Kwako waziri mkuu,mheshimiwa Kassim Majaliwa

mwananyaso

JF-Expert Member
Feb 19, 2017
2,843
3,128
Kwanza napenda kuipongeza serikali kwa kazi nzuri inayofanya kuhuisha uchumi wa nchi na kuwakomboa wananchi hususani wa maisha ya chini,kikubwa cha kupongeza, ni namna mlivyoondoa kodi mbalimbali za mazao na ushuru mwingi uliokandamiza kipato cha wananchi maskini,mambo ni mengi mazuri yamefanyika ,yako wazi ,siwezi yataja hapa yote,

Lengo la waraka huu mheshimiwa waziri mkuu ni kukueleza mambo yanayoendelea nyuma ya pazia kuhusu serikali hii ya awamu ya tano,naweza sema ni hujuma dhidi ya serikali ,hujuma hii inafanywa na Watumishi baadhi, si wote wa kada ya chini kabisa ,watumishi wanaokutana face to face na wakulima ,wafanyabiashara ndogondogo,na wajasiliamali ambao wanakua .
Serikali ikitoa tamko ,mfano wewe,au rais,kwamba wananchi wasisumbuliwe kufanya shughuli zao ,uwekwe utaratibu mzuri wa kuwashughulikia, bado usumbufu huo upo na wanaupata sana kupitia kada ya chini kabisa katika utumishi wa umma.

Wananchi biashara zao zinafungiwa hovyo,hakuna weledi katika kushughulikia sera ya uwezeshaji wananchi,hii inapelekea malalamiko kua mengi toka kwa wananchi yakua mnatoa matamko kama serikali lakini mnawaacha watumishi hao kuwasurubu wananchi,hizi ni kauri za baadhi ya wananchi.

Na wananchi wakiiuliza watumishi hao kulikoni ,wanaambiwa serikali yenu hiyo mliichagua wenyewe,hii inapelekea wananchi kukosa imani ya serikali yao.

Naamini serikali ina mipango mizuri ispokua kuna baadhi ya watumishi ndani ya serikali wanaihujumu serikali.

Mheshimiwa waziri mkuu,pamoja na matamko makali dhidi ya watumishi wanaosumbua wanannchi bado matamko hayo yanapuuzwa,yanabaki majukwaani.

Ni wajibu sasa wa serikali kwenda chini kabisa kuhakikisha usumbufu kwa wananchi unaondoka mara moja na usibaki kama matamko yasio na nguvu yoyote,usumbufu huu unaathari kubwa kwa serikali na chama kama bado kinahitaji ridhaa ya kuongoza ,kwani hao ndio wapiga kura.

Naomba adhabu kali waanze kupewa watumishi ambao wanakiuka matamshi ya viongozi wakuu wa serikali.ikiwemo demotion na hata kuwafukuza kazi

Uwepo mpango madhubuti wa kufuatilia mienendo ya watumishi kada ya chini,kwani hao ndo kila siku wanakutana na wananchi.

Yawekwe masanduku ya kutolea maoni dhidi ya watumishi kada ya chini kwenye serikali za mitaa,na wa kufungua masanduku hayo wawe ni kamati ya ulinzi na usalama ,iwepo siku maalumu ya viongozi hao kujua nini wananchi hakiwapendezi ,na kipi wangepndelea sehemu husika .hii itasaidia kuwabaini na kuwaonya mapema ,kwa madhara yake ni makubwa.
 
Back
Top Bottom