Kwakuwa uliweza kule basi huna sababu ya kushindwa huku,kazana

Deadbody

JF-Expert Member
May 30, 2015
4,274
6,592
Kwa mujibu wa Biologia, baada ya tendo la kukutana kimwili takribani mbegu milioni 200 hadi 300 hutolewa na mwanaume...halafu zote huanza kupiga mbizi kuogelea kwenye njia safarini kukutana na yai la kike. Ajabu ya kwanza ni kwamba sio zote 200 - 300 ambazo hufanikiwa kulifikia yai( nyingi huchoka na kufia njiani maana si mashindano ya mchezo mchezo). Ajabu ya pili ni kwamba kati ya hizi 300 zinazofanikiwa kufikia yai, ni moja tu..moja tu itakayoshinda nakufanikiwa kupenya na kurutubisha yai, na kwa mantiki hii ILIYOSHINDA NI WEWE HAPO.
Umewahi kuwaza kuhusu hili vizuri?
Yaani ulishindana mbio hizo ukiwa huna macho na ulishinda, ulishindana bila elimu na ukashinda,ulishindani bila hata cheti chochote wala msaada wa yeyote ....na UKASHINDA
Nini kinachokufanya udhani utashindwa sasa?
Tena sasa uko na macho yote, miguu, sasa Unamjua Mungu, sasa ukiwa na plan,ndoto na maono.
Kumbuka ULISHASHINDA toka tumboni huna sababu ya kuwa na hofu yeyote, PAMBANA
 
Ni kweli sote tu washindi lakini pia hatuwezi kuipuuza mikatale ya kijamii isiyo na usawa na inayofanya mapambano hapa duniani yawe magumu mno. Na nijuavyo mimi katika mashindano ni lazima kutakuwepo na washindwa pia. Haitawezekana kila mmoja kuwa mshindi hapa duniani kwa kutumia vigezo vilivyowekwa na jamii (mf. utajiri, madaraka, mvuto, umaarufu...). Kwa jinsi mfumo ulivyosukwa, ni wazi kuwa sote hatuwezi kuwa matajiri, wenye madaraka n.k. Na pengine badala ya kumakinikia vigezo hivi visivyo jumuishi vilivyowekwa na jamii, inabidi kila mmoja awe na vigezo vyake binafsi ambavyo vitamfanya kuwa "mshindi" hata kama siyo milionea. Vigezo hivi binafsi vinaweza kuwa kufanya kazi iridhishayo, kujitolea kusaidia wengine, kuwa na familia yenye upendo, KUMCHA MUNGU, kuwa na furaha, kuwa na afya na mengineyo. Vinginevyo kuna hatari ya watu wengi kuishi maisha ya stress wakidhani kuwa ni washindwa kumbe wangejichunguza vizuri wangegundua kuwa ni washindi wakubwa hapa duniani hata kama hawana utajiri, madaraka, umaarufu, mvuto na vitu vingine vinavyosakwa kwa udi na uvumba.

Kwa hivyo, kimsingi nakubaliana na premise yako ya msingi kuwa sote tuliozaliwa tu washindi. Nina tatizo na ushindi wa hapa duniani hasa huu uliowekewa vigezo na jamii. Ati, kwako mtu aliyeshinda hapa duniani ni yupi? Ni tajiri? Ni mwenye madaraka? Ni mtu maarufu? Ni mwenye mvuto? Ni msomi? Ni yupi? Kwa kutumia vigezo hivi (ambavyo the majority hatuna) ni lazima kila mmoja wetu awe na vigezo vyake mwenyewe ali mradi awe na furaha na ridhiko (japo la juu juu) la maisha yake.

Kauli hizi za jumla (motivational speaker type) ni tamu sana masikioni lakini ukikaa na kuanza kuziangalia kwa makini utagundua kwamba they are only a (superficial) fallacy hasa zikiachwa na vigezo vyake vile vile.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom