Uchaguzi 2020 Kwamba Benard Membe, Tundu Lissu, Zitto Kabwe na Seif Sharrif Hamad ndio Wanasiasa Wakuu kwenye Ngome ya Upinzani?

BabaDesi

JF-Expert Member
Jun 30, 2007
6,033
3,944
Kwamba Benard Membe, Tundu Lissu, Zitto Kabwe na Seif Sharrif Hamad ndio Wanasiasa Wakuu kwenye Ngome ya Upinzani?

Kwamba wakubaliane tu na kujipanga kwamba Benard Membe agombee Kiti cha Uraisi, Tundu Lisu awe mgombea mwenza ama Vice Versa, Seif Sharrif Hamad agombee Kiti cha Urais Zanzibar na Zitto Kabwe agombee tu Ubunge wake wa Kigoma ili akishinda awe katika mawaziri watakaounda serikali Mpya?

Hivi kweli wanasiasa wetu wa ngome ya upinzani kweli hawajui kuwa umoja ni nguvu na utengano ni Udhaifu?

Hivi Wanasiasa wetu kweli hawatambui kuwa Ubinafsi wao ni udhaifu unaoweza kuishia kwa Jumla ya kura zao mmoja mmoja kuwa nyingi zaidi ya zile za mgombea kutoka Chama Twawala lakini kwa mtindo huu wa kila Mtu kutaka kwenda Kivyake vyake kutaka Uraisi ni Kukaribisha kupigwa bao la nguvu na Mgombea wa Chama Twawala kutokana na kila mmoja kuwa na kura pungufu dhidi ya mgombea wa Chama Tawala?

Hivi miaka yote hiyo toka upinzani ukubaliwe nchini bado haujajifunza tu kwamba Ubinafsi haujengi??

Hivi Upinzani kweli hawaifahamu hesabu rahisi hii??

UPINZANI AMKENI!!
 
  1. Membe na Lissu hawawezi kugombea Rais na makamu kwa sababu kisheria lazima mmoja atoke Tanzania Zanzibar.
  2. Wamesharejesha fomu, sheria hazitambui muungano wa vyama na wako vyama tofauti
  3. Rais ndio habari, kwenye mafahali wawili hamna anaeweza kukubali umakamu
  4. Mada yako umeijibu mwenyewe mwishoni kwa uzito, ubinafsi.
 
ACT Wazalendo Ni idara ya CCM, kila mahali ACT Wazalendo wamewawekea wagombea wa CHADEMA mapingamizi, hamna sehemu hata moja ACT Wazalendo wamewawekea pingamizi CCM.
Kwanza huyo Membe ni kibaraka.
Mwaka 1995 Augustino Lyatonga Mrema shushushu la kijani aliingia NCCR MAGEUZI na kuisaidia CCM kushinda
Mwaka 2015 LOWASSA pandiki lilipandikizwa CHADEMA.
Mwaka huu 2020 Membe shushushu mbobevu, mtiifu kwa Mwenyekiti wa CCM kapandikizwa ACT Wazalendo ili awaghiribu wananchi
 
Tundu Lisu hawezi kuwa mgombea mwenza wa Membe kwa vile wote ni wa Tanzania Bara.
 
Mkuu ushauri wako uko sawa. Lakini shida iko hapa, kila mmoja anatamani kuwa mfalme wa zile nyika.

Hata hivyo 2015 CCM ilipata 58%. Maana yake hata kama kura za upinzani zote angepewa mmoja bado angeangukia 42%, zisingetosha.
 
Ukawa na Lowassa waliungana 2015 wakaambulia kichapo je lissu peke yake atamuweza Magufuli?. Sitashangaa cdm ikipoteza majimbo na kati nyingi sana. Act wazalendo , wao wakipata wabunge hata wawili kwao ni faida.
 
Hahaha yani mnaijadili ACT?! Bora hata mgeijadili NRA.

ACT labda huko Zanzibar, huku Tanganyika sioni wapi wanaqeza kupata hata mwalimu wa madrasa.

Membe hana ushawishi nje ya ccm.
 
Tundu Lisu hawezi kuwa mgombea mwenza wa Membe kwa vile wote ni wa Tanzania Bara.
Muungano huo hauna tija kwa sababu kwa tume hii, piga ua mshindi atakayetangazwa ni jiwe tu, hata kama amechaguliwa na asilimia 10 ya wapiga kura. Mengine ni kama kula upepo.
 
ACT Wazalendo Ni idara ya CCM, kila mahali ACT Wazalendo wamewawekea wagombea wa CHADEMA mapingamizi, hamna sehemu hata moja ACT Wazalendo wamewawekea pingamizi CCM.
Kwanza huyo Membe ni kibaraka.
Mwaka 1995 Augustino Lyatonga Mrema shushushu la kijani aliingia NCCR MAGEUZI na kuisaidia CCM kushinda
Mwaka 2015 LOWASSA pandiki lilipandikizwa CHADEMA.
Mwaka huu 2020 Membe shushushu mbobevu, mtiifu kwa Mwenyekiti wa CCM kapandikizwa ACT Wazalendo ili awaghiribu wananchi
Kamanda mbona Sosopi kamwekea pingamizi mgombea ubunge wa ACT hapa Isimani?
 
  1. Membe na Lissu hawawezi kugombea Rais na makamu kwa sababu kisheria lazima mmoja atoke Tanzania Zanzibar.
  2. Wamesharejesha fomu, sheria hazitambui muungano wa vyama na wako vyama tofauti
  3. Rais ndio habari, kwenye mafahali wawili hamna anaeweza kukubali umakamu
  4. Mada yako umeijibu mwenyewe mwishoni kwa uzito, ubinafsi.
They will all miss he game! All in all, Kaijage hana ubavu wa kumtangaza mshindi.... Lisu hana ubavu wa kulazimisha ushidi wake utangazwe, Nguvu ya umma Tanzania bado sana! tu waoga kama kunguru
 
ACT-Wazalendo walikuwa na uhakika kuwa Lissu hatatoboa atakatwa tu,Membe alitegemewa kuungwa mkono na Chadema.

Lakini ujio wa Lissu na hotuba zake za kusemea hovyo serikali imempa umaarufu wa aina fulani,na kuifanya Chadema kubadiri muelekeo na kwenda bila ACT.

Kilichofuatac ACT-Wazalendo na Chadema wameshindana kuwekeana pingamizi za viti vya udiwani na ubunge.

Sitashangaa kuona CUF wakishirikiana kwa karibu zaidi na Chadema huko Zanzibar kumshikisha adabu Maalim Seif ili asipande zaidi ya umakamu wa kwanza wa Zanzibar kama ACT itaendeleza kumtilia ngumu Chadema Bara.
 
Back
Top Bottom