mikono salama cha ajabu tunaambiwa kakamatwa na TAKUKURU tarehe 25/05/2021. Je toka atenguliwe mpaka tarehe 25/05/2021 alikuwa wapi? Au alikuwa huru anazunguuka zunguuka huko mitaani wakati ana tuhuma nzito za uhalifu wa kutumia silaha? Kama alikuwa huru muda wote huo, je ilikuwa sahihi kumuacha mtuhumiwa awe huru kiasi hicho na je mtuhumiwa gani mwingine aliyewahi kutuhumiwa na makosa mazito kama ya Sabaya halafu akapata hiyo nafasi ya kuachwa huru halafu akakamatwa baadae sana. Je, kumuacha mtuhumiwa huru muda wote huo hukupingani na ile dhana kuwa angeweza kuingilia uchunguzi? Je vipi usalama wa mtuhumiwa iwapo wangetokea wananchi wenye hasira kali kumdhuru nani angelaumiwa?

Wanasheria mliopo jamvini mtusaidie kutupa maelezo ya kisheria kwenye sakata hili la Sabaya ambaye ana tuhuma za uhalifu wa kutumia silaha na matumizi mabaya ya ofisi je ni chombo kipi cha serikali kinaanza uchunguzi kati ya TAKUKURU na POLISI au ni chombo chochote kati ya hivyo viwili.
 
Haijalishi iwapo wanatufanyia usanii tu au kweli kuna uchunguzi unaendelea...

Lakini jambo moja la uhakika tunalijua, kwamba, kelele za watu dhidi ya uhalifu wowote ni muhimu na za lazima...

Mwendazake John P. Magufuli ilikuwa hivihivi. Watu walipiga kelele sana dhidi ya uongozi wake mbovu na wenye sura zote za kihalifu lakini alijifanya kuziba masikio na kutokuelewa na kupuuza kila kitu. Alijifanya mungu - mtu..

Mwisho wake ndiyo huo wote, tuliona, adhabu ikawa juu yake...

Hata huyu tuendelee kupiga kelele tu hata kama mamlaka zenye jukumu la kuchukua hatua zitajifanya hamnazo a.k.a kulindana...

Lakini ipo mamlaka kubwa na ya juu zaidi isiyo na upendeleo wala kumuonea mtu, Mungu Muumba. Yeye hukumu zake ni za kweli na za haki kabisa...
 
Kesi ya kumteka Diwani wa Sombetini Mr Msuya -Arusha,ile ni jinai.
Inatakiwa awe Arusha Central Polisi,lock up
 
11 Reactions
Reply
Back
Top Bottom