Kwako Waziri Ndalichako chuo cha TEKU kinaibia ada wanafunzi kwa nguvu

Abby Newton

JF-Expert Member
Nov 12, 2017
1,227
2,197
Sote tunakumbuka miaka takribani 2 iliyopita serikali ilivifungia baadhi ya vyuo binafsi kwa sababu ya kuwa na miundombinu duni iliyopelekea kutoa elimu duni.

Mojawapo ya vyuo vilivyofungiwa ni chuo cha TEKU Mbeya.Lakini baada ya kufanya marekebisho kadhaa serikali iliviruhusu tena vyuo hivi kuendelea na masomo TEKU ikiwemo.

Hawa TEKU bado wanaendelea kufanya mchezo na elimu ya watoto wetu.Mimi nina mdogo wangu anasoma pale. Dogo alikuwa hataki kabisa kusoma hapo ila baada ya kukosa vyuo vya serikali kukawa hakuna jinsi ikabidi aombe TEKU na akachaguliwa. Mapema alivyoenda kuchukua fomu ya malipo na ada ilikuwa kama Mil.1,450,000/= Ukichanganya na michango mingine jumla ilikua karibu Mil1,700,000= kwa mwaka wa kwanza.

Ajabu baada ya kufungua juzi kutoka likizo ya Corona ada imeongezeka kwa laki 4 zaidi na sasa ada imefika Mil.2,135,000/= Hatujui baada ya kufungua msimu ujao hali itakuaje maana wanajibadirishia kadri wanavyojisikia.

Serikali ilisema itaweka muongozo wa ada katika vyuo binafsi ili kuzuia upandishwaji holela wa ada. Je mpango huo umeishia wapi. Wanachokifanya TEKU ni wizi,utapeli na uonevu kwa watoto wetu wanaotoka familia za waanyonge.

Tafadhali Mh.Waziri naomba ufuatilie kwa karibu chuo hiki, kwani hata elimu inayotolewa pale ni ya mashaka mashaka. Mtu anaechezea Elimu ni zaidi ya muuaji.
IMG-20200613-WA0000.jpg
 
Hicho chuo ni cha kanisa la Moravian, peleka malalamiko kwa askofu
 
Hicho chuo ni cha kanisa la Moravian, peleka malalamiko kwa askofu
Sawa mkuu lakini vyuo vyote viko chini ya uangalizi na usimamizi wa serikali. Vp km huo Askofu ndiye alipitisha hiyo michango atanisikiliza kweli?
 
Sawa mkuu lakini vyuo vyote viko chini ya uangalizi na usimamizi wa serikali. Vp km huo Askofu ndiye alipitisha hiyo michango atanisikiliza kweli?
Hajaipitisha, ni mbinu za genge la wahuni wachache. Askofu hajui wizi huu
 
Kwanini unapoteza hela wakati atamaliza hana ujuzi wowote
Sikujua km kaomba hicho chuo. Mwishoni kabisa wakati amekosa vyuo vingine akaniambia jina limetoka TEKU.Nilimwambia asiende. Baadae na bodi ya mkopo wakatoa allocation ya majina ya mkopo na jina lake linaonekana TEKU akiwa na asilimia km 70% hivi. Maamuzi yangu ilikua aombe upya mwaka huu ila watu wakasema itakua ngumu kupata tena mkopo.ndo ivo mkuu.
 
Back
Top Bottom