Kwako Waziri wa Afya: Matatizo matatu ya Hospitali ya Muhimbili na Mloganzila ni haya

Zygot

JF-Expert Member
Apr 14, 2016
2,238
2,866
Mheshimiwa Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu, hizi ni Hospitali pacha zenye uzoefu wa uzembe zina matatizo haya matatu;
  1. Madaktari Wazoefu kuhangaikia Hospitali za Mitaani kuliko mwajili wao
  2. Kuwatumia Wanafunzi kujifunza bila Daktari mzoefu mbele ya mgonjwa
  3. Madawa ’feki’ kwa wingi ndani ya Hospitali
Madaktari wako hospitali za Umma kama Kituo cha kutafuta Wateja na kuwaelekeza kwenye vituo vyao vya mitaani ikiwa ni pamoja na Hospitali za binafsi. Kuna sababu gani ya kuendelea kuruhusu Daktari kuhudumu Hospitali za mitaani? Je, Askari Polisi au Askari Jeshi anaweza pia kuhudumu Kampuni Binafsi za Ulinzi?

Nasikia NHIF wanawalipa kutokana na malipo ya Mgonjwa hii ni hatari! Inawafanya kujiingiza kwenye tiba kubwa hata wasizoziweza ili tu wapate pesa

Wanafunzi wamefikia hatua ya kufanya mitihani mbele ya Mgonjwa ambaye hajapewa huduma lakini anatumiwa kama Kituo cha mtihani. Bila hata kuomba samahani, ukiwa hospitali Daktari anajiona kama anakumiliki, ni specimen yake.

Kuna madawa ’feki’ mengi yako kwenye maduka ya hospitali hizi. Yaonekana ni kwa sababu kuna Wagonjwa wengi na waletaji wana dili zao na wahusika.

Mara nyingi utapewa dawa inayoaminika kufanya vizuri katika ugonjwa lakini ukitaka usalama bora ununue ya maduka ya mitaani

Utawala wa hospitali ujiangalie upya! Hili siyo kutafuta sifa.
 
Hospitalini ni sehemu ambazo madaktari baadhi yao hufanya makosa makubwa kwenye miili ya binadamu,ila baadhi ya wananchi hawaelewagi tu nakupelekea hata vifo.
 
Nafikiri ni wakati muafaka kwa watumishi wa umma kwa sasa hasa madaktari kuwa na mwajiri mmoja hawe mwajiliwa wa umma au aende private sector.Hataki aingie mtaani aone watu wanavyosugua viatu..
Ishu ya dawa feki TFDA ndio inapaswa kulaumiwa..maana bongo kila kitu ni feki hadi nywele
 
Hili taifa sijui tunapelekwa wapi, badala ya watawala kuguswa, kuomba radhi na kujirekebisha kwa wananchi wao.

Wao wanakuja na maandiko ya kujitetea ambayo ukiyachunguza kwa umakini pia utakuta yamejaa dharau na matusi kwa wananchi. Inahuzunisha sana na kukatisha tamaa.

Soon tutamsikia ummi mwalimu akija na kelele zake kama muimba taarabu naye akileta siasa kwenye uhai wa watu simply ma PHD holders hawawezi kuongea na mtu ambaye hajaenda shule, very shameful. Mungu tu atusaidie kuona wapi tunapojikwaa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nasikia NHIF wanawalipa kutokana na malipo ya mgonjwa hii ni hatari!! Inawafanya kujiingiza kwenye tiba kubwa hata wasizoziweza ili tu wapate pesa.
Hili nina uhakika nalo ,kwa asilimia 100 ,Kwa tukia moja BENJAMIN MKAPA ,HOSPITALI! GOD HAVE MERCY ON US!
 
Mlundikano wa wagonjwa kuliko idadi ya staff sio shida tena?,gharama za matibabu kuwa kubwa sio shida tena?Kuna research ilifanyika, watanzania wenye uwezo wa ku afford medical services ni less than 20% ,ndio maana ukitangaza matibabu bure e.g. meli ya kichina ile walijaa watu hadi wachina wakakimbia

Hapa issue ni sera ya afya ni mbovu...watanzania wanaoumwa mtaani ni wengi kushinda walioko hospitali

Kwa kifupi tu hili bomu wizara wanalijua ukilitegua hapatakalika ,nani asiejua madaktari na medical staff wa Tanzania wanalipwa kidogo kushinda nchi zote za Africa?


