Kwako Rais na mama yetu Samia Suluhu, usiwasahau vijana wa mafuta na gesi waliosomeshwa kwa fedha nyingi kupitia Wizara ya nishati

Meneja Wa Makampuni

JF-Expert Member
Jul 7, 2020
6,312
8,213
Kwako Rais wetu na mama yetu,
Hongera kwa kuendelea na majukumu yako ya kila siku ili kulisongesha taifa letu mbele.

Mama yetu kuna hawa vijana waliosomea mafuta na gesi, waliosomeshwa katika chuo kikuu cha Dar es Salaam kupitia wizara ya nishati kwa fedha za serikali ili wasaidie taifa letu kuinua uchumi wa mafuta na gesi.
Tunakuomba uwakumbuke kwenye ajira mama yetu.

Shahada za mafuta na gesi zilianzishwa mwaka 2013 kupitia wizara ya nishati katika chuo kikuu cha Dar es Salaam.

Hivyo chuo kikuu cha Dar es Salaam kupitia wizara ya nishati kilianzisha shahada ya jiolojia ya Petroli (BSc. Petroleum Geology), shahada ya Kemia ya Petroli (BSc Petroleum Chemistry) na Shahada ya Uhandisi wa Petroli (BSc. Petroleum Engineering). Lakini mpaka sasa vijana wote waliohitimu wapo majumbani hawana kazi za kufanya wala pakujishikiza. Vijana walishakata tamaa kwasababu tegemeo lao kubwa lilikua wizara ya nishati.

Hivyo mama tunakuomba wakumbuke vijana hawa kwasababu hawaoni uelekeo huko wanakokwenda tofauti na zamani ambapo walikua wakipata mawasiliano ya karibu kutoka wizara ya nishati.

Kuna kipindi Wizara ya nishati iliunda Oil and Gesi Professional Data Base ambapo walikua wakiwasajili kila wanaohitimu shahada za mafuta na gesi Tanzania lakini haieleweki hiyo data base iliishia wapi.

Rejea hii barua ya mwaka 2016, lakini cha ajabu vijana wetu bado wanasugua benchi mtaani hawaoni mbele, mbele Luna giza.

IMG_20210505_225314.jpg

IMG_20210505_225301.jpg

Na pia hiyo data base haikufanya chochote ili kuhakikisha wahitimu wa shahada za mafuta na gesi wanaendelezwa bila kuachwa mitaani huku wakiwa na A na GPA kubwa.

Hivyo mpaka mwaka huu 2021 wahitimu wa shahada za mafuta na gesi (Petroli) wapo wapo tu mtaani hawaelewi wanakoelekea.

Ahsante,
Nikutakie majukumu mema.
 
Kwako Rais wetu na mama yetu,
Hongera kwa kuendelea na majukumu yako ya kila siku ili kulisongesha taifa letu mbele.

Mama yetu kuna hawa vijana waliosomea mafuta na gesi, waliosomeshwa katika chuo kikuu cha Dar es Salaam kupitia wizara ya nishati kwa fedha za serikali ili wasaidie taifa letu kuinua uchumi wa mafuta na gesi.
Tunakuomba uwakumbuke kwenye ajira mama yetu.

Shahada za mafuta na gesi zilianzishwa mwaka 2013 kupitia wizara ya nishati katika chuo kikuu cha Dar es Salaam.

Hivyo chuo kikuu cha Dar es Salaam kupitia wizara ya nishati kilianzisha shahada ya jiolojia ya Petroli (BSc. Petroleum Geology), shahada ya Kemia ya Petroli (BSc Petroleum Chemistry) na Shahada ya Uhandisi wa Petroli (BSc. Petroleum Engineering). Lakini mpaka sasa vijana wote waliohitimu wapo majumbani hawana kazi za kufanya wala pakujishikiza. Vijana walishakata tamaa kwasababu tegemeo lao kubwa lilikua wizara ya nishati.

Hivyo mama tunakuomba wakumbuke vijana hawa kwasababu hawaoni uelekeo huko wanakokwenda tofauti na zamani ambapo walikua wakipata mawasiliano ya karibu kutoka wizara ya nishati.

Kuna kipindi Wizara ya nishati iliunda Oil and Gesi Professional Data Base ambapo walikua wakiwasajili kila wanaohitimu shahada za mafuta na gesi Tanzania lakini haieleweki hiyo data base iliishia wapi.

Na pia hiyo data base haikufanya chochote ili kuhakikisha wahitimu wa shahada za mafuta na gesi wanaendelezwa bila kuachwa mitaani huku wakiwa na A na GPA kubwa.

Hivyo mpaka mwaka huu 2021 wahitimu wa shahada za mafuta na gesi (Petroli) wapo wapo tu mtaani hawaelewi wanakoelekea.

Ahsante,
Nikutakie majukumu mema.
Mama yetu ni msikivu atalifanyia kazi
 
Hapa ndipo ulipo zingua..KY jelly kitu kidogo? Tengeneza basi utengeneze pesa uache kulia lia humu mitandaoni..pia jua hakuna serikali yoyote duniani yenye uwezo wakuajiri wahitimu wote..jiongeze.

#MaendeleoHayanaChama

Sent using Jamii Forums mobile app
Serikali zilizoshindwa kuajiri hujifichia kwenye hii statement "hakuna serikali yoyote yenye uwezo wa kuajiri wahitimu wote"

Nani kasema iajiri wahitimu wote?
 
Back
Top Bottom