Kwako mkuu mpya wa mkoa wa Dar, Mr Abubakari Kunenge zingatia wosia wa Makonda. Mkoa huu unataka mtu 'kaksi' kwelikweli

wakatanta

JF-Expert Member
Feb 5, 2018
2,593
3,148
Ndugu Kunenge una miaka miwili tu ya utumishi kama RAS, si muda mwingi wala mchache kivile katika kusoma mazingira ya game.

Jiji hili limejaa kila aina ya fitina, uzushi, uongo, umbea, dhulma, utapeli, wizi, ujambazi, uliokwenda shule haswa.

Wapo watakao kwambia wewe ni bora sana wakitaka kukuweka sawa, chunga maneno na ndimi zao, nafikiri unajua Rais Magufuli nini anapenda na kipi hapendi.

Rais Magufuli hupenda mtu anayekwenda na mdundo wake kwa kasi ya ajabu, ukionyesha ubunifu wa hali ya juu katika kutimiza majukumu yako.

Sasa ole wako usahau wosia, hutachukua round nikwambie na utakuwa mkuu wa mkoa aliekaa ofisini kwa muda mfupi sana, ujue uko kwenye darubini kali sana.

Ukiituliza daresalaam ujue umeituliza Tanzania,na utakuwa umelinda uchumi wa nchi, kwani asilimia karibu 80 ya mapato ya nchi yanategemewa na hili jiji, kuruhusu vurugu ni kugusa mboni ya jicho ya Rais Magufuli, imani yangu hilo unalijua.rejea covid 19, speech ya mzee Baba kuhusu lockdown ,alikataa kulock jiji.

Tegemea kujalibiwa na maandamano yasio ya msingi, toka kwa wapima kina cha maji mbalimbali wakiwemo wanasiasa, halafu ulegee.

Ukiharibikiwa ni wewe peke yako,sio ooh Magufuli ni rafiki kipenzi wa baba yangu, hilo halipo, utapimwa kwa kazi na matarajio ya Rais Magufuli.

Nimeona nikupe msisitizo ili ujue unakibarua kizito sana mbeleni.
 
Nimesoma kichwa cha habari tu lakini nacoment. Ni hivi, ukiona unatumia nguvu nyiiiiingi sana kuendeaha familia kwa ubabe na mikwara, ujue huna hekima ya kuongoza watu. Dar na sehemu yeyote ya Tanzania, watanzania ni walewale.

So ukaksi wa Makonda ni kutokana na kukosa hekima ya uongozi, kujipendeza, chuki, kiburi, ubabe na kujiona ana mamlaka makubwa na hekima kuliko anaowaongoza.

Dar kuiongoza ni rahisi sana kuliko Mara kwasababu Dar kila mtu yuko busy na mishe ya kutafuta hela.
 
Nimesoma kichwa cha habari tu lakini nacoment. Ni hivi, ukiona unatumia nguvu nyiiiiingi sana kuendeaha familia kwa ubabe na mikwara, ujue huna hekima ya kuongoza watu. Dar na sehemu yeyote ya Tanzania, watanzania ni walewale. So ukaksi wa Makonda ni kutokana na kukosa hekima ya uongozi, kujipendeza, chuki, kiburi, ubabe na kujiona ana mamlaka makubwa na hekima kuliko anaowaongoza. Dar kuiongoza ni rahisi sana kuliko Mara kwasababu Dar kila mtu yuko busy na mishe ya kutafuta hela.
Kama walivyoongoza kina mzee Meki Sadiq, yaani utafute muafaka na muuza cocaine?
 
Kama walivyoongoza kina mzee Meki Sadiq,yaani utafute muafaka na muuza cocaine?
Ikibidi lazima iwe hivyo. Hata serikali zinatafutaga muafaka na Waasi inapobidi. Rudia kusoma uelewe mada yangu. Kupambana na madawa ya kulevya ni hekima kubwa mno na ni tofauti na kutumia ubabe kufokea kila mmoja mpaka watumishi wa umma waliokuzidi umri.
 
Nakwambia Kunenge ni born town kuliko Makonda.

Ndio maana hata kwenye makabidhiano alikuwa anamwita Makonda " bwana mdogo"

Sema kwa sasa Makonda anamtegemea Kunenge kwa ushauri namna ya kuishi maisha ya pensheni!
Kiumri nani mkubwa? Endeleeni kumpamba, msije sema kaonewa
 
Dar ilikuwa inamhitaji sana Makonda au mtu wa kariba ya zaidi ya Makonda, kuna watu wanahitaji viboko na kushurutishwa ili wafanye kazi hii kwa WaAfrica ni muhimu sana..

Nguvu kazi kubwa saana inazagaazagaa tu Dar hapo, Vijana wanatakiwa watumike sio wanaachwa tu na mission town na michezo ya kijinga isiyo muhimu kwa Taifa masikini..

Taifa masikini hili halihitaji waburudishaji, linahitaji wachapa kazi usiku na mchana na wengine wafie kazini kwa manufaa ya vizazi vijavyo...
 
Back
Top Bottom