jouneGwalu
JF-Expert Member
- Apr 11, 2011
- 2,687
- 1,780
Karibu tena JF mtu mzima HK....
Kumbukumbu zinaonyesha mara ya mwisho ulisusa
Kumbukumbu zinaonyesha mara ya mwisho ulisusa
No response my dear jamaa kachumpa nini, mbona kimyaaaa??????Karibu tena JF mtu mzima HK....
Kumbukumbu zinaonyesha mara ya mwisho ulisusa
wapiga kura hawawezi kuwa na locus ya kuamua kunitaka mimi bila chama changu. hizo ni hadithi za baniani mbaya kiatu chake dawa...na kwa nini wanichagulie chama?wananchi wako wakikuambia kua wako tayari kukupa kura lakini hawaitaki ccm kwa hiyo uhamie chadema..utakua tayari kwa hilo au ni bora usiwe mbunge lakini ubakie ccm?
sijawahi kususa JF, huo si ukweli, mi mbona nipo sana tu hapa?No response my dear jamaa kachumpa nini, mbona kimyaaaa??????
Itategemeana na uamuzi nitakaochukua muda huo ukifika. kwamba nigombee tena ama la? Mimi nina fani ya kazi, nina nguvu na ujuzi wa kutosha, pia nina shughuli nyingi na halali za kunipatia kipato changu cha riziki ya kila siku. sitegemei siasa pekee kama ajira yangu, nikionekana sifai basi nitapumzika, hata hivyo wenye uamuzi wa mwisho ni wananchi wenyewe na wala siyo mtu mwenye lengo la kulipiza kisasi. hivyo kama nitaamua kugombea nitawaomba ridhaa wananchi wenzangu wa Nzega, wakisema natosha nitagombea wakisema hapana umechemsha na haujafanya kitu nitaacha! Huwezi kufanya kazi huku ukihofia kufukuzwa chama, ama kuacha kuteuliwa na chama uchaguzi ujao --- sasa utaishije? Zaidi ya hapo una ahadi gani na Mungu kwamba utafika hiyo 2015? Ishi kama vile utakufa leo na utakuwa huru
hiyo hoja yako inaanzia wapi hapa? Hata hivyo Ulaya ipi unaongelea wewe bana?Nilidhani ina PhD kumbe ni MD ? Wenzako wa fani zako Ulaya hawaitwi na Dr.Hata kama ni MD hadi wawe na PhD wewe kaka vipi ?
Mkuu Dr. Kigwa,Katika post fulani last week mdau maarufu wa hapa JF, ndg PASCO, alitaahadharisha kwamba MB wa CCM ndg Hamisi Kigwangalla (Nzega) hawezi kufanya maandamano akiambatana na wananchi kwa kuwa tayari chama chake wilayani hakimuungi mkono. Kilichotokea ni kwamba maandamano yamefanyika na viongozi wa chama na serikali (inayotokana na chma tawala) waliridhia maandamano hayo na tunashukuru yalifanikiwa na yalikuwa na amani tele. Anayeweza kuzuia maandamano ni polisi (kwa sababu za kiusalama) na si katibu wa chama ambaye alikurupuka kuandika barua bila kujua kanuni na taratibu za kisheria zinazohusiana na maandamano na mikutano ya hadhara. Chama cha mapinduzi hakikatai maandamano, in fact kimetufundisha kuandamana kupinga baadhi ya mambo na hata kuunga mkono baadhi ya mambo na maamuzi yanayofanyika. Mimi ni mwanafunzi mzuri wa siasa za CCM na ninaelewa misingi ya uongozi kama inavyowekwa wazi na CCM kwenye maandiko yake, labda kama mtu aniambie leo hii kwamba Katiba, Kanuni na maandiko mbalimbali ya miongozo ya CCM hayafuatwi tena hapo nitaelewa na pengine nitafikiria sasa kama nina ulazima wa kuendelea kufuata itikadi ya chama hiki ama la!
DR Hamis. Unaposema "mabadiriko ya kweli yataletwa na sisi ...!" unamaanisha nini?
Mbunge CCM aongoza maandamano kumpinga mwekezaji Atiwa Misukosuko | Send to a friend |
Sunday, 17 June 2012 09:26 |
0digg Patricia Kimelemeta, Dar na Shija Felician, Nzega WANACHAMA wa CCM na Chadema wilayani Nzega mkoani Tabora jana waliweka pembeni tofauti zao za kisiasa na kuandamana kwa pamoja kuushinikiza uongozi wa Mgodi wa Resolute kutekeleza ahadi walizoahidi wakati wakikabidhiwa mgodi huo miaka mitatu iliyopita. Maandamano hayo yaliyoanzia Nzega mjini hadi Kijiji cha Nata kilichopo nje kidogo ya mji huo yaliandaliwa na Mbunge wa Jimbo la Nzega, Dk Hamis Kigwangallah. Yalifanyika baada ya wamiliki wa migodi hiyo kushindwa kutekeleza ahadi za ujenzi wa shule, Zahanati pamoja na kutoa ajira kwa wakazi wa eneo hilo. Wanachama wa Chadema walionekana wakiwa na bendera za chama hicho huku wakionyesha ishara ya vidole viwili ambayo hutumiwa na chama hicho kikuu cha upinzani nchini. Pamoja na polisi kutanda kila kona waandamanaji hao waliokuwa na bendera huku wamkitembea kwa miguu na baadhi wakiwa katika magari, waliingia katikati ya kundi la wanachama wa CCM na kuanza kutembea kuelekea katika katika Kijiji cha Mwabangu ambapo ulifanyika mkutano huo. Waandamani hao walikuwa wamebeba mabango yenye ujumbe mbalimbali unaoleza jinsi wasivyotendewa haki na wawekezaji kampuni za uchimbaji madini hasa Kampuni ya Golden Pride ya Nzega. Akizungumza katika mkutano huo, Dk Kigwangallah aliwapongeza viongozi wa Chadema waliomuunga mkono katika maandamano hayo na kuwataka wananchi waendelee kumuunga mkono huku akiahidi kuwaletea mabadiliko makubwa. Alisema kuwa wananchi wanatakiwa kudai haki zao kwa njia ya amani na kuongeza kuwa kilio chao tayari serikali imeshakisia na inakifanyia kazi. "Tumieni njia ya amani kudai haki zetu na sio kudai haki kwa kuvunja sheria, niko pamoja na nyinyi nitahakikisha haki zetu zinapatikana," alisema Dk Kigwangallah. Maandamano hayo yalifanyika chini ya ulinzi mkali baada ya awali Jeshi la polisi kuyazuia, lakini baadaye lilitoa kibali kwa masharti kwamba mkutano ukimalizika wananchi watawanyike mara moja. Awali Dk Kigwangallah wakati akizungumza kwa njia ya simu alisema mpaka sasa wananchi wa eneo hilo wanaishi katika mazingira magumu kutokana na wawekezaji kuchukua mgodi huo,jambo ambalo limesababisha kushindwa kumudu hali ngumu ya maisha. Alisema kutokana na hali hiyo wananchi hao wameandamana ili kushinikiza kutekeleza ahadi walizoahidi ili wananchi waweze kunufaika nayo. Aliongeza, mbali na ahadi hiyo, wawekezaji hao pia waliahidi kusimamia miradi ya maendeleo, ikiwa ni pamoja na kuwapa wananchi maji safi na salama lakini mpaka sasa wameshindwa. Alisema kutokanaa na hali hiyo mgodi huo umezalisha zaidi ya Sh1 trilioni,ambapo jumla ya fedha walizoahidi kutoa kwa wananchi ni Sh3bilioni, ambazo kati ya hizo Sh1.9bilioni kwa ajili ya miradi ya maji, lakini mpaka sasa hawalipi bili ya maji, jambo ambalo linaonyesha wazi kuwa wanatumia kwa ajili ya kulipa fidia ya fedha zao. Kigwangwalah alisema kuwa kutokana na hali hiyo wananchi wanaendelea kutaabika na hali ngumu ya maisha huku wawekezaji hao wakivuna mali bila ya kuwatumia wananchi, jambo ambalo ni kinyume na makubaliano. |
hahahaaa usituchonganishe na PASCO bana. hatukufanya maandamano ili kumkomesha PASCO ama mtu yeyote yule. tulifanya maandamano haya ili kuonyesha mshkamano wetu na machungu tuliyonayo. nimemuweka pasco hapa ili kutia chachu ya mjadala wa hoja ya MB anawajibika kwa wananchi waliomchagua ama Chama kilichompa tiketi! nadhani huu ni mjadala muhimu kwa demokrasia ya nchi yetu na haswa ukizingatia tumo kwenye mchakato wa kuandika katiba mpya!
Kuna mambo kama ya mgombea binafsi, hapa yanapata nafasi ya kujadiliwa sasa na umuhimu wake kuonekana
Mkuu kama hauelewi basi bora uulize kulikokupotosha umma! Kuna aina tatu za ma Dr na wote wanastahiki kuitwa Dr.1 ni mtu yoyote ambae amesoma na kupata Shahada ya Uzamivu yaani PhD yeye anastahiki kuitwa Dr mfano Dr Festus Limbu.2 mtu yoyote ambae amesoma na Shahada ya kwanza ya Utabibu wa Binadamu kama alivyo Dr Kigwa ama Tabibu wa mifugo kama alivyokuwa Hayati Dr Omary Ali Juma wote wanastahiki kuitwa Dr.Aina ya 3 na ya mwisho ni mtu yoyote ambae ametunikiwa Shahada ya Heshima kutoka Chuo kikuu chochote kwa mchango wake mkubwa kwa jamii kama alivyo Dr Jakaya Mrisho Kikwete na wengine wengi tu nao wanastahiki kuitwa Dr. Ni hali tu ya watu wengine kupenda kuwabeza wenzao kitu ambacho si sahihi tujifunze kuwa wavumilivu pindi yule tusiye mpenda anapotoa mawazo yake. Hoja ilikuwa si kumjadili Dr Hamisi bali ni maandamano aliyoyaongoza naomba wakuu tujifunze kujibu hoja kwa hoja na tukianza kumjadili mtu badala ya hoja aliyoileta basi tutaonekana ni dhaifu na tuna nia ya kumchafua mtu tu!Nilidhani ina PhD kumbe ni MD ? Wenzako wa fani zako Ulaya hawaitwi na Dr.Hata kama ni MD hadi wawe na PhD wewe kaka vipi ?
Katika post fulani last week mdau maarufu wa hapa JF, ndg PASCO, alitaahadharisha kwamba MB wa CCM ndg Hamisi Kigwangalla (Nzega) hawezi kufanya maandamano akiambatana na wananchi kwa kuwa tayari chama chake wilayani hakimuungi mkono. Kilichotokea ni kwamba maandamano yamefanyika na viongozi wa chama na serikali (inayotokana na chma tawala) waliridhia maandamano hayo na tunashukuru yalifanikiwa na yalikuwa na amani tele. Anayeweza kuzuia maandamano ni polisi (kwa sababu za kiusalama) na si katibu wa chama ambaye alikurupuka kuandika barua bila kujua kanuni na taratibu za kisheria zinazohusiana na maandamano na mikutano ya hadhara. Chama cha mapinduzi hakikatai maandamano, in fact kimetufundisha kuandamana kupinga baadhi ya mambo na hata kuunga mkono baadhi ya mambo na maamuzi yanayofanyika. Mimi ni mwanafunzi mzuri wa siasa za CCM na ninaelewa misingi ya uongozi kama inavyowekwa wazi na CCM kwenye maandiko yake, labda kama mtu aniambie leo hii kwamba Katiba, Kanuni na maandiko mbalimbali ya miongozo ya CCM hayafuatwi tena hapo nitaelewa na pengine nitafikiria sasa kama nina ulazima wa kuendelea kufuata itikadi ya chama hiki ama la!