Kwamba hautambui mji wa Jerusalem wakati anategemea kuwaomba madawa na net za mbu

britanicca

JF-Expert Member
May 20, 2015
13,971
2,000
Kuna watu wengine wananichanganya, Ukimuuliza Magufuli independently anautambua mji wa Jerusalem kama mji mkuu wa Israel Taifa teule la Mungu, Taifa takatifu kabisa kuwahi kutokea, lakin anaibuka mtu from no where kwamba hautambui mji huo? yeye kama nani?

Tuanze kujiuliza wakati sisi Tunajidai kujitenga na mataifa makubwa ,Kagame yupo anaomba waisrael wahamie kwake,
Netanyahu Kaudhuria kuapishwa kwa Kenyatta sisi tunasubiri kuwaita akina Mseven na Nkurunzinzah ambao hawana impact kwa jambo lolote kwetu,

IPO WAPI SLOGAN YA KUTOFUNGAMANA NA UPANDE WOWOWTE YA MWALIMU?
Tumeshuhudia serikali za hivi karibuni zikichagua upande kabisa ,
Mfano mazoezi ya pamoja ya kijeshi kati ya Tanzania na wasoviet suala ili linamtenga Marekani anayewapa ARVS au mnasubiri kupata zile fake za mwenge?

Kuna nini kati ya Magufuli na Wasoviet?

Tumeshuhudia Tanzania ikikiuka maazimio ya baraza la umoja wa mataifa kwa kujihusisha na KOREA KASKAZINI hasa katika masuala ya kuuziana silaha kali kali, ipo wapi NON ALIGNED MOVEMENT?

Leo hii anaibuka Mahiga na kusema kwaamba Tanzania haitambui jerusalem kama mji mkuu wa Israel??? Tanzania kama nani nchi Omba omba ulimwenguni?
Matamko yetu yawe ya Busara na Kujikita kugawa milion 50 za kila kijiji badala ya kuongelea ambayo hatuna uwezo nayo, na wenda yakatusababishia matatizo,

Kashasema Mkuu na kiranja mkuu wa Dunia alafu mtu ambaye hata si msaidizi wa monitor ukanda wa Afrika mashariki unasema sema nini??

Mahiga ungetumia muda wako kulaani yanayoendelea Libya, Rwanda na Uganda ambapo nchi hizo wananchi wake wako kwenye matatizo makubwa ya uongozi wa kidikteta unaenda kukemea mambo ya mji mkuu???

kweli serikali ya awamu ya Tano yaweza kuwa inaendeshwa na media na Kiki za matamko ili waziri asikike yupo

Britanny
 
britanicca

JF-Expert Member
May 20, 2015
13,971
2,000
siyo busara kujipima kifua na mtu ambaye humuwezi, badala akemee hata yanayoendelea kenya , Raila anajiapisha juma lijalo lakini anaenda kurukia waisrael??
 
Ndama Jeuri

JF-Expert Member
Jul 9, 2015
1,335
2,000
Kuna watu wengine wananichanganya, Ukimuuliza Magufuli independently anautambua mji wa Jerusalem kama mji mkuu wa Israel Taifa teule la Mungu, Taifa takatifu kabisa kuwahi kutokea, lakin anaibuka mtu from no where kwamba hautambui mji huo? yeye kama nani?

Tuanze kujiuliza wakati sisi Tunajidai kujitenga na mataifa makubwa ,Kagame yupo anaomba waisrael wahamie kwake,
Netanyahu Kaudhuria kuapishwa kwa Kenyatta sisi tunasubiri kuwaita akina Mseven na Nkurunzinzah ambao hawana impact kwa jambo lolote kwetu,

IPO WAPI SLOGAN YA KUTOFUNGAMANA NA UPANDE WOWOWTE YA MWALIMU?
Tumeshuhudia serikali za hivi karibuni zikichagua upande kabisa ,
Mfano mazoezi ya pamoja ya kijeshi kati ya Tanzania na wasoviet suala ili linamtenga Marekani anayewapa ARVS au mnasubiri kupata zile fake za mwenge?

Kuna nini kati ya Magufuli na Wasoviet?

Tumeshuhudia Tanzania ikikiuka maazimio ya baraza la umoja wa mataifa kwa kujihusisha na KOREA KASKAZINI hasa katika masuala ya kuuziana silaha kali kali, ipo wapi NON ALIGNED MOVEMENT?

Leo hii anaibuka Mahiga na kusema kwaamba Tanzania haitambui jerusalem kama mji mkuu wa Israel??? Tanzania kama nani nchi Omba omba ulimwenguni?
Matamko yetu yawe ya Busara na Kujikita kugawa milion 50 za kila kijiji badala ya kuongelea ambayo hatuna uwezo nayo, na wenda yakatusababishia matatizo,

Kashasema Mkuu na kiranja mkuu wa Dunia alafu mtu ambaye hata si msaidizi wa monitor ukanda wa Afrika mashariki unasema sema nini??

Mahiga ungetumia muda wako kulaani yanayoendelea Libya, Rwanda na Uganda ambapo nchi hizo wananchi wake wako kwenye matatizo makubwa ya uongozi wa kidikteta unaenda kukemea mambo ya mji mkuu???

kweli serikali ya awamu ya Tano yaweza kuwa inaendeshwa na media na Kiki za matamko ili waziri asikike yupo

Britanny
Kutatusaidia nini ?
 
MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Jul 5, 2012
13,025
2,000
Kwa nini kuna baadhi ya Watanzania hudhani Wayahudi ni watu waliokaribu nao?