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tujadili hospitali zetu badala ya barua ya mtu anayeitwa profesa na mkurugenzi.

Tabia za madaktari wetu ni hovyo na hasa kwa mtu ambaye umeshuhudia madaktari wa nchi zilizoendelea. Madaktari wetu bado wana tabia ya sekondari kuamini kwamba kazi yao ni bora kuliko za wengine dunia hii. Wanadeka na kila wakati wanataka kukuonesha kwamba wewe ni mbumbumbu.

Tabia ya kazi zao nje ya mwajili wao ni hatari kwa ubora wa afya za watu. Kuna baadhi wanajiita maprofesa lakini unawakuta saa za kazi wako mitaani upanga kwenye vyumba swa na kioski, wakikusanya elfu kumi kumi! Siyo sababu ya maisha magumu ila ni kutojitambua na tamaa iliyowajaa!

Madawa feki ni kweli kabisaaa! Yamejaa sana hospitali za serikali. Maduka ya mitaani pia yapo lakini hospitali ni zaidi! Nadhani ni kwa kuamini huko wateja ni wengi.
 
Hakuna huo ujinga awamu ya tano, watu wamenyooka sasa nidhamu imerudi kwenye maofisi na watu wanachapa kazi balaa..
Nyie mtakuwa CDM..

Wanaotoa Taarifa kama hizi wanao Ushahidi na mimi pia nimewahi kushuhudia baadhi ya kasoro zilizo wekwa wazi hapa ,mambo ya Chama weka pembeni ili tuondoe Tatizo.Habari ya kusifia sifia tu kwenye Maisha ya Watu achana nayo.
 
We undhani wanapenda kufanya kazi umma na private..mishahara ya umma haitoshelezi mahitaji..na wenyewe wanapambana na maisha yao.
Nafikiri ni wakati muafaka kwa watumishi wa umma kwa sasa hasa madaktari kuwa na mwajiri mmoja hawe mwajiliwa wa umma au aende private sector.Hataki aingie mtaani aone watu wanavyosugua viatu..
Ishu ya dawa feki TFDA ndio inapaswa kulaumiwa..maana bongo kila kitu ni feki hadi nywele

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tujiridhishe na dawa tunazopewa hospitalini kabla ya kuzitumia kama ndizo zenyewe, kuna malalamiko ya watu kupewa dawa ambazo sio za ugonjwa husika. Lakini swali ni je utajaridhishaje kwamba dawa ulizopewa ndizo zenyewe na wewe sio daktari?.
Hapa wafamasia nao wanahusika kwa kutoa dawa ambazo sio, jamani kama dawa hiyo hakuna basi tuambieni haipo sio kutoa dawa ilimradi nisiondoke bila dawa, hii itakuwa kuhatarisha maisha ya mtu au kuua kwa makusudi!
 
mwekundu,
Nimeangali thrd inataja matatizo matatu. Unapojaribu kusema kuna murundikanao wa wagonjwa kuliko idadi ya madaktari unaonesha madaktari wanazidiwa, sawa! Lakini je, wanatoa wapi tena muda wa kwenda hospitali za private na vioski vyao mitaani? Ukweli ni kwamba hawatoi muda wao kwa mwajili. Muda mwingi hawako hospitali, wakirudi wanaripua tu!

Uwezo wa ku-afford medical services hiyo inaeleweka kwa umaskini wetu lakini hiyo ndo ituletee dawa feki? Sera ni mbaya lakini pia watu wa tiba wana tabia mbaya! Huwezi tumia wanafunzi kujifunzia kwa mgonjwa anayejifahamu, bila hata kumuomba radhi. Eti mwanafunzi unakuja kumfanyisha mtihani mbele ya mgonjwa ambaye hajapata tiba!
 
Hili tangazo la lishe ya watoto wa umri kuanzia miezi miwili na bei yake shilingi mia mbili hivi waziri Dr. Umi Mwalimu analusikia?

Mbona anaruhusu watoto wachanga kulushwa vitu badala ya nyonyo la mama?

Na je atakuwa na uhakika gani kuwa wachakachuaji hawawezi haribu afya za watoto?

Naomba mniulizie kwa Dr. Umi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom