Kwako Ndg. Pasco: Maandamano Yamefanyika Bila Idhini ya Katibu wa Chama! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwako Ndg. Pasco: Maandamano Yamefanyika Bila Idhini ya Katibu wa Chama!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by HKigwangalla, Jun 18, 2012.

 1. HKigwangalla

  HKigwangalla Verified User

  #1
  Jun 18, 2012
  Joined: Feb 6, 2008
  Messages: 717
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  Katika post fulani last week mdau maarufu wa hapa JF, ndg PASCO, alitaahadharisha kwamba MB wa CCM ndg Hamisi Kigwangalla (Nzega) hawezi kufanya maandamano akiambatana na wananchi kwa kuwa tayari chama chake wilayani hakimuungi mkono. Kilichotokea ni kwamba maandamano yamefanyika na viongozi wa chama na serikali (inayotokana na chma tawala) waliridhia maandamano hayo na tunashukuru yalifanikiwa na yalikuwa na amani tele.

  Anayeweza kuzuia maandamano ni polisi (kwa sababu za kiusalama) na si katibu wa chama ambaye alikurupuka kuandika barua bila kujua kanuni na taratibu za kisheria zinazohusiana na maandamano na mikutano ya hadhara. Chama cha mapinduzi hakikatai maandamano, in fact kimetufundisha kuandamana kupinga baadhi ya mambo na hata kuunga mkono baadhi ya mambo na maamuzi yanayofanyika.

  Mimi ni mwanafunzi mzuri wa siasa za CCM na ninaelewa misingi ya uongozi kama inavyowekwa wazi na CCM kwenye maandiko yake, labda kama mtu aniambie leo hii kwamba Katiba, Kanuni na maandiko mbalimbali ya miongozo ya CCM hayafuatwi tena hapo nitaelewa na pengine nitafikiria sasa kama nina ulazima wa kuendelea kufuata itikadi ya chama hiki ama la!
   
 2. Kiganyi

  Kiganyi JF-Expert Member

  #2
  Jun 18, 2012
  Joined: Apr 30, 2012
  Messages: 1,244
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 3. Kiganyi

  Kiganyi JF-Expert Member

  #3
  Jun 18, 2012
  Joined: Apr 30, 2012
  Messages: 1,244
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Tunaomba picha Muheshimiwa sana HK au link tunazoweza ona kilichojili huko Nzega....!!!
   
 4. Power G

  Power G JF-Expert Member

  #4
  Jun 18, 2012
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 3,911
  Likes Received: 88
  Trophy Points: 145
  Hongera mheshimiwa kwa kuonyesha msimamo wako wa kuwatetea wapiga kura wako, ingawa hukumu yako itakuwa kwenye uteuzi ndani ya ccm 2015. Tambua kwamba hakuna watu wenye tabia ya kulipa visasi kama viongozi wa ccm.
   
 5. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #5
  Jun 18, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Hii mbona amerecord akiwa nyumbani kwake...au aliandamana yeye na mke wake? tuwekeeni picha za hayo maandamano.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 6. HKigwangalla

  HKigwangalla Verified User

  #6
  Jun 18, 2012
  Joined: Feb 6, 2008
  Messages: 717
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  Itategemeana na uamuzi nitakaochukua muda huo ukifika. kwamba nigombee tena ama la? Mimi nina fani ya kazi, nina nguvu na ujuzi wa kutosha, pia nina shughuli nyingi na halali za kunipatia kipato changu cha riziki ya kila siku. sitegemei siasa pekee kama ajira yangu, nikionekana sifai basi nitapumzika, hata hivyo wenye uamuzi wa mwisho ni wananchi wenyewe na wala siyo mtu mwenye lengo la kulipiza kisasi. hivyo kama nitaamua kugombea nitawaomba ridhaa wananchi wenzangu wa Nzega, wakisema natosha nitagombea wakisema hapana umechemsha na haujafanya kitu nitaacha! Huwezi kufanya kazi huku ukihofia kufukuzwa chama, ama kuacha kuteuliwa na chama uchaguzi ujao --- sasa utaishije? Zaidi ya hapo una ahadi gani na Mungu kwamba utafika hiyo 2015? Ishi kama vile utakufa leo na utakuwa huru
   
 7. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #7
  Jun 18, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Umemkomesha Pasco....
   
