Kwamba kuapishwa kwa wabunge 19 viti maalumu CHADEMA, chama hakijashiriki kufanya uteuzi sawasawa na sheria zinavyotaka. Nini maana yake hasa?

Nimemsikiliza John John Mnyika akitoa tamko kuhusu jambo hili leo...

Kwa ufupi linafikirisha sana. Mtu anaweza kujiuliza kama ndivyo hivi yalivyo mambo haya, nini hasa maana yake...?

Kuna assumption mbili hapa;

MOSI; Kuna shida ndani ya CHADEMA. Ni mchakato halali kabisa umefanyika ndani ya chama bila mamlaka za juu za chama kujua. Wamekuja kushtuka, wanaona manyoya tu huku kuku akiwa ameshaliwa...

MBILI; Kama ni kweli chama hakikushiriki kufanya uteuzi huu sawasawa na taratibu za kisheria zinavyotaka na wakati huohuo hawa wanawake wakapata uhalali wa kisheria kuapishwa kuwa wabunge, then tunapaswa kujiuliza swali moja muhimu sana, kuwa, imekuwaje mambo haya yakawezekana na kuwa halali kisheria...?

Kama tuhuma za CHADEMA kupitia kwa katibu mkuu wake John Mnyika dhidi ya "system" ama "dola" ama "serikali" kushiriki kuihujumu CHADEMA kupitia jambo hili, basi we are in big trouble as nation....!

Kama ilivyokuwa kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka huu 2020 kwa "system" ama "dola" kulazimisha CCM ishinde kwa kura za "wizi wa kishindo" kwenye Urais, ubunge na udiwani, basi hakika hakuna kinachoweza kuizuia hii "system" kufanya lolote jingine kuhalalisha inachokitaka kitokee au kifanyike...!!

Ni tahadhari tu kwa CHADEMA, kwamba, Magufuli atatumia nguvu ya fedha kufanikisha yote haya...

CCM ya Magufuli iko very desperate and strategic kutekeleza mission hii hatari kabisa ya kishetani....

Silaha kuu inayotumiwa kuua kila kitu ni RUPIA yaani fedha...

Kila mtu anahitaji fedha, au siyo jamani?

Anachofanya Magufuli na ambayo ndiyo silaha kuu ndilo anayojivunia kutekeleza adhma yake hii ovu ni kutengeneza njaa ya uhitaji ama njaa ya fedha..

Baadaye, anawatupia mamilioni mbele yao wenye uhitaji aliowalenga lakini huku akisema "terms and conditions apply"...

Hyakanani vile, hata kama ni mume na mke mbele ya njaa ya fedha, possibility ya kusalitiana ni 99%...

Huu ndiyo mtihani CHADEMA wanaopaswa kuushinda kwa sababu Tanzania yetu ya sasa chini ya Magufuli ina akisi simulizi ya hadithi ya ANIMAL FARM...

Mnyama mwenye nguvu kama simba, dubu nk ndiye anaye survive ndani ya ANIMAL FARM...!!
Tunachotaka CHADEMA wawafute uachama hao wasaliti haraka sana
 
Baada ya kusikiliza kile kilichoitwa maamuzi ya kikao cha kamati kuu haya ndiyo nimejionea.

1.Wamevuliwa uanachama wa Chadema kwa sababu hawajatokea kuhojiwa na kamati kuu na siyo sababu ya ubunge wa viti maalum.!

2. Wameambiwa wanaweza kuandika barua ya kuomba radhi ili warejeshewe uanachama wao.!

3. Ndani ya siku 30 wanaweza kukata rufaa kwa kupinga hukumu ya kamati kuu kwenye baraza kuu la chadema.!

4. Chadema iliwaandikia barua mara mbili kuwabembeleza wafike kuhojiwa na kamati kuu pia kamati kuu ililazimika kubadili eneo la kuwahoji kutoka makao makuu ya chadema hadi kwenye hoteli ya kitalii ili kulinda usalama wao.!

Mtu ambaye ni msaliti unaweza kumbembeleza kwa kumwandikia barua mbili na hadi kuingia gharama za kukodi hoteli ili kumuhoji?

Ni vipi msaliti aruhusiwe kuandika barua ya kuomba radhi tu na atarudishiwa uanachama wake?

Mbona Zito Kabwe na Kitila Mkumbo wakati wanafukuzwa hawakupewa nafasi ya kuomba radhi na kurudishiwa uanachama wao?

Hapa kuna sinema inachezwa na ndani ya siku 30 tutaona matokeo yake, kama mtu alikuwa tayari kutengeneza igizo la kuangushwa na konyagi na kisha kusingizia wasiojulikana, hapa kuna mengi yanakuja.
 
Back
Top Bottom