Kwako Mwenyekiti Freeman Mbowe: Sikia maombi yetu. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwako Mwenyekiti Freeman Mbowe: Sikia maombi yetu.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mbaga Michael, May 24, 2012.

 1. Mbaga Michael

  Mbaga Michael Verified User

  #1
  May 24, 2012
  Joined: Nov 17, 2011
  Messages: 2,914
  Likes Received: 202
  Trophy Points: 160
  Kwako Mheshimiwa Mwenyekiti,


  Natumaini unaendelea vizuri na
  ujenzi wa Chama na Taifa kwa
  ujumla.


  Napenda kutumia nafasi
  hii kukutaarifu kuwa Tar 27 MAY
  2012 tutakuwa na mkutano
  mkubwa utakaowakilishwa na
  Wabunge wetu watano hapa
  Marekani Mirage Hall Maryland.  Taarifa za mkutano huu nina
  hakika utakuwa umezipata kwa
  Mbunge wetu anayeshughulikia
  mambo ya nje ndugu Ezekiah
  Wenje kwa kushirikiana na
  mbunge wetu wa viti maalum
  mama Leticia Nyerere ndio
  waliokuwa wanaratibu. Matarajio
  yetu ni kuwa mkutano huo
  utakuwa na wabunge watano
  akiwemo Mh Zitto Kabwe, Mh
  Ezekiah Wenje, Mh Leticia Nyerere,
  Mh Peter Msigwa na Mh Joseph
  Mbilinyi.  Tumepata taarifa kwamba
  kutokana na mabadiliko ya Ratiba
  Mh Joseph Mbilinyi umemwomba
  abadili ratiba yake ili awepo
  kwenye mkutano mkubwa
  unaotarajiwa kufanyika Jangwani
  Dar es Salaam. Lakini napenda
  kutumia fursa hii pia kukuomba
  sana umruhusu Mh Joseph
  Mbilinyi aweze kuja Kwenye
  Mkutano wetu wa hapa Marekani
  ukizingatia kuna wanachama
  wawili waligharamia kumchangia
  Tiketi ya ndege ili aweze
  kuhudhuria kwenye mkutano
  wetu wa Tar 27 MAY 2012.  Kutokufika kwa Mh Joseph
  Mbilinyi kwa kweli kutaathiri sana
  Shughuli yetu kwa kupunguza
  hamasa kwa vijana wengi
  wanaotarajia kuja kumsikiliza Mh
  Joseph Mbilinyi. Tumemwomba
  Mh Mbilinyi kwa siku tatu tu. Siku
  ya Jumanne ya tar 29 MAY 2012
  atakuwa amesharudi kutoka
  Marekani ili aje kuendelea na
  Shughuli nyingine za kujenga
  Chama.
  Hivyo ni matumaini yangu
  utaitikia ombi letu, kwa kuzingatia
  sababu nilizoeleza hapo juu.  Wako Katibu wa Chadema
  Washington DC
   
Loading...