 8. HKigwangalla

  HKigwangalla Verified User

  #8
  Jun 18, 2012
  Joined: Feb 6, 2008
  Messages: 717
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  LOL hahaha
   
 9. nashy

  nashy JF-Expert Member

  #9
  Jun 18, 2012
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 679
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Haya wewe andamana tu Nepi atakushukia huko, au Wasira na Werema hawakupata taarifa, je intelejensia ya Mwema ilikua likizo? Au inafanya kazi Chadema tu? Haya Bashe naye anakupigia tizi, kazi kwako said
   
 10. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #10
  Jun 18, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Hakikisha unapigania sheria ya mgombea binafsi inapitishwa vinginevyo hutabebwa kama ulivyo bebwa mwaka juzi....
   
 11. nashy

  nashy JF-Expert Member

  #11
  Jun 18, 2012
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 679
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  ila nakupa hongera maana umethubutu, umeweza songa mbele watumikie wananchi wako
   
 12. HKigwangalla

  HKigwangalla Verified User

  #12
  Jun 18, 2012
  Joined: Feb 6, 2008
  Messages: 717
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  hahahaaa usituchonganishe na PASCO bana. hatukufanya maandamano ili kumkomesha PASCO ama mtu yeyote yule. tulifanya maandamano haya ili kuonyesha mshkamano wetu na machungu tuliyonayo. nimemuweka pasco hapa ili kutia chachu ya mjadala wa hoja ya MB anawajibika kwa wananchi waliomchagua ama Chama kilichompa tiketi! nadhani huu ni mjadala muhimu kwa demokrasia ya nchi yetu na haswa ukizingatia tumo kwenye mchakato wa kuandika katiba mpya!
  Kuna mambo kama ya mgombea binafsi, hapa yanapata nafasi ya kujadiliwa sasa na umuhimu wake kuonekana
   
 13. DALLAI LAMA

  DALLAI LAMA JF-Expert Member

  #13
  Jun 18, 2012
  Joined: Jan 31, 2012
  Messages: 8,617
  Likes Received: 401
  Trophy Points: 180
  Kigwa toka upigwe mkwara kwa kuhisiwa udau ktk mgomo wa akina ULIMBOKA umenywea,husikiki na uwaziri wa afya ume ukosa...TAMAA YA KISIASA IMEKUFANYA UWE KIMYA USIJIHARIBIE.watu typ yako ni hatari bora mara mia mpinzani wako ndg Bashe
   
 14. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #14
  Jun 18, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,326
  Likes Received: 1,792
  Trophy Points: 280
  Nimependa haya maneno yamebanana kweli kweli...Dr. Hamisi Kigwangalla, MD, MPH, MBA! Ndugu mbunge, Kwa bahati mbaya jamaa yule bila kuwa upande wake kisiasa mbona mtihani.
   
 15. Sangarara

  Sangarara JF-Expert Member

  #15
  Jun 18, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 13,048
  Likes Received: 549
  Trophy Points: 280
  DR Hamis. Unaposema "mabadiriko ya kweli yataletwa na sisi ...!" unamaanisha nini?
   
 16. idawa

  idawa JF-Expert Member

  #16
  Jun 18, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 18,537
  Likes Received: 10,458
  Trophy Points: 280
  mh.kigwangala maandamano yenu yalifanikiwa vipi.?
   
 17. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #17
  Jun 18, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Mkuu asante kwa majibu yako ya busara,
  Nilikuwa naamini kuwa wewe ni mwanasiasa kijana mwenye msimamo, mpigania haki za wanyonge, Je nini kilikufanya kutokusaini wakati Zitto anatafuta watu wa kumuunga mkono ili kumuondoa waziri mkuu, hii inawezekana ni kwasababu kulikuwa na tetesi kuwa ulikuwa umepewa unaibu waziri wizara furani ndiyo maana ukawa muoga....
   
 18. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #18
  Jun 18, 2012
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 51,014
  Likes Received: 23,934
  Trophy Points: 280
  Huwa najiuliza watu wa aina ya Kingwangala wanafanya nini CCM lakini sipati jibu.
   
 19. Ilulu

  Ilulu Senior Member

  #19
  Jun 18, 2012
  Joined: Mar 22, 2008
  Messages: 161
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Hongea sana Mh. Kigwangallah naambiwa ulinguruma vilivyo
   
 20. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #20
  Jun 18, 2012
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,633
  Trophy Points: 280
  Hongera umejitahidi sana lakini angalia warasimu wa chama chako watakushukia au umesahau Selelii alifanywa nini ?.
   
Loading...