kwako yangu ni hifadhi, ya milele si ya muda, | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

kwako yangu ni hifadhi, ya milele si ya muda,

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Magulumangu, May 2, 2011.

 1. Magulumangu

  Magulumangu JF-Expert Member

  #1
  May 2, 2011
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 3,040
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Kwa hadhi na taadhima,kwangu wewe malaika,
  Nilipopatwa hujuma,moyo wangu sisimka,
  Ya kwanza yetu miama,yako sikuwa hulka,
  kwako yangu ni hifadhi, ya milele si ya muda,

  Nilikuwa mkimbizi, yangu mapenzi moyoni,
  Kuvizia kama nzi,kinyesi kwao machoni,
  Cheupe kama la nazi,tui lifikapo mbogani,
  Kwako yangu ni hifadhi, ya milele si ya muda,

  Sikuivunja safari, siku liposema nkome,
  Ilikuwa kama sukari,kwa nyuki ndani kikome,
  Nyingine kanza safari,wako wazazi ni ngome,
  kwako yangu ni hifadhi, ya milele si ya muda,

  Hukuona usumbufu, wao kukupa ulinzi,
  Ndugu wazazi ubunifu, kwako wote walisizi,
  Ukanona yakinifu,si fisadi wa azizi,
  Kwako yangu ni hifadhi, ya milele si ya muda,

  Moyo uliufungua, mkimbizi kimapenzi,
  Limzigo ukanitua, ukasema utalienzi,
  Na sasa ninapumua,sina doa kimapenzi,
  Kwako yangu ni hifadhi, ya milele si ya muda,

  Nilitega tendawili, ndani yangu moyoni,
  Miji mingi si miwili,zawadi hadi manyoni,
  Nakumbuka hadi pili,kisa eti maskini,
  Kwako yangu ni hifadhi, ya milele si ya muda,

  Moyo wangu upo kwako, wewe wake mhifadhi,
  Kihalali jipe jiko,kwako yangu ni hifadhi,
  Twenzetu hata moroko,ya kizanziba mahadhi,
  Kwako yangu ni hifadhi, ya milele si ya muda,

  Sina budi kujisifu, lile lako tabasamu,
  mwendo wako yakinifu,kama twiga muasimu,
  shingo lako malikifu,haleluya kwa karimu,
  Kwako yangu ni hifadhi, ya milele si ya muda,

  Sio kana sina vina, kichwani wewe mrembo,
  usokuwa na kifana,la mgema sio tembo,
  njo kwetu pale banana,ya maisha yetu nembo,
  Kwako yangu ni hifadhi, ya milele si ya muda,
   
 2. Dena Amsi

  Dena Amsi R I P

  #2
  May 3, 2011
  Joined: Aug 17, 2010
  Messages: 13,137
  Likes Received: 254
  Trophy Points: 160
  Wataalaamu wa Mashairi mpo???!!..
   
 3. afrodenzi

  afrodenzi Platinum Member

  #3
  May 3, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 18,135
  Likes Received: 2,398
  Trophy Points: 280
  Yes he is back..
  Kwa poem nakuheshimu. .
   
 4. Magulumangu

  Magulumangu JF-Expert Member

  #4
  May 3, 2011
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 3,040
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Code:
  
  
  DA nimekukosea au? jamani was just my feelings tu kama inakuboa jamani ukimya unakuwa mzuri sana...pole kama yamekuudhi DA sikuwa na nia mbaya na sitegemei uumizwe na feelings zangu....
   
 5. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #5
  May 3, 2011
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,507
  Likes Received: 2,248
  Trophy Points: 280
  kuna wanawake wana bahati sana.hongera yake...
   
 6. Magulumangu

  Magulumangu JF-Expert Member

  #6
  May 3, 2011
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 3,040
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  sio kwamba nimerudi, bali yangu imerudi,
  sikutumwa kama radi, bali ni yake miadi,
  Muulize hata hamadi,sifiki kwake ramadi,
  Asante yako heshima, hata wewe lipotea,

  Jamani nilikumisi,mithili yake amali,
  hata dena amusi,kuponda ya si asili,
  tafuta zote kamusi,kithungu na kiswahili,
  Asante yako heshima,hata wewe lipotea,

  Salamu zangu mahili,mpitishie Osama,
  kule aliko kalili,uanzie na Obama,
  wala hakuna dalili,mpokee wetu Rahima,
  Asante yako heshima,hata wewe lipotea,
   
 7. Magulumangu

  Magulumangu JF-Expert Member

  #7
  May 3, 2011
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 3,040
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135

  strawberry kulamba, avata ya king'asti,
  muumbe wetu rahuba,kama za nuhu nyakati,
  hata wewe kakuumba,kwa ufundi ha mikakati,
  wanawake wenye bahati, wewe ni wao mmoja,

  kioo hakikosei, ukiwa mbele jamani,
  moyo pia hukusei, akwambiapo mwandani,
  msikilize baridei, hata muwapo kigamboni,
  wanawake wenye bahati,hata wewe ni wao mmoja,

  mwandani sipo sifia, njiani wanalopoka,
  wengine hukimbilia,miluzi ya fokafoka,
  kwa nyuma ukijazia,namba nane inaita,
  wanawake wenye bahati,hata wewe ni wao mmoja,

  naomba kura ya ndiyo, nipate wangu uwanja,
  mwambieni hata kihiyo,chakachua siwe tija,
  aliimba hata Kidjo,agolo yake misija,
  wanawake wenye bahati,hata wewe ni wao mmoja,
   
 8. afrodenzi

  afrodenzi Platinum Member

  #8
  May 3, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 18,135
  Likes Received: 2,398
  Trophy Points: 280
  mmmmmhhh
  kweli kofia nakuvulia ,
  kwa mashairi umebarikiwa
  heshima busara yako pia..
  Kwa Mungu nakuombea ..
  Azidi kukuongezea...
   
