Kwamba makosa ya Sabaya hayapo Polisi yapo TAKUKURU? Wadanganyika

Tunahitaji mfumo wa upelelezi unaozingatia haki siyo mwongozo wa siasa. Tunahitaji Katiba mpya.
Uko sahihi kabisa ila kwa sasa nashukuru MUNGU tu kuwa ameshaibishwa, yaani hata akiwa huru hatakua na akili za kipuuzi tena
 
Kwani chadema na wana arusha wote wa jf wanasemaje??? Si niliskia wamechinja mbuzi
 
Ukifikiri kwa akili kubwa utagundua kuwa tatizo la Tanzania siyo katiba mpya wala siyo CCM bali ni wananchi wenyewe.Katiba pamoja na CCM ni secondary problem lakini primary problem ni wananchi.
 
Nimeangalia kwa upana makosa au tuhuma zilizoibuliwa na wananchi dhidi ya Sabaya, nyingi ya tuhuma zinaangukia Polisi isipokuwa tuhuma za Mali na fedha ndo zinaangukia TAKUKURU.

Kinachonishangaza nikuona TAKUKURU wamemshikilia huku Polisi ambao walipaswa kuanzisha uchunguzi kuhusu matumizi mabaya ya ofisi, matumizi ya walinzi au mabaunsa kuumiza watu, kutumia silaha kinyume Cha taratibu wakiwa wapo kimya.

Hapo ndipo unapojifunza kwamba hakuna dhamira ya uchunguzi bali unaendelea Ni udanganyifu dhidi ya wadanganyika. Tujifunze kwenye kesi ya kutekwa MO, tuliambiwa watuhumiwa wamekamatwa ila tumewahi kujua iliishia wapi?

Sabaya alifanya uhalifu Arusha akitumia ID ya TISS lakini alifutiwa kesi akapewa ukuu wa Wilaya, si kwa sababu ni muadilifu Bali kwa sababu tu ni mwanachama wa CCM.

Naaamini hata sasa hivi Sabaya yupo zake kwake ametulia huku tukiaminishwa ameshikiliwa na Kama ameshikiliwa soon ataachiwa au kufikishwa mahakamani kwa makosa yakusogeza muda. Sabaya kiburi alipewa na chama, alisifiwa na chama,hata alipomdharau Pm wakati wa usuluhishi wa mgogoro na RC alipewa maelekezo na hao hao wanaoelekeza achunguzwe leo.

Yawezekana alikwenda Dar akitaka kuingia ikulu akazuiliwa ndo wakaona asiwe kero akamatwe. Niwakumbushe pia kuwa nape alipotengwa na Magu alitumia mbinu hizi hizi za Sabaya kumwona Rais na alisamehewa so usishangae wapo wazee tayari amewatuma kwa Mkuu wa nchi kuomba msamaha life iendeleee.

Tunahitaji mfumo wa upelelezi unaozingatia haki siyo mwongozo wa siasa. Tunahitaji Katiba mpya.

BTW kwenye gazeti nimeona timu inayochunguza imeundwa na Takukuru, Usalama na Polisi
 
Back
Top Bottom