Kwako Waziri wa Maji, Miradi ya maji ambayo haikujengwa na Ruwasa inachezewa

ndege JOHN

JF-Expert Member
Aug 31, 2016
10,954
2,000
Mheshimiwa juma awesso waziri wa maji nakuomba fuatilia miradi ya maji iliyojengwa awamu za nyuma na kukabithiwa bodi za Kijiji inachezewa Sana na Hawa viongozi.

Miradi ambayo Ni mizuri Ni hii iliyojengwa kuanzia 2019 ila ile ya zamani hali Ni mbaya hasa ile ambayo mashine za kuvuta maji zinatumia Diesel viongozi wanaiba mafuta hawajazi tank inavyotakiwa halafu na ma tank yalijengwa chini ya kiwango yameanza kupasuka na kutengeneza nyufa.

Wananchi hawapati maji ni basi tu kwa kuwa sasa hivi ni masika maji sio tatizo sana ila ikifika kiangazi mifugo itahitaji maji hiki ni kipindi Cha kufanyia kazi hio miradi inayosua sua.

kibaya account za miradi hazina pesa miradi haina faida kabisa jumuiya za watumia maji zimeliwa Sana pesa ukitaka ushahidi wa hili ninalokwambia naomba uni PM hata kwa ID nyingine fake nikupe mfano wa mradi fulani ambao najua udhaifu wake mwanzo mwisho maana nimeshakuandikia barua bila kutaja address yangu kuja hapo wizarani lakini nahisi haijakufikia.

Lakini changamoto nyingine Ni baadhi ya wanakijiji sio wastaraabu wanakata mabomba makusudi hasa Yale ambayo yapo juu kwenye makorongo.

Hii inachangia maji kupotea na kuwapa mateso mafundi wakamatwe wapelekwe mahakamani kabisa maana wanajiamini kwa kuwa kesi zao zinaishia kwenye ofisi za Kijiji wanatoka.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom