Kwako Waziri wa Uchukuzi Baada ya SUMATRA kutojibu Maswali yangu

Faana

JF-Expert Member
Dec 12, 2011
31,281
32,325
Moja kwa moja kwenye Mada, Ningependa kukuomba Waziri wa Uchukuzi uwasaidie wananchi wanaoishi Dumila na Turiani kutokana na uzi wangu mmoja ambao nilidhani SUMATRA watakuwa waliufanyia kazi lakini kumbe yawezekana hawakuuona, au waliuona wakaufumbia macho kwa sababu zao.

Mwishoni mwa wiki jana nilisafiri tena kutoka Dumila eneo liitwalo Ferry kwenda Turiani mkoani Morogoro, nilijifunza kuwa wananchi wale wanaibiwa vibaya kwenye viwango vya nauli wanavyotozwa na wasafirishaji.

Umbali kutoka Dumila mpaka Turiani ni kilometer 48, nauli yake ni shilingi 4000, kutoka Dumila au kutoka Turiani mpaka Hembeti ambapo ni kama halfway ya umbali wa kilometre kama 23 au 24, nauli yake ni shilingi 3000, na kutoka Dumila mpaka Mvomero ambapo ni umbali wa kama kilometer 15 kama sijakosea sana, nauli ni shilingi 2000 mpaka 2500.

Nikirejea bei za SUMATRA, natolea mfano wa nauli ya kutoka Dsm hadi Kibaha ambapo umbali wake ni kilometer kama 39 na nauli yake ni shilingi 1000.

Kutoka Morogoro Msanvu mpaka Dumila ni kilometer kama 69 na nauli yake ni shilingi 3000, swali linakuja, je ni kwanini wanacnhi wanaosafiri kutoka Dumila kwenda Turiani na vijiji vilivyopo hapo katikati wanatozwa nauli zisizowiana na umbali halisi? Umbali wa Morogoro hadi Dumila ni mrefu zaidi kuliko Dumila mpaka Turiani, na barabara zote ni lami, tatizo lipo wapi? SUMATRA Mkoa wa Morogoro wapo, Viongozi wa serikali nao wapo, je kuna siri gani imefichika hapo? Je hili nalo ni mpaka lisimamiwe na Mhe. Rais Magufuli?

Mhe. Waziri wa uchukuzi, wewe unapita njia hiyo mara kwa mara, unaweza kusimama pale Ferry ukauliza viwango vya nauli wanavyotozwa wananchi wale ukapata majibu moja kwa moja. binafsi bado sijapata majibu kwanini hali ipo kama hivyo ilivyo wakati vyombo husika vipo.

Pia unaweza kusoma hii:


Nawasilisha
 
Watendaji wa awamu hii wanaogopa hata kujibu maswali hadi maelekezo wapate kutoka jumba jeupe


Huwa wanamsingizia "kutoka juu" ili tusiendelee kuwahoji, kumbe Rais naye hajawaambia wanayosingizia
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom