Kwako Mwanakijiji…Issue uliyoulizia kuhusu sheria ya Pornography et al.

Shadow

JF-Expert Member
May 19, 2008
2,897
671
Wasalaam,


Natumaini unakumbuka vizuri sana kuhusiana na suala ulilowahi kuuliza hapo nyuma kuhusu sheria inayohusiana na masuala ya pornography. Napenda kukujulisha ya kwamba sheria Namba 6 ya mwaka 2008 [Anti Trafficking in Person Act -2008] ambayo imefuta kifungu cha 139A cha makosa ya jinai imeweka bayana hilo suala. Kifungu cha nne cha cheria hii kimeweka bayana kuhusiana na hilo suala.


Kwa kuongezea , vile vile ukisoma vizuri sheria hii, napenda kuwahusia wale walio na wasadizi wa ndani( House Maid) wanaweza kujikuta matatani kama hawa mabinti / wasichana wa kazi wakiamua kutumia sheria hii hasa kifungu kifungu cha 4 kuwafungulia mashtaka ya kuwatumikisha bila ridhaa yao na kadhalika.
Zaidi waweza kuipitia sheria tajwa hapo juu, hapa: http://www.parliament.go.tz/Polis/PAMS/Docs/6-2008.pdf

Note: Naendelea kufuatilia kama waziri husika ameshaitangaza sheria hii kuanza kazi kupitia gazeti la serikali.


Shadow.
 
Back
Top Bottom