silent lion
JF-Expert Member
- Feb 28, 2012
- 1,161
- 1,535
Mheshimiwa wakati unaingia madarakani , wazanzibari wengi nyoyo zetu zilifarijika kwa jinsi ulivoanza kuchapa kazi.
Ziara yako ya bandarini iliibua matumaini kwamba yajayo ni neema tupu.
Mwaka mmoja sasa tokea ushike madaraka , hakuna kilichobadilika zaidi ya kuongezeka kwa usumbufu wa utitiri wa vitengo bandarini. Yaani kila kitengo sasa hivi kiko bandari ya Zanzibar.
Mheshimiwa nikukumbushe tu Zanzibar ni visiwa vyenye idadi chache ya wakaazi, ambao wengi wao wanaishi katika lundo la umasikini. Hivyo mizigo mingi inayoshushwa hapa Zanźibar huwa kama inapita njia tu kuelekea Tanzania bara.
Kitendo cha kuiwekea vikwazo cha sijui mizigo ikaguliwe na majeshi ya ulinzi au ZAECA (takukuru Ya Znz) ni suicidal move na si tu kitafukuza Wafanya biashara, bali kitaua biashara ambayo tayari iko hoi. Ikumbukwe pia gharama za kuleta mizigo Zanzibar (freight charges) ni kubwa mno kulinganisha na bandari ya Dar, na mizigo hua inachelewa mno kuwasili tofauti na bara.
Mheshimiwa kitendo cha kudharau watendaji wa bandari na TRA na kuwaona kama hawafanyi kazi si cha busara.
Its never too late to mend, you can still save Zanzibar,