Kishimbe wa Kishimbe
JF-Expert Member
- Jul 18, 2013
- 5,023
- 4,831
TAHADHARI: JESHI LA WANANCHI NA UHIFADHI WA MAZINGIRA!
Ili kuepuka kuweka picha za kambi halisi za jeshi (CLASSIFIED) hapo chini nimeweka picha ya mandhari nzuri ya mazingira yaliyohifadhiwa vizuri na kanisa la katoliki kwenye mazingira yanayozunguka 'RETREAT HOUSE' YA 'CATHOLIC CHURCH' kwenye viunga vya 'SAINT AUGUSTINE UNIVERSITY, MWANZA CITY'!
Kwakweli kanisa la katoliki ni mfano mzuri sana wa kuigwa wa uhifadhi wa mazingira ikiwa ni pamoja na misitu ya asili yenye mimea na wanyama walio hatarini kutoweka katika viunga vya jiji la Mwanza, na sehemu nyingine nyingi, kutokana na tishio la shuguli za binaadam!
Fig. 01 Mandhari nzuri kutoka 'catholic retreat house of Nyegezi, Mwanza city'!
Taasisi pekee ya umma, nje ya TANAPA na wizara ya maliasili na utalii, inayojitahidi na uhifadhi wa mazingira ni jeshi letu la wananchi maana si ajabu kukuta kambi zetu za jeshi zikiwa na misitu minene yenye miti mingi ya asili na wanyama na ndege wengi walio hatarini kutoweka kabisa kwenye viunga vinavyozunguka kambi hizo. Si ajabu kupishana na swala, nyani, tumbili na fisi kwenye kambi zetu za jeshi kiasi mtu ukasahau na kufikiri upo ndani ya hifadhi zinazoendeshwa na TANAPA!
Hatari inayozikabili kambi zetu za jeshi ni uvamizi wa raia, ikiwa na pamoja na wastaafu wengi wa jeshi kwenye viunga vinavyozunguka kambi hizo na hivyo kulazimu kambi hizo kuhamishwa maeneo husika na kupisha uvamizi zaidi wa raia na kuhatarisha uhifadhi uliodumu kwa muda mrefu na kwa ufanisi mkubwa!
USHAURI: 1) Kambi zetu za jeshi ziweke mipaka wazi zaidi na ikibidi ziweke uzio madhubuti utakaozuia uvamizi wa makazi na shuguli za kiraia.
2) Kama kambi itahamishwa basi wizara ya ardhi iyakabidhi maeneo husika kwa TANAPA ambayo itakabidhiwa jukumu la kuhifadhi misitu na viumbe waliomo kwa ajili ya utalii wa ndani na maeneo ya umma ya kupumzikia! KUNA HAJA KUBWA SANA YA KUHIFADHI MAENEO MACHACHE SANA YALIYOHIFADHIWA KWA AJILI YA VIZAZI VIJAVYO!