 9. Magulumangu

  Magulumangu JF-Expert Member

  #9
  May 3, 2011
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 3,040
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135

  nambie mtu wangu,
  namtafuta hapa judith
  ila nasikia anatangaza ndoa,
  sasa sijui itakuwaje,
  au mambo ya Beijing hayo?
   
 10. Sooth

  Sooth JF-Expert Member

  #10
  May 3, 2011
  Joined: Apr 27, 2009
  Messages: 3,773
  Likes Received: 4,494
  Trophy Points: 280
  Huyajui ya mbele, usiape ya milele,
  Wa kike kama upele, utajikuna upige kelele,
  Uwele si mchele, shida na tabu ni kilele,
  Ya mbele ni kiza, katu huwezi jua

  Kuna tofauti malezi, familia imempatia,
  Kuna kama walevi, bila sababu hulia,
  Pia kuna wezi, mfukoni kucha hupitia,
  Ya mbele ni kiza, katu huwezi jua

  Wengine wana dharau, tena si wakarimu,
  Naomba msinihukumu, tatizo ni baadhi yenu,
  Kwa dhati nawaheshimu, nyie viumbe adhimu
  Ya mbele ni kiza, katu huwezi jua

  Magulumangu unaweza, vina vimekamilika,
  Kwenye mizani umecheza, kama messi unaweza,
  Mji nakupa Muheza, kwenye mnazi nakukweza,
  Ya mbele ni kiza, katu huwezi jua
   
 11. afrodenzi

  afrodenzi Platinum Member

  #11
  May 3, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 18,135
  Likes Received: 2,398
  Trophy Points: 280
  hahahah JUdith yupo
  Nilimuona jana maeneo
  ya kwenye siasa kule
  Soshi ndo anakuja na kuondoka
  hakai sana humu ndani siku hizi
  we mzima kabisa lakini??
   
 12. Dena Amsi

  Dena Amsi R I P

  #12
  May 3, 2011
  Joined: Aug 17, 2010
  Messages: 13,137
  Likes Received: 254
  Trophy Points: 160
  Pole bana usingizi ulikuwa unasumbua.......pole
   
 13. Magulumangu

  Magulumangu JF-Expert Member

  #13
  May 3, 2011
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 3,040
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Mti ulioutua,nadhani upo urimbo,
  Fanya uje tutumua,asijekuwa mrembo,
  wa kike hatosumbua,iwapo huna uringo,
  Niliyaona ya mbele,kioo yeye mrembo,

  Tofauti ni malezi,hilo nakupa hakika,
  Hata kunguru wa mbezi,hafai ye kufugika,
  Wale ulotaja wezi,ukahaba huupika,
  Niliyaona ya mbele,kioo yeye mrembo,

  Wewe unawaheshimu,hilo mkono nanyosha,
  Wao viumbe adhimu,ndo mama yetu maisha,
  kamwe huna hukumu,mfano lulu na isha,
  Niliyaona ya mbele,kioo yeye mrembo,

  Mesi namfagilia,drogba naye ayaweza,
  Ngondya mwana aslia,nilishapita muheza,
  minazi napalilia,muulize hata mbiza,
  Niliyaona ya mbele,kioo yeye mrembo,
   
 14. Magulumangu

  Magulumangu JF-Expert Member

  #14
  May 3, 2011
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 3,040
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Du kumbe usinginzi unazaa hasira basi mie siupendi hahahaha
   
 15. Magulumangu

  Magulumangu JF-Expert Member

  #15
  May 3, 2011
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 3,040
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135

  Nilipitia mitaa ya SIASA duh kina Nnauye wakanitoa eti mi Magamba,
  Soshi yeye sijui inakuwaje anakuja na kupotea,
  anyway hata mie nipo nipo tu si unajua tena umalenga si lele mama..
  Nilikuwa pale DC jana kuonyesha kuwaunga mkono Marekani kwa kumnasa Osama nikitokea Itale pale kumu beatificate Pope II nikiwa na Robert mwana wa Mugabe....
   
 16. birungi

  birungi JF-Expert Member

  #16
  May 3, 2011
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 388
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  wapi babu?? aje aweke shairi la bibi
  magulumangu big up sana

  hii ni zawadi yako
  kwa hiyo tungo yako
  mungu ajibu hitaji lako
  azidishe maradufu furaha yako.
   
 17. Magulumangu

  Magulumangu JF-Expert Member

  #17
  May 3, 2011
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 3,040
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Babu bado yu na bibi,wafurahia maisha,
  wameenzi kama zinabi,mapenzi yao toisha,
  babu asiye kitambi,mazoezi kwake toisha,
  Asante mwana birungi,karibu umalengani,

  mungu baba hujibu,kila mwenye kuhitaji,
  mwenye dhambi pata jibu,bila hata nidi taji,
  weusi hata warabu,kwake yeye si miraji,
  Asante mwana birungi,karibu umalengani,
   
Loading...