Kwakuwa Serikali na Upinzani zimenitenga, Natangaza Maandamano Rasmi ya vijana tuliotengwa02/01/2017

General Mangi

JF-Expert Member
Dec 21, 2013
15,300
23,022
Wana jamvi kwanza poleni kwa masaibu yaliyo ikumba jukwaa letu. Natumai mambo yatakaa sawa

Nimeleta uzi huu kwa wale wote ambao wanahisi kutengwa na serikali hii na hata upinzani kwa kushindwa kukemea yale yanayo endelea hapa nchini.

Ni wazi kwamba serikali yetu ilijipambanua kuwa itatetea masikini ambao ndio wengi nchini lakini imeonekana wazi maneno yale hayana ukweli wowote.
Nasema hivi kwa ushahidi kwamba, masikini wengi ni wale ambao wanakosa huduma za kijamii kama maji, elimu bora, afya, usafiri, umeme, ajira, mikopo n.k.

Kwa makusudi kabisa serikali yetu imekuwa ikiwekeza kwenye mambo ya anasa ambayo hayamgusi mtanzania masikini ambao ni wengi katika nchi yetu.

Tumeshuhudia mandege ya gharama, viwanja vya ndege visivyokuwa na tija, fedha za wahanga wa kagera na mambo mengine kemkem ambayo yameendelea kumtesa masikini mtanzania.

Vijana wengi hatuna ajira, mikopo benk haikamatiki, mazingira ya kujiajiri ni hatari, mikopo kwa wanafunzi imekuwa shida.
Pamoja na kwamba tuna gesi na maji kemkem lakini bado gharama za umeme zipo juu ukilinganisha na nchi ambazo hazina rasilimali kama yetu.

Pamoja na mengi ambayo yamekuwa yakifanywa kwa utashi wa mtu mmoja huku akiyafunika kwa hoja za ufisadi na kutumbua watu, watanzania wengi bado tumelela fofofo.

Hata upinzani wenyewe umekuwa ukijikita katika mambo ambayo yanagusa maslai yao peke yao pasipo angalia mambo ambayo yanahitajika kwa jamii na vijana kwa ujumla.

Sasa natangaza kwamba sisi vijana tuliotengwa na serikali hii tutafanya maandamano na mkusanyiko yasio na kikomo kuanzia tarehe 2 mwezi wa kwanza 2017.(02/01/2017).

Mkusanyiko huu utafanyika kariakoo mpaka pale serikali itakapo tatua matatizo yetu.

Kwasasa tunaandaa mikakati ya kufanikisha hili, hivyo tunaomba kuungwa mkono.

Tutaendelea kutoa update katika uzi huu kadri mipango itakavyo kuwa .

[HASHTAG]#TunatakaAjiraTunatakaMikopoNafuu[/HASHTAG]
Mod tunaomba muheshimu uhuru kama mnavyojipambanua.
Hivyo sitegemei kufutwa kwa uzi huu.
 
Fikiria njia nyingine ya kudai haki yako, Hiyo ya maandamano utatolewa utumbo bure au upate kovu la kudumu! We Shauri yako!!!
 
Na ndo maana imefikia hatua serikali/polisi inataka privacy za wachangiaji kama wewe.

Hii inasikitisha sana uhuru kuminywa kiasi hiki.
 
Back
Top Bottom