Kwako Waziri Ummy Mwalimu kuhusu maambukizi ya COVID-19: Watanzania tunahitaji kupewa taarifa za kila siku (Daily Updates)

Huyu mama msimlaumu ana wakati mgumu kwa sasa na ana mambo mengi yamemzidi,lawama ziende huyu jamaa aliyekimbia dar

♡♤Life belongs to all who struggle for it♤♡♧
 
Siku moja Waziri wa Maliasili alienda kwa Bwana Nyuki, kufika akataka aingie aone mizinga ya nyuki bila kibali, akalazimisha kuingia akijinadi kuwa yeye ni Waziri kwani hajui hadi amwambie awe na kibali?

Dah kuingia kule ndani nyuki wakaanza kumuuma, akaomba msaada kwa Bwana Nyuki, akamjibu akamwambia Waambie wewe ni Waziri, kwani hawakujui?


Sent using Jamii Forums mobile app
 
M-mbabe,
Asante mkuu naunga mkono hoja. Bila hizi taaarifa kwa kweli watu wengi wanapotoshwa na taarifa feki za kwenye social media ambazo sio official. Wizara ilitazame hili jamani
 
Huyo mama keshafeli kitambo swala la kutoa taarifa kila siku bora waachiwe wakuu wa mikoa kila mkuu wa mkoaatangaze kwenye eneo lake.
 
Kichwa cha uzi kimejitosheleza.

Watanzania tunahitaji kujua kinachoendelea kuhusu hili janga. Source ya taarifa za jambo kama hili yapaswa zitolewe na mamlaka husika, ambayo ni wizara inayoshughulikia masuala ya afya (hapa Tanzania wizara hii ina jina refu sana).

Upande wa pili wa muungano (Zanzibar) walau wao wanajitahidi kiasi chake. Huku Tanganyika bado sana.

Taarifa hizi ziwe zinatolewa na waziri mwenye dhamana kila siku kupitia tv stations zote kabla ya taarifa ya habari ya saa 2 usiku.

Taarifa hizi ziwe na data muhimu zifuatazo (at the minimum):

1. Tarehe ya vipimo
2. Idadi ya waliofanyiwa vipimo siku hiyo
3. Idadi ya maambukizi siku hiyo
4. Idadi ya vifo siku hiyo
5.B/down ya maambukizi kimkoa siku hiyo
6. Idadi cumulative kwa vipimo vyote
7. Idadi cumulative kwa maambukizi
8. Idadi cumulative kwa vifo
9. Idadi cumulative kwa waliopona

Hapo juu kwenye namba 2 hadi 5.... hata kama idadi yake ni "zero", itamkwe hivyo. Muhimu ni taarifa iwe public.

Ni katika kuboresha uwazi (transparency).
it's over 3 days tangu update ya mwisho kutolewa.
sasa naona inaelekea saa 10 hakuna updates zozote leo still.... Ummy, are you serious?
 
Hahahaa hahaha hapa mkuu umeniacha kabisa
Siku moja Waziri wa Maliasili alienda kwa Bwana Nyuki, kufika akataka aingie aone mizinga ya nyuki bila kibali, akalazimisha kuingia akijinadi kuwa yeye ni Waziri kwani hajui hadi amwambie awe na kibali?

Dah kuingia kule ndani nyuki wakaanza kumuuma, akaomba msaada kwa Bwana Nyuki, akamjibu akamwambia Waambie wewe ni Waziri, kwani hawakujui?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bwana Chikwuemeka jana ndugu zenu lukuki wamekuja kuwasalimia huko mliko,
Kuzid hata idadi ya December !!!
Umewaona?
Unajambo gani kilingeni baada ya hili
Utasemaje raia ambaye huna hata passport mkuu,unabaki kujilinda tu na watu wako wa karibu kuhakikisha wako salama na kufuata maelekezo ya WHO
 
Hii kitu ilitakiwa iwe hivyo tangia siku ya kwanza ugonjwa huu ulipoingia nchini. Tutakumbushana kumbushana na kuwaelekeza hawa mpaka lini as if hawa viongozi ni laymen?
Walichaguliwa hizo nafasi na wafanye kazi professionally kama inavyotakiwa na sio kwa mazoea.
Wanakera wao mpaka aliyewachagua..
 
Back
Top Bottom