Kwako mwenyekiti wa chama CCM

jogi

JF-Expert Member
Sep 25, 2010
25,558
25,322
Mtukufu Rais Dr. J. P Magufuli, Kwa kuwa wewe ndio mwenyekiti wangu nalazimika kukuuliza maswali ambayo naamini hutayachukia.

Wote tunayo kumbukumbu kuwa salamu ya chama chetu cha mapinduzi ilikuwa hivi:-

-Kidumu chama cha mapinduzi,
-Zidumu fikra za mwenyekiti wa ccm
-Idumu siasa ya ujamaa na kujitegemea.

Japo salamu hii bado inaonekana kuwa na ushawishi miongoni mwa wanachama na wananchi kwa ujumla, haikutolewa taarifa rasmi kwamba nini kilisababisha salamu hii pendwa kwa chama ikaacha kutumika.

Kwa kuwa umeshika hatamu za chama, ni vema sasa ukalitolea ufafanuzi jambo hili.
.....kwanini chama cha mapinduzi kisidumu!!!!

Hii "fikra ya mwenyekiti" imepoteza uhalali wa kudumu???

Siasa ya ujamaa unaisemeaje, bado inatekelezeka? Kama ndio utaifanya itekelezekeje kwenye mfumo wa utitiri wa vyama!!!

Kama hutajali utupe mwongozo pia kuhusu siasa ya nchi yetu, kuna wakati fulani enzi za mwalimu ilikuwa haifungamani na upande wowote! je hali bado iko hivyo hivyo??

Najua maswali haya hutayajibia humu ukumbini, lakini najua utapewa microphone useme na hadhira siku yoyote popote ndani ya mipaka ya nchi yako, hapo hapo chomekea majibu ya maswali haya.

Kwa sasa sisi tunaendelea kuyajadili maswali haya na makada watiifu wa chama ndani ya JF watatetea hoja.
 
Naona bado inafanyiwa kazi na polepole
 
Back
Top Bottom