Hawa jamaa walimtesa na kumuua Yesu. Kwa maana nyingine ni kizazi cha wauwaji.

Ikumbukwe pia hakuna watu wabaguzi kama wayahudi!

Ambao tumeonja maisha ya Israel tumeonja hali ya kubaguliwa.
 
SK2016

JF-Expert Member
Apr 6, 2017
8,009
2,000
Yaani niliposikia haya maneno ya Mahige na Ndugai nilijichekea mwenyewe tu.

Nilitamani wakae kimya tu.
 
umande

JF-Expert Member
May 11, 2012
314
250
Povu limekutoka utafikiri wewe ni Muisrael vile, Nawe bora ungetumia muda wako kujadili mambo mengine kuliko kutuletea mambo ya mji mkuu hapa. Mtumie na ujumbe raisi wa Korea Kaskazini ambae nae haitambui kabisa nchi inayoitwa Israel
 
likandambwasada

JF-Expert Member
May 27, 2015
5,410
2,000
NI KIHERE HERE TU, TANZANIA ILIYOHESHMIKA NI YA NYERERE TU AMBAPO AKIONGEA UN ASSEMBLY WATU WALIMSIKILIZA KWA UMAKINI, HAWA WA SASA HAWANA JIPYA, WANASUBIRI KUKU KWA MRIJA HALAFU WANATAMAN KUKANA SERA ZAO WAKAT HAIWEZEKANI.
 
Kinambeu

JF-Expert Member
Nov 2, 2014
903
500
Wakristo wengi hawajuwi history ya wayahudi na waliowengi wanadhani wayahudi ni Wakristo na waupenda ukristo.

Wayahudi walipitisha sheria mwaka 1975 kukemea kufanya mihadhara ya kidini yenye lengo la kuwasawishi wayahudi wawe Wakristo ama waislam. Waliweka kifungo cha miaka 5 jela Kwa kosa la kuhubiri dini tofauti na kiyahudi.

Wayahudi huwabagua wote wasiyo wayahudi uwe mkristo Au muislam. Kwahiyo kukaa na kushangilia wayahudi Kama watu watakatifu sana ni kukosa uelewa. Nenda Tel Aviv utajionea mwenywe jinsi wayahudi walivyo wabaguzi Kwa dini zingine.

Kwahiyo kuwapamba wayahudi Kama watu wazuri mno ni kukosa maarifa na kutoruhusu akili yako kufikiri Kwa upana. Hawa ni wayahudi watabaki kuwa wayahudi hadi siku ya kiama na wataendelea kubagua Wakristo na waislam na wengine wote wasiokuwa wayahudi
 
kigogo warioba

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
5,981
2,000
Hivi tanzania itanufaika au inapata maslahi gani isipoitambua jerusalem kuwa mji mkuu.!? Kiongozi hana uhakika au hajui kinachodndelea israel na hii itamfanya aonekane anapwaya katika nafasi yake, sizonje atamtumbua kwa kumsahihisha na atatoa tamko la kuitambua jerusalem kuwa mji mkuu:D:))8)
 
Shepherd

JF-Expert Member
Dec 14, 2012
2,216
2,000
Israel ni nchi iliyoweza kugeuza jangwa kuwa ardi yenye rutuba na kuchuja maji ya bahari nakufanyia nayo kilimo cha umwagiliaji.
 
chuse tbr

JF-Expert Member
Aug 11, 2013
436
1,000
Britannica huwa unaandika vizuri sana ila usipotoshe Rwanda haiwachukui wa Israeli ila inachukuwa wakimbizi waliokataliwa Israel tena kwa malipo kwa kila mkimbizi. Ili kujua kama hawa waisraeli ni wabaguzi wanahamasisha watu kuhamia huko ila Waafrika wanafukuzwa
 
tashwishwi

JF-Expert Member
Sep 25, 2014
2,254
2,000
Kwa nini kuna baadhi ya Watanzania hudhani Wayahudi ni watu waliokaribu nao?

Hawa jamaa walimtesa na kumuua Yesu. Kwa maana nyingine ni kizazi cha wauwaji.

Ikumbukwe pia hakuna watu wabaguzi kama wayahudi!

Ambao tumeonja maisha ya Israel tumeonja hali ya kubaguliwa.
Suala la kumuua Yesu ni maandiko kwa hyo lazima angeuwa tu na juu ya hilo hawana hatia, they are innocent. .

Kuhusu suala la ubaguzi nadhani bora hai wanao bagua hivyo kuliko wale waliowatesa mababu zetu kwenye biashara ya watumwa, waliwatesa na kuhanisi wasizae kabisa...

I hate Arabs more than any race in this universe
 
Odhiambo cairo

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
15,090
2,000
Kwa nini kuna baadhi ya Watanzania hudhani Wayahudi ni watu waliokaribu nao?

Hawa jamaa walimtesa na kumuua Yesu. Kwa maana nyingine ni kizazi cha wauwaji.

Ikumbukwe pia hakuna watu wabaguzi kama wayahudi!

Ambao tumeonja maisha ya Israel tumeonja hali ya kubaguliwa.
Mataifa yote ya weupe ni wabaguzi kwa mtu mweusi. Nenda hata kwa masikini wenzetu India, waarabu wote, wazungu karibu wote, nenda Russia hutatamani kurudiko. Mtu mweusi (mTz) anabaguliwa popote si kwa wayahudi (Israeli) tu. Angalia yanayotokea Libya kwa waafrika wenzetu bara moja , lakini tu kwa sababu wao ni waarabu wanamuuza mtu mweusi!!!
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom